Uliza swali lolote kuhusiana na kusafiri kwenda nchini Afrika Kusini kwa kutumia barabara

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
4,040
8,895
Wale wote wanaopenda kwenda nchini Afrika Kusini kwa basi au njia ya barabara ila wamekuwa hawana taarifa za kutosha nawakaribisha hapa kuuliza swali lolote nitawajibu.

Pia na wadau wwngine mliowahi kutumia njia hii karibuni mtoe michango yenu tuwasaidie hawa vijana wakasafishe macho kidogo

Kukosa nauli ya ndege haimaanishi ndio usisafiri

Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ivi ni njia gani iliyo nyepesi kwa njia hizi mbili, moja njia ya mtwara ama njia ya tunduma na ipi gharama yake ni nafuu kati ya njia hizo mbili
 
Nauli bei gan, vip natakiwa niwe na vitambulisho gani, vip hotel za kufikia, vip kuhusu swala la comfort ktk safari, isijekuwa mateso kama ya wana wa israel

Naomba kujua kutoka dar had kwa madiba kwa bas ni bei gani, nataka nizamie nikajaribu maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Kutoka Tunduma/Nakonde hadi Lusaka ni Kwacha 260h hadi 290( 50000 hadi 65000 hivi).
Kutoka Lusaka hadi Johburg/South Africa Kwacha 850( 150000 za kibongo).
Bei hizo ni za wiki hizi mbili-UPDATED.
MABASI YA UHAKIKA TUMIA KAMPUNI YA JULDAN BUS. HAWA UTAPANDIA NAKONDE HADI LUSAKA WATAKUFAULISHA KWENYE BASI LAO JINGINE KUBWA SANA LINALOVUKA BORDER HADI SOUTH..

Ok sawa,na inaweza chukua siku ngapi mpaka kufika
 
Ok sawa,na inaweza chukua siku ngapi mpaka kufika
Safari yote inachukua siku nne mpaka tano kama hakuna matatizo yoyote njian ama break down, inatakiwa usiwe na pesa chini ya laki tatu kwa gharama za kusafiri tu mpaka unaingia Jo'burg , ila siku iz cio mahala pazur kwenda, wazulu wamebadilika,wabaguz,wakatili,wanachukia wageni hasa weusi wenzao, pale south Africa kuna uhalifu mkubwa unaofanywa na watu weusi ivyo tumepoteza sifa yetu ya kuonekana ni watu wema,#kasikilize wimbo wa inspector aroun unaitwa NJE NDANI#

Inamaana nikitaka kwenda na kurudi niandae kama laki sita sio
 
Hivi kwa wanaojua kati ya Johannesburg, Pretoria na Cape town ni jiji gani ambalo ni zuri, salama, lenye wenyeji wakarimu na pia gharama nafuu zaidi kwa kutembelea na familia kwa ajili ya mapumziko tu ya kama wiki mbili?
 
Ok sawa,na inaweza chukua siku ngapi mpaka kufika
Kutoka Nakonde/Tunduma hadi Lusaka siku moja, kutoka Lusaka hadi Johburg masaa 24 Non-stop ila kuna border mbili lazima msimame ya kwanza inaitwa Chirundu hii ni Zambia kuingia Zimbabwe hapa ni nusu saa au saa moja mmevuka, ipo nyingine inatwa BEITBRIDGE Kutoka Zimbabwe kuingia Afrika kusini hapa lazima msimame masaa 2 hadi 5. Wanakagua balaa. Ila kama una passport na yellowa fever haina shida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi upatikanaje wa ajira kwa ujumla na ukoje huko kwa sie wenye elimu ya form four?

Na kuna fursa gani nzuri zaid ya usajaji wa ajira?

Pia weka ufafanuzi khs visa na kama kuna usmbufu kuingia south africa border.

Pia gharama za pakulala za bei rahs na chakula, ili kama mtu anajipanga kwenda kutafuta maisha ajiandae kwa sh ngaoi kwa muda fulani.
 
Mabasi yenyewe ndio hayo
IMG_20190111_112253.jpeg
IMG_20190111_112250.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom