Uliza swali lolote juu ya Afya ya Ngozi


ZAGANZA

ZAGANZA

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Messages
639
Likes
308
Points
80
Age
33
ZAGANZA

ZAGANZA

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2014
639 308 80
AINA ZA NGOZI.
Kuna aina nne za ngozi ya binadamu:

1.Ngozi ya kawaida(Normal Skin)

Hii ni ngozi ambayo ina mafuta na unyevu wa kawaida kwa ajili ya ustawi mzuri wa ngozi, hivyo huwa ni ngozi isiyo na mikunjo ya aina yeyote na huonekana vizuri. Pia ni ngozi ambayo ni vigumu kuwa na chunusi na matatizo mengine ambayo yanapatikana katika aina nyingine za ngozi. Kwa hiyo ni ngozi inayohitaji matunzo ya kawaida kama vile, kuisafisha na kuipatia unyevu wa kawaida kabisa(moisture).

2.Ngozi kavu(Dry Skin)
Ni ngozi ambayo ni rahisi kujikunja(wrinkles) na hivyo kuzeeka haraka na hii hutokana na kiasi kidogo cha mafuta kinachotengenezwa katika mwili. Hii ni ngozi ambayo haiendani na mazingira ya baridi kwani huwa kavu sana. Hii ni ngozi ambayo inahitaji unyevu(moisture) kwa wingi,kwa hiyo ni vyema kutumia vipodozi ambavyo vina unyevu mwingi mchana na usiku unapolala ili kuzuia mikunjo(wrinkles) na muonekano wa kuzeka kwa ngozi.

3.Ngozi yenye mafuta(Oil Skin)
Hii ni aina ya ngozi yenye mafuta mengi na hivyo kupelekea mtu kung’aa na hivyo kukosa mvuto. Pia ni ngozi ambayo ina uwezo wa kushika uchafu kama vumbi kutoka kwenye mazingira na hivyo kuonekana ni chafu.
Pia ni ngozi ambayo ni rahisi kuwa na chunusi kutokana na hayo mafuta pamoja na sababu zingine,hivyo inahitaji matunzo mazuri na ya kila siku ili kupunguza au kuondoa matatizo yanayoambatana na aina hii ya ngozi. Watu wenye ngozi ya aina hii wanatakiwa wawe na mtindo mzuri wa kimaisha ikiwa ni pamoja na vyakula wanavyokula,hali ya usafi na kutumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yao, ambapo vitu vyote vikifanyika kwa usahihi vitafanya ngozi iwe ni nzuri na yenye mvuto.
Kitu kizuri kwa watu wenye ngozi yenye mafuta ni kwamba ngozi zao hazipati mikunjo(wrinkles) na hivyo ngozi zao hazizeeki mapema.

4.Ngozi ya mchanganyiko(Combination Skin)
Hii ni ngozi ambayo ina sehemu ambazo zina mafuta na sehemu nyingine ambazo ni kavu, hivyo ni mchanganyiko wa ngozi yenye mafuta na ngozi kavu au ngozi ya kawaida.
Mara nyingi sehemu za uso kama vile paji la uso,kwenye pua na kwenye kidevu kunakuwa na mafuta mengi, wakati sehemu za shavuni na maeneo yote kuzunguka mdomo na macho huwa ni kavu.
Hapa unatakiwa utunze hizo sehemu za ngozi kutokana na aina yake,kama hiyo sehemu ina mafuta, tunza kama ngozi yenye mafuta,pia tumia njia za kutunza ngozi kavu sehemu ambapo kuna ngozi kavu.

JINSI YA KUWEZA KUITAMBUA NGOZI YAKO NI YA AINA GANI


Ni vizuri sana kwako kuweza kujua aina ya ngozi yako maana itasidia wewe uweze kuitunza ngozi yako vizuri.Vile vile itakusaidi katika kujua ni vipozi vya aina gani utumie kutokana na ngozi yako. Hakuna ngozi mbili ambazo zinafanana exactly ila zinatofautiana ambapo inawezekana ngozi yako ikawa ni Ngozi Kavu, Ngozi ya Kawaida, Ngozi ya mafuta na ngozi mchanganyiko yaani combine skin.Ili kujua ngozi yako ni ya aina gani osha uso wako kwa kutumia sabuni ya kusafishia uso then baada ya dakika 30 chukua tishu na futa sehemu ya paji lako la uso, kwenye pua, kidevu na mashavu.

Kama tishu hiyo haitaonyesha kuwana mafuta baada ya kufuta basi ngozi yako itakua ni aina ya ngozi kavu.
Ngozi kavu huwa inaonekana rough na hukabiliwana mistari na wrinkles lakini kama ngozi yako kuna sehemu nyingine inakua kavu sehemu nyingine inakua na mafuta basi ngozi yako itakua ni ngozi mchanganyiko.
Ngozi ya kawaida au Normal skin huwa inaonekana laini na ngozi hii ya mafuta ukiigusa unayahisi mafuta na huwa inang`aa. Ngozi hii ya mafuta huwa inakabiliwa sana na blackheads na pimples/chunusi na kwa kuwa ngozi hii ni sensitive inahitaji special care na umakini na vipodozi unavyopaka kwenye uso wako.
Kwa watu wenye ngozi sensitive kama hii ni lazima kutumia misaada ya ushauri kwa wataalamu wa ngozi ili kulinda ngozi zao kupata mzio/allergic. Ni lazima mara kwa mara uwe na utaratibu maalum wa kuihudumia ngozi yako kulingana na mahitaji ya ngozi yako na huenda ikachukua muda mrefu kwa ngozi yako kurudia hali ya kawaida kuweza kuondokana na hili tatizo.

Kwa ushauri BURE juu ya afya ya ngozi yake, wasiliana nami

0713 03 98 75
Bro.Mussa,
Mtaalamu wa Afya ya Ngozi
 

Attachments:

M

mselambaya

Member
Joined
Jan 10, 2017
Messages
94
Likes
56
Points
25
Age
24
M

mselambaya

Member
Joined Jan 10, 2017
94 56 25
Kuna Dawa ya kuondoa kovu kwenye ngozi ya uso
 
sonnita

sonnita

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2014
Messages
904
Likes
251
Points
80
Age
29
sonnita

sonnita

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2014
904 251 80
Kuna njia ya kuondoa facial black spots naturally? (vilivyotokana na vipele vilivyoisha/kukauka/kutumbuliwa)
 
ZAGANZA

ZAGANZA

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Messages
639
Likes
308
Points
80
Age
33
ZAGANZA

ZAGANZA

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2014
639 308 80
Kuna njia ya kuondoa facial black spots naturally? (vilivyotokana na vipele vilivyoisha/kukauka/kutumbuliwa)
Tumia natural Clay , piga: 0713-039875
 

Forum statistics

Threads 1,262,530
Members 485,585
Posts 30,124,993