Umaarufu wa CCM wazidi kupotea, sasa watumia nguvu kuteka hafla za kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umaarufu wa CCM wazidi kupotea, sasa watumia nguvu kuteka hafla za kitaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 4, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  WanaJF:

  Sasa ni wazi kabisa umaarufu wa CCM umeanza kupungua kwa kiasi cha kutisha kiasi kwamba hata zile shughuli za kitaifa zinalazimishwa kuwa ni za CCM. Leo hii JK alifungua barabara ya 60km kati ya Mwandiga na Manyovu mkoani Kigoma, katika hafla ambayo ilitekwa na CCM kwa kuwepo watu wa magwanda ya kijani ambao bila shaka walitayarishwa rasmi kupamba hafla hiyo.

  Mbunge wa eneo hilo, Zitto Kabwe, alijikuta akihutubia na umati wa wana-CCM ingawa jimbo lake hilo wengi ni Chadema kwa vile mwaka jana tu walimchagua yeye Zitto wa chama hicho na kumbwaga yule wa CCM.

  Kweli tutaona vituko vingi kutoka kwa wanamagamba wanapoelekea kupotea katika medani ya siasa hapa nchini!


  Source CH ten news bulletin today.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nami nimeiona hiyo. Pole Zitto lakini kaza uzi, mradi wananchi wanajua wewe ni Mbunge wao. hawa watu wa magamba hawana hata haya!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Watafanya kila aina ya vitimbi, lakini ni watu wa kuondoka tu. Wameshindwa kusimamia nchi. Wanataka kuwadanganya wananchi kwamba hiyo barabara iligharamiwa kwa hela za mashamba ya CCM? Yako wapi hayo mashamba?
   
 4. Bollo Yang

  Bollo Yang JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 440
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Acha bangi kwanza ndio uje hapa
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kuna thread moja jana niliiona ikisema kwamba CCM inaelekea kuyateka maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru. Lakini watarangia nini -- giza totorooo wakifanya maadhimisho hayo?
   
Loading...