Umaarufu wa Kikwete upo juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umaarufu wa Kikwete upo juu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zawadi Ngoda, Sep 14, 2009.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ukisoma JF na magazeti mengine unaweza kudhani kwamba, mwaka 2010 Kikwete hawezi kuambulia hata 20% ya kura za watanzania. Lakini hali halisi nchini ni nyingine kabisa. Nimetembelea Mwanza, Lindi,Tabora, Ruvuma, Dodoma, Dar es Salaam na baadhi ya vijiji na kupata picha halisi.

  Nimetembelea vijiji sita, na nikajaribu kueleza jinsi Kikwete alivyowaangusha wakulima kwa ahadi hewa. Vijiji vya Tabora na Ruvuma, walinieleza kuwa wao ni wakulima wa Tumbaku na toka Kikwete aingie madarakani wamesikilizwa sana kwa kuwabana wawekezaji katika eneo hilo. Aidha wale wa Ruvuma walifurahia kuona mwaka jana zao hilo liliongezeka mara mbili, na kila mmoja alihisi tofauti katika mfuko wake. Hali kama hiyo nilielezwa na wananchi wa Tabora. Kifupi katika mikoa yote nilipata majibu ya kuonyesha wanaimani na Rais Kikwete.

  Maeneo ya mijini kulikuwa na majibu mchanganyiko. Kuna ambao hawakujali ni nini amefanya, wao cha muhimu ni chama wanachokishabikia.Kundi hili lilifanya kama asilimia 30. Kuna wengine ambao ni zaidi ya 40% ambao wao hawakufikiria kuwa kubadili chama ni jibu. Wakitoa mfano wa Kenya, Zambia na Malawi na kusema wanamarafiki wengi wanatoka huko na kueleza hakuna mabadiliko yeyote yale kwa mwananchi wa kawaida kiuchumi. Wakithibitisha hayo na kusema, ona wakenya wanakimbilia nchi yetu kama sisi tutakavyo kwenda Ulaya. Mmoja wao alisema "Braza si unasikia kila siku polisi wanakamata Waithiopia, wasomali na wanaijeria". Kama hapa pabaya kwanini waje, Kikwete wetu ni mtoto wa mjini. Katufungulia wamachinga masoko." Hapo sikuwa na neno.

  Huwezi kuamini Kule kijijini nilipoendelea kuleta longo longo kidogo nipigwe, ilibidi nikubaliane nao. Na nilipojaribu kuwauliza kama wanafikiriaje ule waraka wa Kanisa katoliki? Ukweli hawajapata kusikia kitu kama hicho. Nilikuwa nao mkononi waraka huo, na nilijaribu kuwasomea. Hata pragraf moja sikumaliza, kabla sijanyamazishwa na mmoja na kuungwa mkono na wote. "Unajua hayo mambo ya kwenye makaratasi sasa hivi sisi hatuangalii, tunachoangalia ni kama tunapata fedha ya kusomeshea wanetu na pesa kidogo kidogo ya kununu dawa. Haya mambo ya Ufisadi tumeyasikia toka enzi ya fagio la chuma, sijui nani alikuwa Rais." Walinijibu hivyo, na nilikuwa mtiifu nikijua kuwa niliepuka mkong'oto dakika chache zilizopita. Mara moja nikaukunja waraka wa Pengo na kuuweka mfukoni kwa haraka sana.

  Nikiwa hapo Magomeni nilipozungumzia waraka wa Kichungaji kuelekea uchaguzi 2010, nao walinibeza na kusema du hata kanisa nalo linataka kura ill lile. Hapa nikafahamu kuwa waraka unaweza kumpa umaarufu zaidi Kikwete kuliko walivyodhania. Sikuweza kuamini vipi anaweza kuwa maarufu licha ya kutolewa mabomu mengi ya ufisadi. Ni nini hasa mwananchi wa kawaida anapima uongozi bora. Hivi magazeti na JF yawezekana kuwa hawajui wananchi watakacho? Nikapigwa na Bumbuwazi!

  Amini usiamini umaarufu wa Kikwete upo juu sana kuliko aonekanavyo magazetini na katika JF. Ningeviomba vyombo vya habari (magazeti na jf) kuchukua statistic angalau kwa watu laki moja na kuhakikisha haya nisemayo. Cha kuzingatia ni kutochukua hiko kipima joto katika mtandao, badala yake waende kwa wananchi, wapiga kura. Nasema hivi kwasababu kwenye mtandao wengi wapo ughaibuni, hivyo si wapiga kura active.
   
 2. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zawadi,

  Kama sikosei wewe tokea mwanzo uliupinga waraka wa wakatoliki ninavyokusoma humu kwenye JF?? Sasa hii mada uliyotuletea leo hii si ni yale yale!

  Mimi nadhani waraka umeshasambaa na wenyekuelewa wameelewa ambao bado wataelimishwa kwani haya mafundisho yanatolewa na wataalam kutoka hapa Dar jimboni. Madhumuni ya huu waraka ni kufundisha watanzania kuchagua viongozi bora na kupinga ufisadi n.k

  Tupaze sauti wote tukemee ufisadi kwa nguvu na pia tuchague viongozi bora wa kupeleka nchi yetu kwa ajili ya kizazi kijacho.

  Kuhusu JK kukubalika au kutokubalika wewe ulivyokuwa unauliza ulikuwa unatumia vigezo gani? Mimi kwa kuangalia haraka haraka ninaangalia uchaguzi wa Tarime, Busanda, na Biharamulo. Sasa wewe sijui ulitumia vigezo gani?
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,030
  Likes Received: 23,953
  Trophy Points: 280
  Ili ujue hii thread yako ina ukweli au uongo kiasi gani, angalia idadi ya watakaoichangia. All the best.
   
 4. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  UPUPU mtupu!
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Issue siyo umaarufu wa kuuza sura, tunataka utekelezaji.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Acha umbea.....
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  I like the heading wengine tukisoma neneo juu tunajua ni mbinguni. Kwa maana hiyo umaarufu wake hauko kwa waliomchagua bali uko juu mbinguni sounds true and strange.

  Wananchi waliwabana wawekezaji, unaongelea toka duniani au Tanzania? Mwananchi wa tanzania unamjua wewe, hajui kabisa umombo watabanaje mwekezaji anayeongea kimombo, kiswahili chao cha shida mkalimani ni jamaa mmoja mjanja mjanja wasiasa ambaye ana udalali wake wa kutakata unategemea atamsaidia mwananchi kumbana mwekezaji?

  Tofauti ya mifuko yao pressumably ya suruali kwa manaume na kwenye sidiria kwa wanawake, hii siwezi kubisha kabisa uko sahihi, Kama mjini pochi zimekonda kama zina virusi kijijini utategemea nini tofauti wanayoisema ni negative/downward difference and not otherwise.Wangekuwa na hela nyingi kiasi hicho unadhani kungekuwa na urban migration ya kiasi hicho. Waje mjini kufanya nini tegeta posta saa mbili nzima anayeenda bara amefika moro wao wanalala kwenye DCM

  Maeneo ya mjini: hawa ndo wale wanaojiita wajanja, hawajajiandikisha hawapigi kura wala nini wao asubuhi mpaka jioni kubangaiza hata ukiwauliza simple quesion kuhusu tanzanian politics atatoa macho, wanachojua ni kuwa tanzania sasa hivi life iko tough shauri ya mafisadi na sio economic recession. Ni kweli ajira zimetolewa kwa wamachinga, kuuza vocha juani na katikati ya barabara ( mungu usiwafungue macho wawekezaji walete auto vending machines) kuendesha bajaj ( auto rickshaw) pikipiki za miguu miwili toka china ( hospitali ya moi imezidiwa na wagonjwa kama unabisha kaangalie) ajali kila dakika na mwisho madalali wa viwanja na wapiga debe stendi hao ndo walioulizwa na ndio wakatoa tofauti ya kenya na tanzania sio sober person.

  Kijijini nilipoendelea kuleta longolongo kidogo nipigwe watanzania si mabwege tena walijua unawasanifu hali yako haikuwa ya mwanakijiji wa kweli, labda hujaonekana ( assuming huko ni kwenu) kwa karibu miaka 20 halafu unasema maisha mazuri hata asiye na akili zitarudi ghafla na atakupiga, wanajua ufisadi upo lakini unachekelewa, ndio hasira zao.

  Magomeni wao wana akili sana "kanisa nalo linataka kura ili lile" very thoughtful of them, poor you, you underestimated their thinking. Anayetaka kura sio kwa ajili ya kujenga nchi bali kwa ajili yake mwenyewe hivyo wanaona individualas hawawasaidii labda institutions kama kanisa ambazo zimeshare nao problems kwa kuwapa elimu, dawa na chakula angalau kwa bei poa pale kinapohitajika.

  Wapiga kura hapa sitii neno zaidi ya kusema mabadiliko makubwa yanahitajika kwa mfano katiba mpya, watanzania waishio nje wapige kura, wagombea binafsi nafasi zote,waruhusiwe tume huru ya uchaguzi, iliyo na uwakilishi wa vyama vyote na mashirika yasiyo ya kiserikali ( NGO) uandikishaji makini wa wapiga kura, jinsi ya kuharibu shahada za wapiga kura na wananchi wapewe elimu ya uraia yakiwa ni baadhi tu ya mambo wa msingi kuangaliwa.
   
 8. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Zawadi nimemshauri siku nyingi kuwa apunguze muda wa kutazama aljazeera ili atumie muda wake kuongea na watanzania wote na sio tu wa magomeni (ambao wana akili sana kwa mtazamo wake).
   
 9. m

  magagana New Member

  #9
  Sep 14, 2009
  Joined: Sep 12, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  loliondo nako yupo juu? acha sihasa zako
   
 10. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  Zawadi Ngoda, molimoli mkwamisi: Nakumbuka hoja yako ya jana, naona umeachana nayo kabisa leo. Hata hivyo nimekupata vizuri, bila shaka unatokea kitengo cha Tabwe Hiza pale Lumumba. Mkuu njaa njaa ziangalie sana, zitatupeleka pabaya.
   
 11. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Genius!!
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Niliziona mbio na issues hapa then gear ikawa kwa waraka, ukamgeukia Pengo na sasa umeonyesha true colour yako si mbaya.

  Hapa ni JF, mkitumwa baada ya maelekezo basi get back your common sense na waulizeni maswali kabla hamjaja hapa. Kuhimili mikiki ya JF inatakiwa utulie.

  Haya wacha tuendelee kuona umaarufu ila kwa uhakika saa hata watu wa kijijini kwangu wamejua Kikwete hakumaanisha alicho sema na kaipa CCM wakati mgumu sana.
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Sep 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Umaarufu wa JK (kama upo) unatokana na ignorance na kutofuatilia mambo (indifference) kwa watz walio wengi. Ingekuwa nchi nyingine Rais anayedai hajui sababu ya umaskini wa nchi yake angeshapinduliwa siku nyingi! Kwa sasa tuendelee na utulivu na amani wakati tunamsubiri Rais ajaye asiye msanii!
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Sep 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Zawadi ukiondoa chuki ulizonazo dhidi ya kanisa katoliki (ambazo umezionyesha mara kwa mara kwenye thread na post mbalimbali) tujulishe ni sehemu gani ya waraka usiyoipenda (kwa sababu yoyote ile) au kuielewa ili tuelewe kampeni zako dhidi ya waraka wa kanisa katoliki (mwongozo wa waislamu inaonekana sio issue kwako) zinalenga nini?
   
 15. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,577
  Likes Received: 925
  Trophy Points: 280
  Ndiyo!Umaarufu towards negativity.
   
 16. W

  Wincheslaus New Member

  #16
  Sep 14, 2009
  Joined: May 10, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli utabaki palepale kwamba, umaarufu wa Kikwete bado upo juu. Kwa wananchi ambao tuko mawilayani, hatuwezi kupotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari, au baadhi ya watu wanaomponda Rais wetu KIKWETE! Yeye ni mtu wa watu na mwenye nia safi kwa Watanzania wote, labda tu baadhi ya ya watendakazi wake, hawawatimizii wananchi kile kinacholengwa na Rais wetu, na hivyo watu wengine kuona umaarufu wake umepungua. Mwenye upeo wa kuona mbali atakubaliana na mimi, kwamba Rais wetu ameshatimiza ahadi zake nyingi alizotuahidi na inabidi yote ya mema, tumshukuru kwa jitihada zake, na sio kuraumu kila mara. Kikwete kama si utaratibu wa katiba ya nchi yetu, bado anahitajika kwa kipindi kisichopungua miaka 15. Naviomba vyombo vya habari muda wote, kutoa sifa za ukweli pale inapobidi na si kufuata kauli za watu wasiopenda mema kwa kupindisha ukweli.
  Bashungwa- KAGERA
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kaka wewe umeletwa humu kwa kazi moja tu ? Ujisemee wewe mwenyewe wilayani kwako sisi yuko wilaya zingine the guy hafai na watu wanasema openly na hada kule mnako dhani mmewekeza kura zenu .Ngojeeni cha moto .
   
 18. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Haya na tuangalie!!!!!!
   
 19. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ni kweli baadhi ya maeneo kama Mbeya,moshi na maeneo hayo uliyoyataja hana wakati Rahisi. Lakini hata huko ulikokutaja ukweli tofauti za kura hazikuwa kubwa sana kati ya mgombea wa Wapinzani na CCM.

  Hata hivyo napenda kukukumbusha kwamba, uchaguzi wa wabunge na wa uraisi katika Tanzania yetu ni tofauti sana. Ukiangalia uchaguzi wa 2005 hata maeneo yale ambayo wabunge wa upinzani walichaguliwa, bado sehemu nyingi ni Kikwete ndio alipata kura nyingi kuliko mgombea wa Urais wa upinzani wa chama ambacho mbunge wake kachaguliwa.

  Kuna sehemu walimwambia wazi wazi kuwa hatuna matatizo nawe, ila huyu mbunge wenu wa CCM hatumtaki. Hii inaonyesha wazi kuwa kuchukua matokeo hayo ya chaguzi ndogo kama kigezo, tunaweza tukawa si sahihi. Na ndio maana nimeviomba vyombo vya habari viwe makini au specific kwenye vipima joto vyake. Kama unahitaji kujua juu ya mbunge chukua kipima joto cha mbunge, halikadhalika kwa Rais.

  Waraka wowote utokao nje ya serikali naupinga, kwa sababu naamini kabisa kuwa kesho na kesho kutwa hata mimi Zawadi Ngoda nitataka kutoa wakwangu. Kumbuka hatuna sheria inayokataza kutoa nyaraka kama hizo toka Taasisi, mashirika ya dini, NGO au watu binafsi. Mimi nafikiri wakati umefika sasa hivi kuwa na sheria hiyo.
  Kwa wale wanaofikiri kuwa ninachuki na kanisa katoliki, napenda kuwatoa wasiwasi kabisa, kuwa sina chuki na kikundi chochote kile ikiwa pamoja na kanisa katoliki. Tatizo kubwa la wenzetu katoliki, ni kudhani kuwa kanisa hilo halifanyi makosa. Hivyo klikosoa kanisa katoliki ni sawa na kuwatukana wakatoliki. Hayo yalikuwa ulaya miaka ya 1950, sasa sisi lazima tujifunze kutokana na makosa. Katika thread zangu zote nimerudia tena na tena kuwa napinga waraka wowote ule utokao nje ya serikali.
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Too easy to predict, huna la ziada ,mnapenda kupamba hata pasipopambika mwambieni ukweli ili arekebishe mambo ,Wilaya zipi unazosema zile ambazo treni linapita baada ya miezi mitatu ili wanachi wapate usafiri,au zile ambazo shule zake za msingi zina mwalimu mmoja tu kwa miaka minne iliyopita au zile wanawake kumi wanakufa kila siku kwa vile hakuna mganga au muuguzi kwenye zahanati,au zile ambazo waarabu wamepewa vitalu na wananchi wanachomewa nyumba zao au zile wakurugenzi wanakula pesa za watoto yatima zilizotolewa na serikali labda wilaya yako sisi wilayani kwetu ummarufu wake umeshuka kwa kasi mno hakuna anayetaka kuona anatawala tena
   
Loading...