YouTube
JF-Expert Member
- Jul 24, 2012
- 936
- 361
nilkuwa najiuliza sana kafanya nini haswa cha kuwashinda viongozi wengine waafrika waliopata kutokea na waliofanya mengi ya kuwahusu waafrika, nikawa nahisi si bure ni zawadi ya wa Magharibi walioyompatia baada ya kuwardhisha. na wengi wetu waafrika tumekwuwa "brain washed" na hata kuwasahau viongozi wetu mashuhuri waliopita e.g kwame Nkurumah
na leo saa 3usiku nimesikia maoni ya mchambuzi mmoja alikuwa kwenye kipindi cha bbc swahili kinachorushwa na star tv akichagiza kwamba Mandela alikuwa ni maarufu zaidi Magharibi kuliko hata Afrika, sababu baada ya kutoka gerezani aliwapa wazungu kilie walichokitaka. akaongeza na kuna kipindi alipotoka gerezani ANC iligawanyika wale waliotaka mabadiliko makubwa na wale waliokuwa laini kwa wazungu akina Mandela, Thabo Mbeki n.k
huyo mchambuzi akaongeza;
......Mandela ameondoka na ametutoka na lakini mfumo wa ubaguzi aliouacha ni uleule wa ubaguzi
.......umaskini afrika kusini kwa waafrika kusini ni uleule na bado sana kuuondoa.
.......waliofaidika ni wa wale wa chama chake cha ANC waliokuwa na msimamo laini dhidi ya mabadiliko ya kweli na ambao wamekuwa matajiri wa kutupwa sana na waafrika kusini wengi wakiwa maskini.
wazungu/makaburu ni kama waliingia naye mkataba wamuachie huru, then wampe urais , lakini kusameheana ni lazima.
watakuja watu na mapovu yao hapa na kusema hakuna kama Madiba na wala hawana point za kusema anawazidi akina Kwame Nkuruma, Jk Nyerere n.k
watashupalia ooh Mdiba kafanya Menigi sana;-
eti kafuta ubaguzi wa rangi..... hivi ni kweli kafuta ubaguzi wa rangi au makaburu waliona tu waachane na sera ya apartheid baada ya kusoma alama za nyakati??
......kingine alichofanya ni kuwasemhe wazungu,,,,, hivyo viwili ndio alivyofanya vya kuwa praise kiasi hiki???
......au kukaa jela kwa miaka 27 ndio ishu kubwa sana,,,,,,

Mtu ukimfanyia makosa makubwa harafu akasamehe utampenda zaidi, lakn mapenzi hayo sio ya dhati ni majikombo kwa muhusika ili asije kumbushia madhira na madhara ulompatia hapo awali. Kwenye biblia imeandikwa mtu anayesahemewa deni kubwa huwa karibu zaidi na msamehe deni kuliko aliyesamehewa hela ya mboga.
Mandela ni mvumilivu kwel kweli, alisamehe deni kubwa na kusahau madhara yaliyosababishwa na watesi wa waafrika. Pengine ndo ilikuwa njia sahihi kwa wanyonge kutoweka ligi na wenye mabavu, atakumbukwa kwa hilo mchana ama usiku. Kweli mandela hakutaka kuwaoesha wazungu makosa yao, aliwafundisha kuwa wanaweza kupuuzwa kwa yale waliofanya. Alisamehe wazungu kirahisi kuliko hata weusi, alishindwa kumsamehe Winnie ambaye kama binadamu n baada ya Mzee kuwa jela miaka 27 alibanjuka na Dali Mpofu, ambaye alikuwa Mwanasheria wao.
Swali linalobaki kuwa nyeti sana na ambalo ningependa kuliongelea ni umaarufu ambao mandela alitunukiwa baada ya kushindwa kutoa hukumu ya haki kwa wazungu kwa makosa waliyoyafanya kwa makusudi, maana hawajafanya mara moja wala mbili, wala hakufanya mzungu mmoja wala wawili tuseme ilitokea bahati mbaya ktk maisha. Ghafla kama ilivyo ktk mikakati ya wazungu ktk kutoa kile kinaitwa elimu, walimbeba Mandela juu ya vongozi wote wa afrika juu ya kila mtu kama kwamba mandela alisaidia ukombozi wa Africa, kushinda aliyestahili tuzo hiyo Mwalimu Nyerere, Nyerere hakupendwa sana na wazungu maana aliwapinga waziwazi na kukemea vitendo vyao, aliyekosa nyerere kinyume na mandela amlipa adhabu yake. Mandela ukiacha S. Africa ambako kwa dhati kabisa anahitajika kuitwababa wa taifa, hakuna tena nchi ya afrika ambayo alitoa mchango wake.
Ukiwapinga wazungu unakuwa adui, kama ilivyo kwa Nyerere, Mugabe tunaona anapendwa sana ispokuwa ghafla anakuwa mbaya saaana baada tu ya kupinga wazungu kumiliki ardhi kubwa mno Zimbabwe. Gadafi alipotaka kuonesha nji kwa waafrika aliuawa na hawa hawa wazungu, tena juzi tu, kama kusamehe ni dili mbona hajaachwa, OSAMA mbona hakusamehewa? Kusamehe asamehewe mzungu sifa kibao.
Wasiwasi wangu Heshima anayopewa Mandela isije kuwa ni hongo kwa vile alivyosaliti weusi kwa kutotoa adhabu kwa makosa makubwa ya wazungu, sijui kama kutotoa adhabu ni sahihi, dunia inaangamia kwa watu wema kushindwa kuwakataza watu waovu, kushindwa kutoa adhabu stahiki kwa makosa kunawezajenga picha mbaya sana. kwa hili japo mandela ni baba afrika kusini sio baba afrika wala kwamaoni yangu hakaribii hata kwa nusu mchango wa Nyerere ambaye anasthili kuitwa baba wa afrika.
Mitego iko mingi huu nao ni mtego kwa mwafrika, lazima tuung'amue. Tumehongwa pesa, madaraka leo hata sifa tunahongwa tunafumbia macho ukweli. Kama ilivyo kwa elimu, pesa na wakati/muda hakuna mwafrika anayejua vyote hivyo zimetoka wapi, lakn tunatumia tu, madhara ya kuwa watumiaji tu ni kutambulika kama wajinga mbele ya mzungu (Biology, Chemistry Physics, Maths nani aliamua ziwe zilivyo), kutambulika kama masikini mbele ya mzungu maana ndo mwenyehela (kumbuka hoja za Muhongo jana Nkrumah Hall), kutambulika kama watu wasijali muda there is no hurry in Africa. Ukweli hatujui nani alileta vitu hivi kwa faida ya nani?
Japo sio vema sana kuwalinganisha marafiki hawa lakni ifahamike, Nyerere kakopwa sifa zake na kupewa Mandela kwa faida ya Wazungu.
Nawasilisha