Umachinga au Ujasiriamali ni hatua ya kutoka katika uchumi mdogo kwenda uchumi wa kati na baadae uchumi wa juu

UMACHINGA SIO KIPAJI, SIO SIFA, SIO CHEO, SIO KIPAWA | UMACHINGA NI HATUA YA KUFIKIA NDOTO YA KUWA MFANYABIASHARA MKUBWA NDANI|NJE YA TANZANIA
__________________________________________
Niserikali ya kichawi tu ndio inaweza kujisikia fahari mtu kujiita Machinga miaka nenda rudi uje na nimchawi pekee ndio anaweza kujisifia yeye ni mmachinga mzoefu,Umachinga sio sifa wala kipaji ni hatua|daraja la kupita kwenda hatua ya juu zaidi katika kumiliki na kuendesha biashara kubwa,Kila anayetamani machinga aendelee kuwa machinga huyo ni muuwaji wa ndoto za watu hao nani mtu hatari sana kwa Ustawi wa Taifa na Watu wake hasa hao machinga,Akitokea mtu anayetafuta nafuu kwenye Siasa akakwambia wewe Machinga endelea kuwa machinga nitakulinda huyo ni hatari kuliko mchawi na hafai kuwa kiongozi kama anashindwa kukuongoza kwenda kuwa mfanyabiashara mkubwa na anafurahia namna jua linavyoishia mwilini mwako siku kwa siku ili tu siku moja umpigie kura huyo hakufai wewe wala Mungu,

Tanzania inajumla ya Wamachinga 2,335,711 wenye vitambulisho huku wafanyabiashara wakifikia 3.8M,Hii ni sawa nakusema idadi ya wamachinga Tanzania ni 62% ya walipa kodi wote wa nchi hii,Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza wamachinga wapangwe vizuri maana yake watolewe Juani wapeleke kwenye maeneo ambayo watatambulika ( Permanent premises) ili kutimiza ndoto yao ya kuwa wafanyabiashara wakubwa,hapa lazima tumpongeze sana Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan ,Moja ya Sharti kubwa la kupata mkopo toka benki yoyote ya Biashara ni kuwa na eneo sahihi na kufanyia biashara ( business premise ).Nahapa natamani wamachinga mnielewe vizuri nimesema umachinga sio kipaji ni hatua ya ukuaji katika biashara hivyo ni lazima ifike siku Muhitimu huo Umachinga ila kamwe hamuwezi kuuhitimu Umachinga mkiwa Chini pembeni ya Barabara,

Wamachinga wa nchi hii wamefanyiwa sana siasa na imefika wakati wamejiona kama wao ndio wenye turufu ya Siasa na Wanasiasa wa Tanzania badala ya kuwaza zaidi kesho yao katika biashara zao,Leo Machinga akihamishwa kupelekwa mahali patakapoamua kesho yake iliyonjema anahisi kaonewa kwakuwa tu uchaguzi umekwisha,Tunataka viongozi kama Rais Samia wasiojali kesho yao kisiasa ila Kesho ya wamachinga na watoto wao na watoto wa watoto wao,Kama Rais Samia atafanikiwa kuwahitimisha Umachinga hao watu 2.34M maana yake by 2024|25 Tanzania itakuwa na walipakodi zaidi ya 6M na itakuwa rekodi nyingine kwake kwani tangu Uhuru walipakodi wamefikia 3.8M kwenye nchi ya watu 60M,kwa akili za kawaida Watu wanaweza wakadhani machinga wanaonewa kumbe wanasaidiwa kufikia ndoto zao kirahisi, Mwenye masikio naasikie haya,

.........Kazi iendelee .........

VIVA TANZANIA | VIVA SAMIA | VIVA CCM​

View attachment 1937108

Mimi na familia yangu tunamtaka Samia,
Machinga wasaidiwe kuwekwa sehemu sahihi wapate mikopo,
 
Wamachinga watanzani wamelemazwa nakubaliana na wewe,

tena wamechezewa sana

Hawakuwa na wakuwasaidia kufikia malengo yao zaidi ya kutafuta kura tu wakati wa uchaguzi, shame

Machinga badala ya kusaidiwa hata kutafutiwa mikopo wanapewa kadi hazina hata majina yao,

Bank gani itampa mkopo huyu mtu anayefanya biashara barabarani?

Nani atoe malikauli kwa mtu asiye na anuani ya biashara

Wamachinga wa Tanzania wameteseka sana,

Hongera sana Rais Samia tunakupenda sana,

Umetisha sana kiongozi
 
Haha haha hii nchi inawatu aise!

Sasa pesa ya ndege na wamachinga wapi na wapi Mjomba? Au sijaelewa,

Machinga ndio mwekezaji wa kesho, Ndio CEOs waajao, ndio mabilioners wajao,

Kosa kubwa lililofanyika ambalo Rais Samia anaenda kulifuta ni kuwaacha Machinga kuwa adresslessly ,

Bank haiwezi kukupa mkopo wa 2M huku unazurula Mtaani au umekaa pembeni ya barabara, Hii haikubalika kabisa,

Bank wanataka uwe na eneo lako official,

Kitendo cha kuwaacha machinga wakizurula mtaani sio Sifa au tendo la huruma kwao ni kuua ndoto zao za wao kuwa wafanyabiashara wakubwa kesho,

Asante Rais Samia kuwatoa ndg zako wamachinga juani

___________________________________
Machinga ni madalali wa kuuza bidhaa za viwanda vya China huwezi kuza uchumi kwa kuwa mchuuzi.Uchumi unakuzwa kwenye uzalishaji tokana na raslimali tele zilizojaa nchini ambazo hazitumiki sababu ya mipango mibovu ya wanasiasa.
 
..usim-dismiss moja kwa moja hoja ya ununuzi wa ndege na suala la machinga.

..aliyeleta hoja ya ununuzi wa ndege amelenga ktk vipaumbele visivyo sahihi vya serikali ya ccm.

..twende mdogo mdogo. Wamachinga ni vijana waliokimbia KILIMO toka maeneo mbalimbali nchini.

..serikali ingewekeza ktk kuwainua WAKULIMA / WAFUGAJI bila shaka ingepunguza migration ya vijana kuja mjini kufanya umachinga.

..serikali imetumia sh trillion 2 kununua ndege. Wakati huohuo bajeti ya wizara ya kilimo ni sh billion 294. Na zaidi ATCL inaendeshwa kwa hasara mwaka hadi mwaka.

..Maana ya takwimu hizo ni kwamba ununuzi wa ndege toka kwa mabeberu ni sawa na bajeti ya miaka 7 ya wizara ya kilimo.

..Hoja ni kwamba serikali iwekeze kwenye KILIMO na UFUGAJI pamoja na mnyororo mzima wa thamani ya mazao ktl sekta hizo ili vijana wengi wavutiwe kujiajiri huko.
 
SOMA HII POLEPOLE UTANIELEWA
____________________________________
80% ya Watanzani wanategemea kilimo,
58.1 ni wakulima
20% ni wafanyabiashara na makundi mengine,

Mimi nazungumzia hiyo 20% kwani Taifa hili si la wakula pekee,

Wakati unazungumzia kusaidia wakulima zungumzia pia kusaidia wafanyabiashara |wamachinga pia,

Kuwa mmachinga hakukuzui kuwa mkulima pia,

Bajeti ya 294BL kwenye kilimo ni pesa nyingi kwakuwa Serikali haiendeshi kilimo moja kwa moja kama ilivyo TAMISEMI kujenga shule na madarasa,

Wanaoendesha kilimo ni wakulima wao wenyewe,

Sasa mnataka tutenge pesa nyingi kununua nini kwenye kilimo?

Kununua ndege ni jambo jema hasa tunapotaka kukuza utali kwa hii Royal Tour

Mfano mwaka 2018 utalii ulileta jumla ya Tsh 5trilioni ,

Sass hasara ya 153 Bl kwenye 5T ni kitu gani?

TUACHANE NA HISTORIA INASEMAJE TUMUUNGENI MKONO MAMA.
 
Machinga ni madalali wa kuuza bidhaa za viwanda vya China huwezi kuza uchumi kwa kuwa mchuuzi.Uchumi unakuzwa kwenye uzalishaji tokana na raslimali tele zilizojaa nchini ambazo hazitumiki sababu ya mipango mibovu ya wanasiasa.

Nakuelewa japo kila kitu ni hatua, Tutafika tu very soon,

Tumuunge mkono mama
 
Machinga ni madalali wa kuuza bidhaa za viwanda vya China huwezi kuza uchumi kwa kuwa mchuuzi.Uchumi unakuzwa kwenye uzalishaji tokana na raslimali tele zilizojaa nchini ambazo hazitumiki sababu ya mipango mibovu ya wanasiasa.
Nguvu kazi iliyolala ya wamachinga ingeongozwa kutumika vyema, nchii hii ingekuwa mbali kimaendeleo. 80% ya wananchi inayodaiwa ni wakulima Tanzania, imebaki tarakimu tu. Mashambani wamebaki vikongwe, vijana wengi wako kwenye umachinga mijini, na wengine kwenye boda boda na daladala za baiskeli, ambapo miaka ijayo nchi itaagiza mbegu za kiume kutungisha mimba. Joto la ingine na kiti cha baiskeli ni harari kwa afya ya uzazi.
 
Wakoloni wao waliona fursa tele ya nguvu Kazi plus raslimali tele zilizomo wakafanya makubwa.
Tunaongozwa na vipofu, watawala ni kama wapangaji vile awafikirii kuijenga nchi bali kujifisadi binafsi.
 
SOMA HII POLEPOLE UTANIELEWA
____________________________________
80% ya Watanzani wanategemea kilimo,
58.1 ni wakulima
20% ni wafanyabiashara na makundi mengine,

Mimi nazungumzia hiyo 20% kwani Taifa hili si la wakula pekee,

Wakati unazungumzia kusaidia wakulima zungumzia pia kusaidia wafanyabiashara |wamachinga pia,

Kuwa mmachinga hakukuzui kuwa mkulima pia,

Bajeti ya 294BL kwenye kilimo ni pesa nyingi kwakuwa Serikali haiendeshi kilimo moja kwa moja kama ilivyo TAMISEMI kujenga shule na madarasa,

Wanaoendesha kilimo ni wakulima wao wenyewe,

Sasa mnataka tutenge pesa nyingi kununua nini kwenye kilimo?

Kununua ndege ni jambo jema hasa tunapotaka kukuza utali kwa hii Royal Tour

Mfano mwaka 2018 utalii ulileta jumla ya Tsh 5trilioni ,

Sass hasara ya 153 Bl kwenye 5T ni kitu gani?

TUACHANE NA HISTORIA INASEMAJE TUMUUNGENI MKONO MAMA.

..kundi la wamachinga ni lazima lipungue kwani likiongezeka ni tatizo.

..na kundi hilo linapunguzwa kwa kuhakikisha tuna-deal na matatizo kule ambako ndiko chanzo cha wamachinga, yaani vijijini kwenye jembe la mkono, na wafugaji wa kuhamahama.

..kilimo na ufugaji kikiwa kina tija, basi vijana hawatakimbilia kwenye umachinga.

..hatua nyingine ya kupunguza umachinga ni kuweka mazingira wezeshi kwa wamachinga ku-graduate kwenda kwenye daraja la mfanyabiashara mdogo, wa kati, na hatimaye mkubwa.

..Tunaposhauri serikali iwekeze kwenye kilimo/ ufugaji tunamaanisha wakulima wapewe mafunzo, tuongeze skimu za umwagiliaji, kuwe na masoko ya uhakika, kuwe na research ya mbegu bora, usindikaji na uhifadhi mazao uongezeke, etc etc.
 
..kuna la wamachinga ni lazima lipungue kwani likiongezeka ni tatizo.

..na kundi hilo linapunguzwa kwa kuhakikisha tuna-deal na matatizo kule ambako ndiko chanzo cha wamachinga, yaani vijijini kwenye jembe la mkono, na wafugaji wa kuhamahama.

..kilimo na ufugaji kikiwa kina tija, basi vijana hawatakimbilia kwenye umachinga.

..hatua nyingine ya kupunguza umachinga ni kuweka mazingira wezeshi kwa wamachinga ku-graduate kwenda kwenye daraja la mfanyabiashara mdogo, wa kati, na hatimaye mkubwa.

..Tunaposhauri serikali iwekeze kwenye kilimo/ ufugaji tunamaanisha wakulima wapewe mafunzo, tuongeze skimu za umwagiliaji, kuwe na masoko ya uhakika, kuwe na research ya mbegu bora, usindikaji na uhifadhi mazao uongezeke, etc etc.

Nitarudi
 
Mkuu kwa andiko lako hili unamaanisha Biashara sio kitu kizuri,

Ila Kilimo na ufugaji,

Hii si sawa, Nchi lazima iongozwe kwa sekta zote,

Hawa watu 2.34M wakifikia mitaji ya 4M waanze kulipa kodi Taifa litanufaika zaidi,
 
Hayo maneno ni very unscientific na huwezi kuyalinda au kuya defend na data wala takwimu bali labda na ushabiki wa kisiasa! Hiyo pesa ya kununua ndege moja ingefanya nini!? Wamachinga wako dunia nzima hata huko kwenye pesa zaidi ya hizo za ndege moja wapo! Nenda New York wapo, nenda Washington wapo, nenda Cairo wapo na nenda sijui wapi wamachinga wapo!

Na huko ni pia ni "kushindwa kwa sera za CCM"? Wamachinga au Umachinga ni zao la ukosefu wa ajira ingawa inapaswa kuwa a stepping stone to MFANYA BIASHARA na hatimaye TO MWEKEZAJI kwa kutumia mtaji na fursa zilizopo, kuendelea kuwa Machinga miaka nenda miaka rudi ni kuwa FAILURE IN BUSINESS!

Chief, anaweza kuwa hana maneno ya kisayansi kuzingumzia bei ya ndege na kama peaa hizo zingeweza kumaliza tatizo la wamachinga. Sayansi umeikosa katika kutotaja bei ya ndege moja na kiasi cha pesa ambacho kingemaliza nafasi ya umachinga!!

Umesema machinga wako dunia nzima. Sijafika miji yote ya dunia nzima lakini nimefika miwili kati iliyotolea mifano. Nimesikitika sana kuwa umefanya ghiliba. Kwa makusudi umeamua kutambua umachinga bila kueleza mfanano au tofauti za biashara hiyo. Unataka kusema NY au DC (washington ni state) machinga wao wamejenga vibanda mabarabarani? Kuwa wanazunguka mitaani wakiuza bidhaa mkononi hata bidhaa za vyakula na vinywaji? Kwamba kwenye traffic lights ndio maeneo ya masoko yao?? Umesema uongo na sikia aibu!!

CCM italaumiwa kwa sababu ya kuwaita hawa na mama ntilie wanyonge na kuwa wanawapigania. Kumbe wanachofanya ni kuhakikisha hawaondoki ktk kundi hilo kwa kuwatambua kwa vitambulisho na kuwafanya sheria za majiji na miji haziwahusu wao.

Hakuna serikali isiyojiendesha kwa kodi (VAT). Bidhaa zote za machinga ni upotevu wa kodi kwa serikali na serikali makini hufanya bidii kupunguza kundi hilo badala ya kuliwekea mazingira ya kukua. Machinga wa miji mikubwa huruhusiwa kutumia public lands zilizotengwa kwao angalau siku moja katika week (sawa na minada hapa kwetu). Usidanganye kuwa umachinga ni swala la kila siku huko.
 
Rais Samia ni mnyenyekevu | Mpole| anastaha | mpenda watu, | Mpenda maendeleo | mchamungu | Mzalendo wa kweli
 
Chief, anaweza kuwa hana maneno ya kisayansi kuzingumzia bei ya ndege na kama peaa hizo zingeweza kumaliza tatizo la wamachinga. Sayansi umeikosa katika kutotaja bei ya ndege moja na kiasi cha pesa ambacho kingemaliza nafasi ya umachinga!!

Umesema machinga wako dunia nzima. Sijafika miji yote ya dunia nzima lakini nimefika miwili kati iliyotolea mifano. Nimesikitika sana kuwa umefanya ghiliba. Kwa makusudi umeamua kutambua umachinga bila kueleza mfanano au tofauti za biashara hiyo. Unataka kusema NY au DC (washington ni state) machinga wao wamejenga vibanda mabarabarani? Kuwa wanazunguka mitaani wakiuza bidhaa mkononi hata bidhaa za vyakula na vinywaji? Kwamba kwenye traffic lights ndio maeneo ya masoko yao?? Umesema uongo na sikia aibu!!

CCM italaumiwa kwa sababu ya kuwaita hawa na mama ntilie wanyonge na kuwa wanawapigania. Kumbe wanachofanya ni kuhakikisha hawaondoki ktk kundi hilo kwa kuwatambua kwa vitambulisho na kuwafanya sheria za majiji na miji haziwahusu wao.

Hakuna serikali isiyojiendesha kwa kodi (VAT). Bidhaa zote za machinga ni upotevu wa kodi kwa serikali serikali makini hufanya bidii kupunguza kundi hilo badala ya kuliwekea mazingira ya kukua. Machinga wa miji mikubwa huruhusiwa kutumia public lands zilizotengwa kwao angalau siku moja katika week (sawa na minada hapa kwetu). Usidanganye kuwa umachinga ni swala la kila siku huko.
Labda nikupe somo kidogo ya chanzo cha neno "machinga au wamachinga". Jina hili chanzo chake ni USA na Uingereza ambako lugha ya Kiingereza imeshamiri.Neno "machinga au wamachinga" limetoholewa na Kiswahili kutoka neno au maneno ya Kiingereza ya "Matching Guys" yaani wale wanaotembea! Sasa hata hao wa NY au Washington D.C. na huko kwingine ni Matching Guys with their merchandize (bidhaa) mbalimbali hata ikiwa ni FOOD VEHICLE, they are always on the move from one point in the Cities to another! Hiyo ndiyo maana na chanzo cha machinga! Suala la aidha nimesema ukweli au hapana ni suala la uelewa wako ila ukweli ni huo hapo juu, wamachinga wako all over the world and especially in big and upcoming cities and towns kwani huko ndio kwenye wateja wao!

Serikali yoyote duniani lazima ilenge aidha kuwakuza hawa wamachinga from petty traders au wafanya biashara wadogo wadogo (zingatia wadodo wadogo SIYO WADOGO, kuna tofauti kati ya hao wawili!) hadi wafikie kuwa entreprenuers na hatimaye Business people na hadi kuwa Investors! Haya yanawezekana kama walengwa wenyewe wanajitambua na wanakubaliana na nini Serikali yao inawataka wafanye kwa faida yao. Na hiki ndicho kinacholengwa na Serikalia ya CCM. Sijui kama unalielewa hilo au kama unakubaliana nalo - kama ni ndiyo au siyo, basi unahitajika majadala mwingine on this.

Mwisho nikumbushe tu kuwa suala la "umachinga" au "wamachinga" ni dhana ambayo unapoizungumza lazima iendane na suala la mtaji wa mhusika na biashara ya mhusika kwani mtu mwenye bidhaa zenye thamani ya mamilioni ya fedha hawezi kuwa machinga hata kama anafanya biashara hiyo akiwa on the move! Hiyo haiwezekani na hata utaratibu na sheria hazikubaliani na hilo, popote duniani.
 
Brother, you are lost deep in the maze of political hurdles!!! Unazungumzia nadharia mimi nazungumzia kilicho machoni, huenda wewe ni mmoja wa watu wanaoandika mabandiko mazuri kuhusu kukwamua hawa machinga ili wawe wafanyabiashara wakubwa. Ili awe mfanyabiashara mkubwa anahitaji elimu ya biashara (kama sio uzoefu wa miaka mingi) na mtaji. Kikubwa zaidi anahitaji kuwa na sustain faida kutoka kwenye anachofanya, sio kila siku wanaongezeka machinga watatu eneo alipo wakiuza bidhaa zile zile - kama wenye mahitaji wasipoongeza kipato na kuhitaji zaidi au wasipoongezeka, idadi inayoongezeka ya machinga itafanya wasikue (over-supply).

Ni wazi uko knowledgeable, huna integrity au honesty tu. Nimeweka wazi kuwa namna tunavofanya umachinga Tz sio sawa na NY au DC. Umekwepa kwa makusudi (kwa sababu ya kukosa honesty) kuelezea kuwa umachinga huko uko regulated. Umesema hata chakula kiko kwenye food truck. Hapa nyumbani kuna mama ntilie wako juu ya mitaro ya maji machafu! Wako kwenye traffic light stops!! Je uliona wapi NY kukiwa hivo? Ni kwa sababu kuna regulations zinazoonga mambo hayo ambayo sisi hapa kwa kuwa tunawatumia kisiasa (kuwaweka katika kundi la wanyonye tusiotaka watoke) utakuwa bodaboda hahitaji leseni, helmet, wala kuendesha mwendo unaoongoza wenye magari. Mama ntili anauza chakula nje ya mgahawa unaotoa huduma ya chakula pia, na machinga wanaozunguka kutwa wakiuza bidhaa mpaka usiku saa 5 (unaweza kuiita hii ni hardwork, ninaiita sacrifice).

Kwa makusudi hukuzungumzia ukosefu wa mapato ya serikali kupitia VAT. Wakati mwenye duka anakusanya VAT kwa serikali katika manunuzi, mmachinga hafanyi hivo. Kwa hiyo ni sahihi kusema kuongezeka kwa wamachinga ndio kupungua kwa mapato ya VAT kutoka kwa registered businesses. Na matokeo yake ndio haya, Tanzania ni moya ya nchi chache duniani zenye kiwango kinachovuka 15% VAT. Na hapo kilipunguzwa kutoka 20%. Jambo hili ni moja ya sababu zinazofanya biashara zisizoweza kukwepa kodi kulipa sehemu kubwa ya kodi, kwa sababu uwigo wa walipa kodi ni mwembamba hivo kodi zinakuwa juu.

Mkuu, ni wazi hatuwezi kujadiliana kuhusu jambo hili - huenda wewe ni mmoja wanaodhani kuna idadi kubwa ya wafanyabiashara wa kati walikuwa ni wamachinga siku za nyuma. Sijui kama una takwimu hizo zaidi ya kumtaja Bakhresa. Wafanyabiashara wa kati wa nchi hii wamesaidiwa mikopo na mabenki - hawakuwahi kuwa machinga. Sasa wao ndio wanawapa nguvu wa machinga. Hawataki kundi hili liondoke ili wasilipe kodi. Wamachinga wamepanwa upande mmoja na wanasiasa, upande mwengine wakanyabiashara wa kati!! Hawachomoki.
 
Mama anatoa Tsh 23.8BL kwaajili ya elimu bure | Mimi Mama Samia hata akiongoza hadi 2035 ni poa to,
 
Hoja yako ni nzuri kama mtu amelenga kusoma na kutafakari.

#Mama 2025
 
Ndani ya Uongozi wa Rais Samia,
Mahakama huru,
Bunge huru,
NGOs huru
Media huru

TanzaniakwaniSisi tunatakaje?
 
Mwanamke wa kwanza kuhutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa la 76 tangu tupate uhuru ni Mama Samia Suluhu Hassan,

We Proud on you Mama
_________________________

IMG-20210918-WA0036.jpg
 
Back
Top Bottom