Karibu Shamba Nurseries
Maumba strt,Boma rd
Njia ya kwenda kwa mkuu wa mkoa,baada ya chuo cha Anglican.
Morogoro
0714 600575 || 0620598113

Huduma zetu
- miche mbalimbali ya matunda,mbao,viungo,tiba nk tunaandaa na kusafirisha
-Tunashauri kuhusu kilimobiashara na masoko
-Tunashauri kuhusu kudhibiti changamoto katika kilimo
-Tunasupply mbegu za miche mbalimbali katika miradi na bustani
-Tunasimamia mashamba na miradi.
Nk

Kwa kawaida miche ikiwa inahamishwa shambani inahitaji kupata joto la wastani wa kati ya 20-27°C japo inawezekana kuvumilia mpaka 30°C,ila ikishafikia 27°c sio salama kwa zoezi la kupanda miche shambani kwako. Kwa sababu inaathiri kushika mizizi na inaweza kuua miche pamoja na kiasi kikubwa cha uvamizi wa wadudu au magonjwa shambani. Sehemu ambazo ni rahisi kuziona au zinaweza kupata changamoto ya joto kali ni kama vile mizizi kuungua,mashina kukauka,majani kupoteza rangi ya kijani na kukauka hivyo kupoteza uwezo wa kujitengenezea chakula.



Madhara ambayo miche inaweza kukumbana nayo ni pamoja na;
i. Mmea kukosa maji au kupoteza maji.
ii. Ardhi kupoteza maji na kupandisha joto.
iii. Mizizi kuungua au kuoza
iv. Miche kukauka
V. Miche kukosa uwezo wa kujitengenezea chakula na upandishaji wa maji.

Changamoto kwa mkulima mwekezaji
i. Hasara ya kiuwekezaji kwa kupoteza Pesa na nguvukazi.
ii. Kuongezeka kwa gharama za umwagiliaji katika miche.
iii. Changamoto ya magonjwa na wadudu
iv. Kupoteza mahusiano mazuri na wafanyakazi au vibarua wake shambani.
V. Gharama za kuzoesha mimea mazingira mapya mfano mifumo ya maji au vivuli zinaweza kuongeza zaidi gharama za kiuwekezaji.

Muda gani ni nzuri wa kupanda miche?
Inategemea na mambo kadhaa kama vile kalenda ya mvua,aina ya miche na hatua ya uwekezaji kwa mradi husika.
a/ Nyakati za siku muda nzuri ni aidha asubuhi sana au jioni walau jua na ardhi linakuwa limepoa.
b/ kipindi ambacho mvua zimenyesha walau mara mbili tatu kwa kuwa zinakuwa zimepoza ardhi.

Njia zipi zinaweza kuwa na matokeo sahihi katika kukabiliana na changamoto ya joto?
Kuna njia kadhaa kama ifuatavyo;
a. Ratiba na njia nzuri ya unwagiliaji walau kupunguza joto katika ardhi kunasaidia kuipa mimea nguvu na uwezo wa kuvumilia.
b. Matandazo iwe hai au Yale yasiyo hai,yanaweza kusaidia kupunguza changamoto kwa maana yanabakiza unyevu nyevu pembezoni mwa mche.
C. Vivuli kwa maana aidha miti au kuweka teknolojia yenye kutoa kivuli kwa miche kupunguza ufikiwaji wa mwanga wa jua moja kwa moja.
d. Uchaguzi wa aina zinazovumilia joto na upotevu wa maji,kwa kila aina hapa kuna aina inavulimia (Wasiliana nasi kwa ushauri zaidi.
e. Kutembelea shamba mara kwa mara na kukagua miche kunasaidia kujua dalili ya changamoto hasa katika majani ya miche kama ni hai au imekufa.
f. Utunzaji wa ardhi yaani kubadilisha muundo wa udongo (soil structure) katika kuupa uwezo wa kutunza maji na kupunguza joto kama vile matumizi ya pumba nk.
g. Kufuata kalenda za utabiri wa hali ya hewa katika kupanda ni jambo jema na zuri katika uwekezaji pamoja na ushauri wa kiutaalamu.
IMG-20231022-WA0010.jpg
IMG-20231018-WA0140.jpg
 
Nimepanda miche na sasa inamatunda ni mipapai inakwenda Kwa kasi. Kila mmoja unazaidi ya matunda 20.
IMG_20240114_113854.jpg
 
Habarini za asubuhi wakuu.
Ni free kabisa,leo tutumie fursa kwa wale wenye challenge ya miti yao ya matunda,viungo au mingine mingine ya muda mrefu muweke matatizo yenu hapa na nitayajibu,lengo la kudisplay na wengine wajifunze,inbox sitajibu kitu. Hii ni njia shirikishi kati yetu. Wiki kuu njema.

Good morning everyone. It's completely free, today let's take advantage of the opportunity for those who have challenges with their fruit trees, spices, or any other long-term issues, share your problems here and I will respond to them. The goal is to display and for others to learn, I won't respond to inbox messages. This is a collaborative way among us. Have a great week.

IMG_20230819_171319061.jpg
IMG_20240304_095403855.jpg
IMG_20240304_095403855.jpg
 
Habarini za asubuhi wakuu.
Ni free kabisa,leo tutumie fursa kwa wale wenye challenge ya miti yao ya matunda,viungo au mingine mingine ya muda mrefu muweke matatizo yenu hapa na nitayajibu,lengo la kudisplay na wengine wajifunze,inbox sitajibu kitu. Hii ni njia shirikishi kati yetu. Wiki kuu njema.


Good morning everyone. It's completely free, today let's take advantage of the opportunity for those who have challenges with their fruit trees, spices, or any Perennial plant issues, share your problems here and I will respond to them. The goal is to display and for others to learn, I won't respond to inbox messages. This is a collaborative way among us. Have a great week.

IMG_20230819_113457526.jpg
IMG_20240304_095403855.jpg
IMG_20231210_142216611.jpg
 
Back
Top Bottom