Umaarufu wa Chadema wapungua (Gazeti la Tazama) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umaarufu wa Chadema wapungua (Gazeti la Tazama)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Revolutionary, Apr 23, 2011.

 1. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna mikakati ya muda mrefu na ya muda mfupi kwa vyama vya siasa kuwin washabiki na wanachama wengi kipindi fulani!

  Hapa kuna long term strategies na short term strategies ikitiegemeana na haswa ideology ya viongozi wa chama. Ideology nzuri ni zile zinazohusisha mchanganyiko
  sahihi wa long term na short term strategies kwa wakati na mahala pale.

  Mikakati ya muda mrefu (Long term strategies) huwa imara na very effective kama itakuwa engeneered na futuristic leaders wenye mitazamo (vision) iliyoyukuka (kama Mwl Nyerere. Mikakati hii ya muda mrefu huleta ukombozi kweli na unaodumu kwa muda mrefu (kama utapata ushikiano wa kutosha). Hii huhitaji viongozi thabiti (a bit dictating) kufikisha nchi wanakodhamiria, Mfano mzuri kwa Afrika ni Rais Paul Kagame wa Rwanda au kidogo Rais Mkapa (kwa alivyokuwa na mtazamo wa kupunguza deni la Tanzania hadi mwaka 2001 Tanzania ikaqualify kusamehewa deni la USD 3 billion Kinyume na sasa.

  Hata hivyo viongozi wengi wenye mlengo huu hutokea kutopendwa sana kutokana na wao kutoleta mabadiliko ya haraka haraka ambayo watu hupenda kuyaona na kutokana na kuwa wababe kiasi fulani.

  Viongozi wengine wengi kwa kutopenda complication na kutaka kufurahisha furahisha watu ili wapendwe fasta fasta mfano mzuri ni Rais Kikwete na Ideology yake ya Liberal Populist na mikakati yake ya danganya toto (quick win) ambayo huwa haidumu, najua mnakumbuka, mikakati yake iliyokuwa na slogan kama "Kasi mpya Ari mpya, Nguvu mpya", "Maisha bora kwa kila mtanzania", Mabilioni ya Kikwete, ahadi zake kama ile ya Ajira Millioni ambazo zilimfanya apendwe na KUSHINDA KWA KISHINDO, lakini sasa zimemgeukia na Kuponea chupuchupu kugalagazwa katika uchaguzi uliopita. KWA MTAZAMO WANGU BINAFSI, MIKAKATI NA AHADI ZA DANGANYA TOTO AMBAZO ALISHINDWA KUZIDELIVER NDIO CHANZO CHAKE KUFANYA VIBAYA UCHAGUZI ULIOPITA kinyume na CCM wanavyotafuta Mchawi wao nje ya chama hicho na kuanza kuvua magamba bila matarajio mazuri.

  Nina hakika kama Kikwete angekuwa na mikakati sahihi ya kudumu na angetimiza ahadi zake angeendelea kupendwa despite vijembe vya Chadema na hayo wanayowasingizia JF na mahasimu wao wengine!

  CHADEMA NA MIKAKATI DANGANYA TOTO (Quick win Strategies!)
  Hivi Karibuni CHADEMA wametokea kupendwa na watanzania wengi. Hii inatokana na na sera mikakati inayowavutia wengi. Kwa mtazamo wangu ni kwamba NYINGI YA SERA NA MIKAKATI YA CHADEMA (except Katiba na mingineyo) NI YA MUDA MFUPI INAYOENDANA NA KUDANDIA DANDIA HOJA NA KUIBUA HOJA NA MASUALA (HOT ISSUES) MBALIMBALI YALIYOMAARUFU KWA WAKATI FULANI TU!

  Tunaweza kuona mifano katika hoja nyingi za maandamano, zile zinazoibuliwa na viongozi hao na baadhi ya zile zinazopelekwa Bungeni, mfano baadhi ya Hoja mpito za Mh Mnyika (kuhusu NSSF na nyinginezo) na wengineo pamoja na mkakati wa kuidhoofisha CCM. Nawapongeza kwa ujasiri na uthubutu wa katika kuibua ishu mbalimbali bila woga.

  Lakini angalizo ni kwamba hoja na mikakati mingi ni ya kufanya CHADEMA kipendwe tu kwa wakati fulani (wakati huu) na kuna hatari ya chama kupoteza wapenzi na washabiki kwa in a long term na haswa kama CCM itajizatiti na kuanza kuwajengea imani watanzania.

  NINI KIFANYIKE.
  1. Nashauri pamoja na mikakati hii danganya toto, CHADEMA wawe na waendelee kuwa na mikakati mikubwa ya mtazamo wa mbali wenye lengo la kuikomboa Tanzania kiuchumi na muda mrefu ambayo nguvu zao zote na matendo yote ya kila siku yataelekezwa kufikia lengo hilo kuu, Lengo ambalo liwe wazi na waweze kulidefend watakapokuwa critisized na wapunguze kutumia nguvu nyingi kwenye mambo yasio na matokeo ya muda mrefu.[ni kazi ya Chadema kutafsiri ushauri huu katika vitendo, so I wont dictate what to do]
  2. Viongozi na wanachama na hasa wabunge wawe waangalifu, waadilifu na makini na madaraka yao na siku zote wafanye maamuzi sahihi hata kama yatawachukiza marafiki zao wa Muda Mrefu!
  3. Chadema wasikae tu kutetea hoja au kutekeleza tu "POPULAR ISSUES" kwa wakati fulani bali wakae na watende mambo kimtazamo.
  4. viongozi wakubali kwamba kazi nzuri walioianza hawataweza kuikamilisha peke yao yawapasa wawaandae vijana watu (vijana) thabiti na makini watakaoendeleza mapambano kwa nguvu zaid na zaid.

  4 Chadema wawe watiifu na wanyenyekevu kwa waliowachagua na Watananzania ili watu waendelee kuwa na imani na Chama na mikakati yao.

  NAJUA WADAU MNA MICHANGO MINGI ZAID YA HII.

  Bila mikakati ya Muda mrefu, yenye mitazamo thabiti ya kuitoa Tanzania kutoka A kwenda B intakuwa ni kazi sana CHADEMA kushika Madaraka ya Serikali na haswa kama CCM itajirekebisha na kurudi kwenye reli kwa kurudisha uadilifu na uwajibikaji! The Mighty CCM Machinery is has all the advantage!

  AND MIND YOU,RAIA NI OPPORTUNISTIC IN NATURE! WATANZANIA WASIJE WAKAWATAFINA CHADEMA MKAISHA UTAMU WAKAWATEMA KAMA BIGJII! kama wanavyotaka kuifanya CCM sasa!

  Otherwise CHADEMA IS JUST ANOTHER "BUBBLE GUM POLITICAL PARTY" [kama nyimbo za bongo fleva (not hip hop) zinazotoka leo kesho tunazisahau tunapenda nyingiine....
   
 2. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Time Will Tell
   
 3. T

  Technology JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  you are using very long sentences explain small things, In short nadhani ungependa nchi hii itawaliwe na JESHI au????
   
 4. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jeshi is not on the list mkuu, mapendekezo yangu kwa Chadema yako wazi na ni kwa heri si shari.
   
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kama Bubble Gum Political Party inaweza kumlazimisha Rais akaagiza be ia sukari ishue,then let it remain a permanent bubble gum party.Na kama inaweza kusaidia muswada fyongo wa mabadiliko ya katiba urejeshwe kwa waliouandaa,then let it remain chama cha big jii.

  Ni ulevi kufikiria masuala ya muda mrefu wakati watu wana njaa,wanahitaji kula next day or even the same day.Njaa haisubiri ideology.Tumbo linahitaji chakula.Ukiwa na kansa husubiri i-develop ndio uanze kuishughulikia.Inahitaji kukabiliwa papo hapo.

  Mikakati ya muda mrefu ni muhimu,lakini kwenye dharura kunahitajika mikakati ya muda mfupi-na hata ikibidi ya papo kwa hapo-ali mradi kila Mwananchi ajisike kuwa hajalaaniwa kuzaliwa katika nchi iitwayo Tanzania.

  Busara kidogo tu zingeweza kukupa mfano wa namna nchi mbalimbali duniani,zikiwemo mataifa makubwa kama US na UK zinavyoshughulikia kuyumba kwa uchumi wa dunia.Kuna mikakati ya muda mfupi kuhakikisha uchumi wa nchi husika hauelekei shimoni,na mikakati ya muda mrefu kuhakikisha kilichotokea hakirejei tena.In your view labda ungependa kuona nchi hizo ziki-deal na tatizo hilo kwa mtizamo wa miaka 50 ijayo ilhali economies zao zinaelekea shimoni.

  Bottom line is,kasi yaChadema inazidi kuwakurupua propheties of doom,conspirancy theorists na wababaishaji wengine.Watakuja na chambuzi tamu na so convincing lakini walalahoi wanapaswa kuwa makini kwa sababu kama CCM ilivyojivua magamba-from chatu to mjusi ndivyo mafisadi watakavyojibidiisha kuja hapa na kujifanya ni wenzetu wenye uchungu na nchi yetu lakini kwa vile mchawi hakusi kibuyu cha kuwangia watashindwa kujizuia kuitupia dongo Chadema.
   
 6. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  At least ameeleweka acha uvivu wa kusoma
   
 7. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ha haaa mkuuu taratibu, hala hala kidole na macho. Mchango wako umetukuka sana, hata hivyo sijasema napinga pasee sera danganya toto za Chadema hapana, hiyo ni saafi sana na wanafanya vizuri sana. What I see lacking ni the vision of where Chadema want to see Tanzania and more the strategies to achieve them na hizi sera za fasta fasta za kutatua matatizo ya fasta fasta na hoja za kuleta umaarufu wa fasta fasta zitekelezwe kwa kuzingatia ile long term stratergy, nadhani hivyo ndio long term strayegists hufanya. Hao marekani wenyewe kila wanachofanya ni kwa ajili ya kusum up to their goal, which is to remain the world's economically most powerful nation, na wanfaynya hivyo at any cost jhata kwa kizijasusia au kuziterorze nchi nyingine!
  Bila long term strategies tutakuwa tunapigania kushusha tu bei za sukari na mafuta and forever remain one of the poorest country in the world!
  Let's think and act in that big picture!
   
 8. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  MI nakushukuru kwa changamoto uliyoleta na nadhani kama mtu siyo mshabiki wa vyama anaweza kuelewa unataka kuona zaidi strategy kuliko tactics ila mi nisingekubaliana na terminology ya 'danganya toto' kwani mi naamini CDM hasa baadhi ya viongozi wake akiwemo Dr Slaa wanafanya vitu kwa true conviction. Hata hivyo wamekosa kabisa mwongozo wa muda mrefu yaani STRATEGY ambayo huwa inatolewa na STRATEGISTS.
   
 9. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nashuru umenielewa!

  Danganya toto ni lugha tu ya picha ili ujumbe ufike sawasawa kwa mantinki ya kwamba mambo huwa yanafanyika kutatua matatizo ya fastafasta, kama tatizo ni njaa basi watu wakipewa chakula wakashiba basi mchezo umekwisha! Ni kama mtoto mdogo anavyopewa pipi akisumbua ili atulie, big challenges still remain on our way!
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tatizo la sasa ni tatizo la siku zote la Watanzania. Tuna mtindo wa kutukuza vyama vya siasa kama dini na viongozi wa vyama hivyo kama mitume. Mwanzo ilikua CCM na kuna watu wali kifuata chama na kukubaliana kila Mwl. Nyerere alicho kisema bila kuhoji. Tunaona mazao ya mentality hiyo mpaka leo ambapo wabunge wa CCM wako tayari kukubaliana na chama chao katika kila kitu bila kuhoji.

  Leo hii kuna mashabiki wa Chadema ambao wao hawa taki baya lolote lisemwe juu ya chama na viongozi wao. Tuna rudi kule kule kwa kuabudu chama na kufuata kama mabeberu bila kupinga. Leo hii kuna baadhi ya watu hata useme kitu cha kweli juu ya Chadema kama huki tukuzi utaitwa fisadi na majina mengine.

  Nchi za wenzetu zimeendelea kwa sababu watu wapo tayari kuhoji. Angalia leo Marekani. Marekani mbunge yupo tayari kupingana na chama kwa maslahi ya taifa au wapiga kura wake. Marekani mtu yupo tayari kumpigia mgombea wa chama kingine kama anaona ndiye anaefaa. Lakini Tanzania leo hii bado sisi tuna fikra za kufuata vyama vyetu kwa lolote.

  Kuna mambo mengi Chadema na viongozi wake wanaweza kuji rekebisha. Lakini mtu usivitaje hata kama uko wazee vipi uta semwa na kuna wapumbavu wata kuwa tayari kutetea chochote tena kwa maneno ya kisomi ili hali hoja ni za kitoto. Bado safari ni ndefu sana.
   
 11. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Shurani sana kwa mtazamo wa hekima uliotupa, Ni kweli kabisa ulichosema.....Mimi kwangu ni Tanzania kwanza, Chama cha siasa baadae!
   
 12. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Umesema kweli lakini Sinai hakim unaowaeleza wanakuelewa. Tatizo ni ushabiki. Chadema haikushusha bei ya sukari kwani hata sasanqua bado bei iko juu katika baadhi ya maeneo sijui polisi wa cdm hawajafika huko! Tatizo la cdm ni kutokuwa na viongozi wenyewe maono vision. Ukiwauliza swapo wanataka Tanzania ya namna gani lini,hawnajibu. Ni ufisadi,bei ya sukari, cement. 5000/-.kiongozi wa chadema mwenye maono nani dr slaa, Mbowe, Ndesamburo lema na nani? Watendelea tu kuiamsha ili iendelee kutawala vizuri.
   
 13. K

  KWELIMT Member

  #13
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Hapa umesema ukweli, mikakati ya mda mfupi na mrefu ni muhimu sana.najua kuna watu wanakupinga tu hawajaisoma thread yako na kuielewa.

  big up up....................up .......up
   
 14. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Nimekuelewa sana
   
 15. ChescoMatunda

  ChescoMatunda JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,189
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Big up kwa mawazo yako ya mapema muda upoo bado kuyafanyia kazi lakini pia naamini chadema wanazingatia hiloo sidhani kama wangemwaga mbinu zao za muda mrefu hapa so kuwa karibu na uchangie kwa ukaribu pale cdm hapa jf ni porojo na mawazo yako tuu ambayo sio lazima kila mtu akubali.
   
 16. A

  Abba Member

  #16
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mleta hoja inaonekana wewe ni mwanafunzi mgeni wa political science ambaye amesoma chapter mbili tu za political theories book alafu unataka kuwa kuwa political strategist! Think again.....
  Ulikuwa wapi wakati chadema inanadi mikakati na sera zao wakati wa kampeni mwaka jana? Je ulichukua hatu kukisoma kitabu kile cha sera zao? Kama kweli ulisoma usingekuwa unaandika haya unayoaandika sasa kama kweli una nia njema.
  Lengo la muda mrefu na lengo kuu la Chadema ni kujenga Tanzania yenye uchumi imara na yenye kuheshimu demokrasia,haki za raia na kutengeza fursa ya ajira kwa watanzania ili waweze kuendesha maisha yao. Lakini vile vile walizungumzia mikakati ya muda mfupi 2010-2015 ikiwemo; kuwekeza sekta ya nishati, kuwekeza katika sekta ya elimu-shule za kanda (the like of Tosamaganga, Ndanda, Mazengo,Tabora etc),kubadilisha mfumo wa utawala katika nchi yetu (Gavonors) amabyo nigeria/USA wanatumia na imeonyesha kuwafaa sana.Bahati mbaya mikakati haikuweza kutekelezwa kwa sababu ya uwizi wa wazi na aibu wa ******. Sasa unapokuwa chama cha upinzani huna nafasi ya kutekeleza mikakati yako ya muda mrefu na unabaki kuwa govt watch dog huku ukiwakumbusha wananchi what you can offer in short and long term. Chadema kama Republican Party ya marekani(Japo sio mshabiki wao) wamekuwa mstari wa mbele kusisitiza haja ya serikali ndogo, haja kuwa na fesical responsibility and accountability (moja ya ajenda katika vita dhidi ya ufusadi). Lakini vile vile kama wademocrat wamekuwa wakisisitiza haja ya kujenga taifa lenye watu wa kipato cha kati. Kwahiyo sera,mikakati ya muda mfupi, wakati na mrefu zipo!
   
 17. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante saaana! Idumu Tanzania!
   
 18. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Shukrani Mkuu, japokua ninachomaanisha si kwamba Chadema wamwage kikakati yao hapa, la, ingawa si vibaya! Wananchi wanatakiwa kuijua, mimi binafsi kama mwananchi pia nahitaji kujua!
  Najua mna mambo mengi mazuri lakini ni muhimu kuyatenda na kuyacommunicate kwa wahusika ambao ni wananchi sio kuyakalia tu maofisini na majumbani kwenu!
   
 19. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata JK anajua kama CDM ni chama cha msimu.

  so, hakuna jipya hapa. only duplicates.
   
 20. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  nadhani umeeleweka mkuu....
   
Loading...