Umaarufu kwa wasanii chanzo cha kuambukizwa VVU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umaarufu kwa wasanii chanzo cha kuambukizwa VVU

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Lucchese DeCavalcante, Apr 20, 2011.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  [​IMG][​IMG][​IMG]
  Imeelezwa kupenda umaarufu na sifa kwa wasanii wetu ni miongoni mwa sababu za kuambukizwa VVU

  Wasanii wametajwa kuwa hatarini kuambukizwa virusi vya UKIMWI kutokana na umaarufu walionao na kujikuta wakishawishika kuingia katika vitendo mbalimbali vya hatari kwa afya zao hasa vya ngono.

  Hayo yamesemwa wiki hii na Muelimisha rika Taji Liundi wakati akiwasilisha mada kuhusu Umuhimu wa Msanii Kutunza Afya Yake kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo alisema kwamba, umaarufu, ushawishi na kutojitambua miongoni mwao ndiyo chanzo kikubwa cha wao kuwa hatarini kupata maambukizi hayo.

  “Kutojitambua, umaarufu na ushawishi mkubwa walionao wasanii katika jamii huwafanya wawe hatarini kuathiriwa na ugonjwa wa UKIMWI kwani hufuatwa na kundi la watu na mara nyingi kujikuta wakishawishiwa kufanya ngono katika mazingira yasiyo salama” alisema Taji Liundi ambaye ni Kamishna msataafu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS).

  Aliongeza kwamba,kada ya wasanii imekuwa ikiathiriwa na ugonjwa huu toka umegunduliwa kwani katika nchi zilizoendelea kumekuwa na taarifa za vifo vya wasanii wengi vinavyotokana na UKIMWI huku akiweka wazi kwamba kutumia vibaya umaarufu ambako kumekuwa kukichanganywa na matumizi ya vilevi ni sababu nyingine kuu.

  Alizidi kueleza kwamba,uwepo wa tunzi za kimapenzi katika kazi za sanaa ni changamoto nyingine kwani imezifanya kazi za wasanii kuwa za kusisimua na kuamsha utendaji ngono miongoni mwa wanajamii na kuwaacha wao wakiwa waathirika wakubwa.

  “Ukitazama nyimbo za wasanii wa kizazi kipya utaona ni zenye maudhui ya rika la adolescence (umri wa makumi),zimebeba ujumbe wenye kuhamasisha mapenzi na ngono na hapa ndipo tunapoona mabadiliko makubwa ya vijana wakihamasika kufanya yale wanayoyaona na kuyasikia kupitia vyombo vya habari” alisisitiza Taji.

  Alimalizia kwa kuwaasa wasanii kujitambua, kujilinda na kuwajibika katika kupambana na VVU/UKIMWI huku akiwaeleza kwamba,umaarufu na ushawishi walionao huathiriana na jamii (Two way effects) hivyo hawana budi kuwa makini.

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, wasanii wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu dhidi ya UKIMWI kwa jamii na kujisahau wao binafsi kwamba wako katika mazingira hatari ya kupata maambukizi.

  Alisema kwamba,BASATA katika mpango mkakati wake wa 2011-2014 itajikita katika kutoa elimu kwa wasanii na kuwapa ufahamu juu ya ugonjwa huu hatari ambao umekuwa ukiwaua wasanii mbalimbali duniani.
   
 2. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  dah hii ni kweli asee,they get wasted,manake wakishafanya filamu muda mwingi wanakuwa hawana kazi ya kufanya,so they get wasted,bierre,ngono,starehe disko na raha za kutosha kama yule Rose Ndauka yule mhhhhh....
   
 3. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Sasa mbona umewaweka pamoja na Mheshimiwa Rais. Unamaanisha naye pia ni msanii?
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Sasa mbona umewaweka pamoja na Mheshimiwa Rais. Unamaanisha naye pia ni msanii?

  Ha ha ha ha, umenichekesha sana. pitia zawadi hapa PPF Tower

   
 5. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  mkuu unafikiria mbali sana lolz
   
 6. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  You are such a genious Askari Kanzu mie hata sikuliona hilo
   
 7. K

  Kana Amuchi Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe umenena
   
 8. c

  chaArusha Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Tatizo lengu liko kwa huyo muelimisha rika, Taji Liundi. Jamaa ana sifa ya kuwafanyisha ngono watoto wadogo katika clubs na mahoteli tofauti jijini Dar. Sasa anapotoa wosia kama huo napatwa na kigugumizi
   
 9. k

  kaliakitu2008 Member

  #9
  May 5, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna msemo unasema fuateni maneno yangu na si matendo. Kwa hiyo kwa tabia ya muelimishaji TL ni vyema akatoa mada hata kama yeye ni mchafu kihivyo cha msingi sikia maneno yake na yeye matendo yake yaache kama yalivyo. Mara ngapi twawaona viongozi wa dini wakiwa katika mimbari wanatoa mahubiri mazuri lakini wakishuka kutoka sehemu hizo wanakuwa chui kwa kondoo na mbuzi?
   
 10. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nimekukubali mzee...birds of the same feathers flock together, au vipi? hao ni wasanii wetu bongo!
   
 11. k

  kinubi Senior Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  mhhhhhhh!!!!!!!!
   
 12. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hapo kweli umenena
   
Loading...