Uliza swali lolote kuhusu jinsi ya kutumia mtandao kupata wateja!

Dr. Said

Senior Member
Nov 16, 2010
112
526
Hi,

Mimi naitwa Dr. Said Said na ni mkurugenzi wa kampuni ya Online Profits, kampuni inayowasaidia wajasiriamali kama wewe kuweza kunasa wateja kama smaku kupitia mtandao.

Kama unabiashara na unahangaika kupata wateja kutumia mtandao wa intaneti basi nakukaribisha uniulize swali lolote na mimi nitajitahidi kukujibu.

Karibu...
 
Biashara za mtandaoni nyingine zinaambatana na picha ya kitu kinachouzwa, picha huwa nzuri na ya kuvutia nahisi wengi huweka picha za kudownload lakini ukiletewa kitu chenyewe kinakua sio cha kuvutia kama kwenye picha. Je nini kifanyike kuepuka hili?

Kama wewe mnunuzi hakikisha
  1. Unanunua katika tovuti zenye kuaminika
  2. Unasoma description ya product unayotaka kununua
  3. Unasoma reviews za watu ili ujua watu wanasema nini kuhusu muuzaji yule. Kama reviews ni nzuri ila wewe hujaridhika na bidhaa inawezeka hukusoma description ya products vizuri. Kama reviews mbaya usinunue.
Kama wewe muuzaji hakikisha picha unayoweka haitofautiani na bidhaa unayotaka kuuza.
 
Nitumie mbinu gani ili niongeze idadi ya Wateja katika biashara yangu?
 
Naomba mwongozo kufungua sponsored page za fb na instagram

Hakuna kitu kinachoitwa sponsored page. Ila kuna sponsored post ambayo ni post za Facebook au Instagram zinazolipiwa kwa ajili ya kuendesha matangazo.

Kufanya hivyo fuata hatua zifuatazo:
  1. Hakikisha una kurasa ya biashara kwenye Facebook (business page). Kwa maelekezo jinsi ya kufanya hivyo, kasome blog post yetu ya 'Jinsi Ya Kuanzisha kurasa Ya Biashara Kwenye Facebook' hapa.
  2. Weka tangazo lako kwa kufuata linki ifuatayo: Se connecter à Facebook | Facebook
    1. Chagua aina ya tangazo unalotaka
    2. Walenge watu husika
    3. Chagua wapi unataka tangazo lako lionekane. Hakikisha Intagram inakuemo katika chaguo lako.
    4. Lipia tangazo lako. Kufanya hivyo utahitaji visa/mastercard au paypal.
Japokuwa kuna maelezo ya kina natumai utakuwa umepata mwanga.

Nategemea siku za karibuni kuandika post ya kina ya Jinsi Ya Kuweka matangazo kwenye Facebook na Instagram. Nita share humu ili na wewe upate faida.
 
Asante sana nliifungua tayari hio page ila kwenye malipo ndo sikukamilisha na nliona kama gharama sana halaf coverage yake inakua ndogo nitashkuru sana ukiishea hio naomba pia uwekee mkazo sehem ya namna ya kupromote
 
Gharama mbona ya kawaida? Ni budget yako na jinsi unavyolenga watu.

Kasome kitabu changu cha Masoko Facebook kujifunza zaidi.

Ni BURE
 
Hiki ni chakula,mboga. So wanaume kwa wanawake wananunua. My target ni jamii nzima

Bidhaa ambazo hupatikana kiurahisi sokoni ni tabu sana kupata wateja kwenye mtandao kwa sababu watu wengi wanajua wapi wanatakiwa kuenda kupata dagaa.

Ila kama utakuwa na OFA KABAMBE ya muda mfupi isiyopatikana kwengine kokote utaweza kupata wateja wengi.

Ni kuweka tangazo (hususan katika Facebook/Instagram) kuwambia kuwa siku fulani utauza dagaa kwa nusu ya bei (mfano). Waambie kuwa dagaa ni chache na wahakikishe wanawahi kupata OFA hii.

Ila kama OFA yako haitokuwa na mvuto sana utapata shida kupata wateja kupitia mtandao.
 
Nafanya biashara ya kuuza mikoba na Wateja wangu ni wanawake wa rika zote
 
Kwaiyo ukitaka kufungua kampuni account kwa fb au insta kuna malipo yanahitajika?
 
Back
Top Bottom