Salaam wakuu
Walokole wenzangu, Bwana asifiwe na hongeleni kwa ibada za kukanyaga mafuta, kupanda na kuvuna na ibada za kufunguliwa kutoka kwenye vifungo mbali mbali.
Kuna kitu leo ntaomba tusemezane kwa roho safi kabisa.
Ni desturi na mazoea kila mwisho wa mwaka kunakua na pilika mbalimbali za mafundisho, semina na makongamano ya kuhitimisha mwaka.
Mnakumbuka mwezi kama huu mwaka jana tulipewa utabiri wa kila namna kuwa mwaka huu 2017 lazima tutoboe kiuchumi. Tuliaminishwa na kutabiriwa spesfically kabisa na wenzetu walipakwa mafuta na kunyweshwa.
Ila kwa utafiti wangu toka Octoba nimekuwa curious kutaka kujua maoni ya wapendwa wenzangu juu ya hili. Je ni kweli tabiri zile zimezaa matunda?
Kwetu kanisani na hata baadhi ya sehemu nazopendaga kuabudu hali ya Wakristo wengi wako choka mbaya, biashara nyingi zimegoma na deal nyingi zimeyeyuka sana mwaka huu. Wale waliohaidiwa kuolewa hadi leo tumebakiza siku chache mwaka uishe bado ni bila bila....
Naomba nijilizishe toka kwako Mpendwa hivi mautabiri yale yote yalikuwa mbwembwe tu?
Je kweli kwa kadiri tulivyo panda tumevuna?
Naanza kupata mashaka, juhudi zetu za kupanda zinawanufaisha wachache sana huku kundi kubwa tukiishi kwa kujifariji tu!!!
Baba wachungaji karibuni pia mtuambie Mmebarikiwa kwa kiwango gani Kwa kupanda kwenu na sio kwa kupewa na kutumikiwa.
Isije kuwa nyie nanyi ni kama mganga asiyejiganga.... Mnatajirisha wengi ila katu nyie hamuwezi pia kutumia njia na kanuni hizo mkafanikiwa.
Karibuni wapendwa