Umaarufu wa Mandela alaumiwe Nyerere

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170


Umaarufu wa Mandela alaumiwe Nyerere

"Mods plse hii mada msiiunganishe kwa sasa"

Hivi karibuni kumeibuka mdahalo kuwa Mandela hastahili umaarufu kiasi hiki kuliko akina Nyerere, Kwame Nkurumah, Sekou Toure etc. Ni mjadala muhimu maana unafikirisha vichwa hasa kwa kizazi cha sasa ambacho wengine pengine hawajui kwamba kuna nchi kama Namibia zilipata uhuru kamili mwaka 1990.

Kwa mara ya kwanza nimelisikia jina la Mandela nilikuwa darasa la pili na baada ya hapo nilikuja kufahamu kuwa this name was everywhere Mchakamchaka, majina ya mabweni, vitongoji, jeshini, redioni magazetini everywhere. Serikali ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kulitangaza jina hili chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere "Maskini mzee huyu hakujua huyu jamaa angekuja kumpiku kwa umaarufu" Ni Nyerere huyuhuyu aliyetuletea hata wimbo wa taifa uliotungwa Afrika kusini kule kule kwa Mandela. Wimbo ambao hata wenye nao waliuimba hadharani kwa mara ya kwanza in October 1989.

Lakini hii haikuwa Tanzania tu jina la Mandela lilipeperuka kila kona ya Afrika as far as Egypt, Ghana, Guinea to name a few. Jina la Mandela likageuka kuwa "symbol" ya ukombozi barani Afrika lakini hii haimaanishi kulikuwa hakuna viongozi wengine ANC au ya kuwa ANC ilianzishwa na Mandela. Ikumbukwe kuwa Mandela alikuwa ni kiongozi muanzilishi wa "Umkhoto we sizwe" (Spear of the nation) kilichokuwa "kikundi cha kigaidi" chenye lengo la ku "sabotage" miundombinu ya serikali ya makaburu ili kuipa presha ya kuingia kwenye meza ya majadiliano. Hivyo basi to any fair- minded person kufungwa kule kwa mandela ilikuwa ni stahili. Kimataifa ikajulikana hivyo na ndiyo maana nje ya Afrika zaidi ya Cuba na Europe's eastern bloc hakuna mahali Mandela alionekana shujaa katika siku za awali za kifungo chake.

Ni Nyerere na wenzake waliopaza sauti ya juu ya mfungwa huyu wakamobilize wananchi wao wakiaambia dunia bila kuchoka juu ya udhalimu wa serikali ya makaburu. Ikumbukwe kuwa

"Tanganyika became one of the first countries in Africa to impose sanctions on South Africa. The majority of countries in the western bloc and all those making up the eastern bloc were first to impose sanctions against South Africa in the 1960s. Only the United States (US) and the United Kingdom (UK) continued their friendly relations with South Africa for much of the 1970s. It was not until the call for sanctions against and disinvestment from South Africa became part of a wider, global political campaign that the US and UK heeded the call for a boycott of the apartheid state."

Lakini je nini maana ya Symbol?

1. Rosa Parks

11akf1z.jpg


"On December 1, 1955, in Montgomery, Alabama, Parks refused to obey bus driver James F. Blake's order that she give up her seat in the colored section to a white passenger, after the white section was filled. Parks was not the first person to resist bus segregation.

Huyu mama pamoja na kuwa activist lakini alikuwa mtu mdogo sana kiupambanaji kulinganisha akina Daisy Bates, Alice Paul, Victoria Woodhull etc.

Umaarufu wa mama huyu haukuishia hapo tu kwani; Kwa wasiofahamu ni kwamba mama huyu alipofariki mwili wake uliwekwa katika state capitol akiwa ni miongoni mwa wamarekani 30 tu, na mwanamke wa kwanza kuwahi kufanyiwa hivyo tangu taifa hilo lianziswe
"Only 30 Americans have been given the honor of lying in state at the Capitol rotunda. Most have been Presidents or war heroes. Rosa Parks, heroine of the civil rights struggle, is the first woman to have this honor"

2. Aung San Suu Kyi
11qiaeq.jpg


An international symbol of the fight against oppression and a unique figurehead for democracy. But, Aung San Suu Kyi -- the woman who took on Myanmar's military rulers armed with little more than the strength of her convictions. Lakini je was and is she alone?

3. Hector Pieterson

14nzgjk.jpg


Hector Pieterson (1963 – 16 June 1976) became the subject of an iconic image of the 1976 Soweto uprising in SA. Inasadikika watu zaidi ya 400 walikuwafa katika hii uprising, lakini kwa nini jina hili moja tu ndiyo maarufu mpaka sasa, na kuna hata museum yake?

Na si hao tu wapo akina Dalai Lama, Malala Yousafzai etc.

Lakini above the symbol status ikumbukwe kuwa kuwa katikati ya miaka ya 80 South Africa reached a boiling point. Hali ilikuwa mbaya kupelekea a civil war. There was just one man who could stop that and this was Mandela na makaburu waliukubali ukweli huo mchungu. It is true kuwa Mandela aliandaliwa kuface uhalisia wa nyakati mpya, sometimes katika siku za mwisho za ufungwa alikuwa akipelekwa downtown Capetown usiku kwa matembezi, alihamishwa kutoka selo hadi guest house. Kwa mtu wa calibre ya Mandela na after that long suffering hivi vilikuwa ni vitu vidogo mno kumfanya abetray watu wake.

The nation was deeply divided, na kulikuwa na vita ya wazulu na makabila mengine ikiendelea in full swing wakati huo. Mandela akatoka jela, watu wengi wamesahau kuwa kulikuwa na miaka mine ya ku-set pace kabla Mandela kuchaguliwa raisi. Mandela alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia hiyo civil war kutokea, lakini pia aliwakaribisha maadui zake kwenye serikali yake. Alishawahi hata kumkaibisha na kunywa nae chai mke wa mwanzilishi wa apartheid (dec.) Akastaafu uraisi baada ya kipindi kimoja tu, nadhani haijawahi tokea Afrika hii.

Hivyo basi suala la umaarufu wa Mandela kuwa umetengenezwa na "wazungu wa magharibi" ni habari ya kizushi maana kama ni umaarufu tulianza kumpa sisi wenyewe waafrika na baadae Eastern Europe na Latin America. Ikumbukwe kuwa hao tunaosema walimpa umaarufu, wengine walimuweka kwenye listi ya magaidi as late as 2008.

Kwa hiyo basi wanaodhani umaarufu wa Mandela umekuzwa na "wazungu wa magharibi" wangeanzia kwanza hapa nyumbani kumlaumu Nyerere. Na waliosahau kuwa memorial service ya Nyerere nayo ilijaa dignitaries mbalimbali kutoka pande zote za dunia wajikumbushe kupitia link hizi. Au naye alikuzwa na wamagharibi?

1. The world turns out to honour Nyerere

2. Dignitaries Pay Tribute to Nyerere

3. Africa, World leaders honour Nyerere


Tuendelee kujadili.......
 
Back
Top Bottom