Umaarufu wa Wema Sepetu umeporomoka zaidi tangu alipohamia CCM akitokea CHADEMA

Nashindwa kuwaelewa wafuasi wa cdm.. ukienda kwao unafaa.... ukiondoka hufai...hawajitambui kabisa
 
Wakati mwingine hasira hasara Mimi ni mmoja wa watu ambao hawakuamini kuhama kwa Wema kulikuwa kwa dhati. Kilichofanywa na Wema ilikuwa hasira na kilichotokea ni kuizira Ccm.sasa hasira imeisha harafu ndiyo hayo. Kumbuka Wema ni muigizaji pia.
 
Huyu Wema angejikita kusaidia makundi maalumu/ walemavu angekuwa maarufu sana.
Alikuwa na nyota ya kupendwa.

Sasa yeye umaarufu wake ameuwekeza kwenye SIASA za hovyohovyo zinazoambatana na KIKI za kijinga.

Ndiyo maana anadharaulika.
Mungu anisamehe kwa kusema ukweli.
 
Umaarufu wa Wema ungekuwa umeshuka tusingeona unaleta uzi wa kumuhusu yeye,kumbe bi dada bado ni maarufu japo si mwanasiasa...!!!
 
No research no right to speak. Unazungumzia mawazo yako bila tafiti. Hizi ni akili za vijana ambao hawaitendei haki elimu waliyosomea hata kama elimu hiyo wameipata kwa kukariri.
 
Umaarufu wa Wema ungekuwa umeshuka tusingeona unaleta uzi wa kumuhusu yeye,kumbe bi dada bado ni maarufu japo si mwanasiasa...!!!
Huu ni mrejesho wa uchungzi wangu! Mbona Umaarufu wa Magufuli ukishuka huwa unaeletwa hapa au nao wanakuwa wamedanganya huku haujashuka
 
Toka mzee wa 'baby fly back to kili' ampige chini hakika umaarufu wake umeporomoka sana!
 
Wema angejikita kwenye kusaidia jamii mfano watoto walemavu. Kufanya kama anavyofanya Hoyce Temu. Atumie umaarufu wake kuchangisha pesa za kutibu na kuwasaidia ma kundi yanayohitaji katika jamii.
Huo UMAARUFU ndio wamesema HANA tena au UMEPUNGUA au nimeelewa vibaya. Pesa atachanga za nani kwa mantiki hiyo?! Au afanye ile huwa wanaita KOLABO
 
Huo UMAARUFU ndio wamesema HANA tena au UMEPUNGUA au nimeelewa vibaya. Pesa atachanga za nani kwa mantiki hiyo?! Au afanye ile huwa wanaita KOLABO
Angepata manangement nzuri, angeandaa fund rising dinners pia kuomba msaada kwenye makampuni makubwa, hata chama chake na kuwa na kipindi kwenye TV kuonyesha kazi zake na kuhoji wahitaji na walionufaika na msaada wake.
 
Back
Top Bottom