Umaarufu/Umashuhuri wa Mandela uliotengenezwa na Magharibi na Wazungu!

Mandela ni zaidi ya Kagame, mambo yanayomuweka juu ya yote ni kifungo na msamaha kwa wazungu.
He spared them, sina uhakika kama kulikuwa na makubaliano kabla lakini kwa kuwasamehe wazungu nao wakaamua kumlipa fadhila kwa namna hiyo, umaarufu ulio overated.
Kiuhalisia yupo nyuma sana ya viongozi wengi wa kiafrica.
 
Nimeguswa na jambo moja. Mandela anasifika kwa kusamehe. Aliwasamehe makaburu lkn hakumsamehe mkewe Winnie. Winnie alitoka nje ya ndoa huku Mandela akitumikia kifungo cha maisha.

Iweje Mandela awasamehe waliyo mtendea makubwa lkn asimsamehe Winnie na kumtaliki!? Uwezekano wa Mandela kuachiwa kwa sharti la kuwasamehe makaburu na kuwaacha waendelee kuhodhi uchumi ni mkubwa. Hata hivyo bado naamini aliyoyafanya nyerere ktk ukombozi wa afrika ni makubwa kuliko ya Mandela.
 
nilkuwa najiuliza sana kafanya nini haswa cha kuwashinda viongozi wengine waafrika waliopata kutokea na waliofanya mengi ya kuwahusu waafrika, nikawa nahisi si bure ni zawadi ya wa Magharibi walioyompatia baadah ya kuwardhisha. na wengi wetu waafrika tumekwuwa "brain washed" na hata kuwasahau viongozi wetu mashuhuri waliopita e.g kwame Nkurumah

na leo saa 3usiku nimesikia maoni ya mchambuzi mmoja alikuwa kwenye kipindi cha bbc swahili kinachorushwa na star tv akichagiza kwamba Mandela alikuwa ni maarufu zaidi Magharibi kuliko hata Afrika, sababu baada ya kutoka gerezani aliwapa wazungu kilie walichokitaka. akaongeza na kuna kipindi alipotoka gerezani ANC iligawanyika wale waliotaka mabadiliko makubwa na wale waliokuwa laini kwa wazungu akina Mandela, Thabo Mbeki n.k

huyo mchambuzi akaongeza;

......Mandela ameondoka na ametutoka na lakini mfumo wa ubaguzi aliouacha ni uleule wa ubaguzi

.......umaskini afrika kusini kwa waafrika kusini ni uleule na bado sana kuuondoa.

.......waliofaidika ni wa wale wa chama chake cha ANC waliokuwa na msimamo laini dhidi ya mabadiliko ya kweli na ambao wamekuwa matajiri wa kutupwa sana na waafrika kusini wengi wakiwa maskini.

wazungu/makaburu ni kama waliingia naye mkataba wamuachie huru, then wampe urais , lakini kusameheana ni lazima.

watakuja watu na mapovu yao hapa na kusema hakuna kama Madiba na wala hawana point za kusema anawazidi akina Kwame Nkuruma, Jk Nyerere n.k

watashupalia ooh Mdiba kafanya Menigi sana;-

eti kafuta ubaguzi wa rangi..... hivi ni kweli kafuta ubaguzi wa rangi au makaburu waliona tu waachane na sera ya apartheid baada ya kusoma alama za nyakati??

......kingine alichofanya ni kuwasemhe wazungu,,,,, hivyo viwili ndio alivyofanya vya kuwa praise kiasi hiki???

......au kukaa jela kwa miaka 26 ndio ishu kubwa sana,,,,,,

Sijui kama mleta mada anajua kuwa Africa kusini mauaji yalikuwa ni makubwa kwa kipindi cha mwaka 1990-1994 baada ya mandela kuachiwa possibly kuzidi kipindi chote cha ubaguzi.wakati Rais wa wakati huo De Krek hataki kunegotiate na anawatumia inkhata -chief butelezi kuuwa wafuasi wa ANC ni ANC pekee iliyo kuwa inasukuma maongezi/negotiatios pekee. Butezezhi na wafuasi wake waliua watu wengi sana na kundi moja la wazungu wasio taka mabadiliko. Mabomu yalikuwa yanategwa kila kona ka Iraq vile na hata airport lakini mandela alitumia maneno ya kulaani tu na kuinsist vyama vyote viendelee na majadiliano.Mandela alikataa kuachiwa huru kwa masharti mwaka 77 akisisitiza kuachiwa kwangu kusiwe na masharti.Mandela alikuwa na approach ya Jesus kwa wale wakristu wanajua.....baada ya kuwa rais aliunda tume ya maridhiano akisisituza "bila msamaha hakuna taifa". Najua mleta mada anafikilia kama Malema....alipenda nguvu iendelee kutumiaka lakini bila busara ya mandela south Africa isingekuwepo...imagine chief Butelezi alikubali kuingia kwenye uchaguzi zimebaki siku 8 tu za kupiga kura na ilibidi jina lake libandikwe kwenye listi ya wagonbea kwa gundi....they were ready to kill ANC followers, kundi la wazungu wenye msimamo mkali same...serikali ya Dekrak same except his experience the late Madiba....mleta mada fanya research kidogo usitumie akili ya jamaa wa BBC.....Mandela was a leader, true friend of the world.
 
Akiwa pale Robben island,Madiba alikutana na yule nyoka(draconian bloodline) aliyemuuliza swali lile lile kama alilomuuliza Yesu jangwani.Majibu ya Madiba na Yesu yalitofautiana.Viongozi wetu wengi wamekutana na huyu nyoka na wamechagua kupewa dunia na yaliyomo.Wamechagua kubaki wao salama at the expense of entire human race either kwa kujua au kwa kutokujua.Mungu awasamehe.Hamba kahle Madiba.Watu wa aina ya Nyerere ni wachache sana kizazi hiki.Hutokea mara moja moja sana.Watz watamkumbuka sana mwalimu.
 
Nimeguswa na jambo moja. Mandela anasifika kwa kusamehe. Aliwasamehe makaburu lkn hakumsamehe mkewe Winnie. Winnie alitoka nje ya ndoa huku Mandela akitumikia kifungo cha maisha.

Iweje Mandela awasamehe waliyo mtendea makubwa lkn asimsamehe Winnie na kumtaliki!? Uwezekano wa Mandela kuachiwa kwa sharti la kuwasamehe makaburu na kuwaacha waendelee kuhodhi uchumi ni mkubwa. Hata hivyo bado naamini aliyoyafanya nyerere ktk ukombozi wa afrika ni makubwa kuliko ya Mandela.

Duh....sikuwahi kuwaza kuhusu hii nyundo.
 
Duh kumbe amekufa kiukweli sijawahi mfikiria sana Mandela bt anaweza akawa amfanya mambo makubwa kam nchi ila kwa Africa sijaona au sina information sana kuhusu hilo.

Hapa Africa mwanaume jk nyerere alikufa wakati bado anamchango mkubwa sana bt hawa waliopo ni vipele vya wamagaribi tu.

Mandela sielew hata mchango wa s Africa kama Tz labda kuturahisishia njia za kupitisha Unga ila kwa kujikwamua sijui.

Kama vipi Nirekebishwe
 
Mleta mada waweza kuwa na point (hata km ni hisia zisizo na evidence) lakini timing ya mada si sahihi. Hebu acha tumzike mzee wetu na kama bado kuna tija tutajadili.
 
Dunia ijiandae na mazishi ya "kukata na shoka".Ni zawadi ya mwisho ambayo yule joka huitoa kwa wale wote waliokubali ama kumwabudu au kutoingilia maslahi yake ili waliobaki duniani watamani "utukufu" huo.Nothing new in this world.It's all about "ancient war".Ila mojawapo ya mambo yaliyompa wakati mgumu Madiba katika siku zake za mwisho ni kutoridhika nafsini mwake na uamuzi aliochukua Robben island.
 
Mandela alikuwa mpigania haki za mzawa SA na alisimamia msimamo huo katika kipindi chote cha ubaguzi nchini SA, lakini watafiti wa mambo wanadai wazungu walimrubuni alipokuwa jela wanahisi labda alirubuniwa kirahisi kwa sababu aliyachoka maisha ya jela au vinginevyo, na inasemekana msamaha alioutoa kwa walowezi (na pengine ndo kitu kilichomjengea heshima zaidi duniani) ulikuwa sharti la kwanza katika mkataba uliomtoa jela, hiki kitu kilimfanya ajione na aonekane mnafiki kwa wapiganaji wenzie, dhambi ya kujiona mnafiki ilikuwa inamsumbua sana na ndio maana aliamua kuongoza kwa muda mchache sana na kumwachia Thabo Mbeki japo bado uwezo na nguvu za kuiongoza SA alikuwa nayo! kitu ambacho kwa watu wengi wanampongeza coz alitofautiana na viongozi wengi wa kiafrika! Huyu ndiye Nelson Mandela kiongozi mwenye sura mbili japo wengi tunaiona moja na kuisifia Sura ya upiganaji, sura ya ukombozi na sura yake ya pili sura ya kukata tamaa, sura ya kurubuniwa na sura ya kinafiki ikifichwa sana katika historia hasa zile historia ya kizungu! japo kidogo ila naamini nmeeleweka kwenu wandugu..................
 
Waafrika tumeanza kuamka tena usingizini..Mungu aendelee kutusaidia...
huenda Nyerere mwingine akazaliwa Afrika. Uchambuzi mzuri huu!
 
Mandela kajitolea maisha kwajili yasouth africa ule ubaguzi haukuondoka hvhv ila kwatabu kubwa alozipata mandela thatsy maisha yke alikua jela so ulitaka nn tena yy kam binadam hakosi mapungufu yke hayo mengine wafanye wengine
 
Jana usiku nilikuwa najadiliana na rafiki yangu with liberal minds na tukafikia hitimisha kuwa MANDELA alikuwa ni JANGA kwa WASOUTH na AFRIKA kwa Ujumla. Baadhi ya sababu za msingi ni kama alivyosema mtoa mada.
 
Utaifakwanza nitaendelea kuchangia kwa maswali:

Tanzania kama taifa lina sifa dunia au halina, na kwa nini?

Vipi ukilinganisha sifa za Tz na SA duniani zinalingana? Je ni kiongozi yupi aliye nyuma ya sifa za taifa lake iwe ni Tz au iwe ni SA?

Kati ya Nyerere na Mandela nani alinyanyua mikono mambo yalipo muwia magumu? AU kati yw hawa wawili nani alishi ndoto zake kwa ukamilifu zaidi?
 
nilkuwa najiuliza sana kafanya nini haswa cha kuwashinda viongozi wengine waafrika waliopata kutokea na waliofanya mengi ya kuwahusu waafrika, nikawa nahisi si bure ni zawadi ya wa Magharibi walioyompatia baada ya kuwardhisha. na wengi wetu waafrika tumekwuwa "brain washed" na hata kuwasahau viongozi wetu mashuhuri waliopita e.g kwame Nkurumah

na leo saa 3usiku nimesikia maoni ya mchambuzi mmoja alikuwa kwenye kipindi cha bbc swahili kinachorushwa na star tv akichagiza kwamba Mandela alikuwa ni maarufu zaidi Magharibi kuliko hata Afrika, sababu baada ya kutoka gerezani aliwapa wazungu kilie walichokitaka. akaongeza na kuna kipindi alipotoka gerezani ANC iligawanyika wale waliotaka mabadiliko makubwa na wale waliokuwa laini kwa wazungu akina Mandela, Thabo Mbeki n.k

huyo mchambuzi akaongeza;

......Mandela ameondoka na ametutoka na lakini mfumo wa ubaguzi aliouacha ni uleule wa ubaguzi

.......umaskini afrika kusini kwa waafrika kusini ni uleule na bado sana kuuondoa.

.......waliofaidika ni wa wale wa chama chake cha ANC waliokuwa na msimamo laini dhidi ya mabadiliko ya kweli na ambao wamekuwa matajiri wa kutupwa sana na waafrika kusini wengi wakiwa maskini.

wazungu/makaburu ni kama waliingia naye mkataba wamuachie huru, then wampe urais , lakini kusameheana ni lazima.

watakuja watu na mapovu yao hapa na kusema hakuna kama Madiba na wala hawana point za kusema anawazidi akina Kwame Nkuruma, Jk Nyerere n.k

watashupalia ooh Mdiba kafanya Menigi sana;-

eti kafuta ubaguzi wa rangi..... hivi ni kweli kafuta ubaguzi wa rangi au makaburu waliona tu waachane na sera ya apartheid baada ya kusoma alama za nyakati??

......kingine alichofanya ni kuwasemhe wazungu,,,,, hivyo viwili ndio alivyofanya vya kuwa praise kiasi hiki???

......au kukaa jela kwa miaka 26 ndio ishu kubwa sana,,,,,,
Brother you are very right,Mandela doesnt deserve the name FATHER OF AFRICA just the way magharibi wanavolazimisha iwe Yeye ni baba wa watu wa Africa Kusini WEUSI kwa WEUPE. Africa katufanyia nini mandela zaidi ya vionozi wetu wa Africa pamoja na chumi zao ndogo kumsaidia mandela na watu wa Africa Kusini kupata amani waliyo nayo.Mpaka hadi leo Africa hatujaona mchango wa Kipekee wa South Africa wenye Msimamo wa Kiafrica zaidi ya kuendelea konyonya nchi maskini za Kiafrica achilia mbali kuwa na uchumi mkubwa katika bara hili. For me better GADAFI than MANDELA katika kuipigania AFRICA ni mtizamo tuu.
 
Ua very rite, black south africans wanamchukia sana jamaa, wanasema hata mateso aliyoyapata ya kuumwa mda mrefu ni sababu ya usaliti mizimu ilikua haitaki kumpokea...kuna mahero wq ukweli kama sobukwe hawasemwi sana coz walikua na misimamo ya kutetea maslahi ya blacks
 
Nimeguswa na jambo moja. Mandela anasifika kwa kusamehe. Aliwasamehe makaburu lkn hakumsamehe mkewe Winnie. Winnie alitoka nje ya ndoa huku Mandela akitumikia kifungo cha maisha.

Iweje Mandela awasamehe waliyo mtendea makubwa lkn asimsamehe Winnie na kumtaliki!? Uwezekano wa Mandela kuachiwa kwa sharti la kuwasamehe makaburu na kuwaacha waendelee kuhodhi uchumi ni mkubwa. Hata hivyo bado naamini aliyoyafanya nyerere ktk ukombozi wa afrika ni makubwa kuliko ya Mandela.
That can be true kuwa Nyerere alifanya mambo makubwa sana kwa bara la Afrika, kulinganiisha na Mandela.

Kitu pekee ambacho kimempandisha sana chati Madiba,ni kule kuhukumiwa kifungo chat maisha,kwa ajili ya kupigania haki ya watu weusi,ambapo hata hivyo alitumikia kifungo cha.miaka 27, ambapo baada ya hapo,aliachiliwa huru na serikali hiyo hiyo ya makaburu,iliyokuwa imemfunga kifungo cha maisha!
 
Wacha ulevi kaka hilo hatulikatai ni baba wa watu wa Africa Kusini na kama ulivoeleza hapo juu he deserve dat BUT Mandela can and Shall never be The father of Africa kama Wazungu na washenzi wachache wanavoiaminisha Dunia huyo mzee hawezi vaa viatu vya Nkuruma, JK nyerere na Hata Ghadafi katika kupigania UHURU WA AFRICA na Haki za waafrica ikiwa ni pamoja na unyonyaji wa waafrica.hao makaburu siyo tu kwa sasa wanawanyonya Waafrica kusini weusi wanainyonya Africa kwa ujumla huu ndo ukweli R.I.P MADIBA!
 
Hizi bangi mnazovuta kweli mbaya, hivi umeenda afrika kusini na ukafanya utafiti wa hiko unachoongea, kuna viongozi wangapi waafrika ambao wameshika nafasi nyeti ndani ya serikali na kuna mabilionea wangapi weusi ambao wamenufaika na uhuru walioupata.

Uwezi kusema makaburu waondoke kabisa kwa sababu hawana pakwenda na wamekuwapo South Africa kwa zaidi ya miaka mia mbili sasa wewe ulitaka afanye nini. Ni ukweli kuwa Mandela ana roho nzuri ukilinganisha na viongozi wengine wa Afrika kwa maana ndio kiongozi pekee alieongoza kwa miaka 5 na kukubali kupumzika tofauti na viongozi wengine wenye uchu wa madaraka. sasa kosa lake liko wapi?

Nafasi zipo na kuna fair competing ground na kuna wazawa wengi ambao walipewa maeneo ya kilimo a wengine ni wamiliki wa makampuni ya wine huko south africa. sasa mlitaka mlishwe keki midomoni acheni kuzubaa na kupenda kutoa lawama zisizo za msngi kufanya kazi kwa bidii ndio njia ya kupata maendeleo tatizo case study inaonyesha wa South Africa weusi wengi ni wavivu na hili linaukweli kwa muda niliosoma na kukaa South Africa hili nililiona. Ndio maana wakiona wageni wanawapiga kwa sababu wanaona ni more hardworking kuliko wao

Back
Top Bottom