Uliza swali lako kuhusu CFD, Options, Bonds, Stocks and Currency Trading (Forex)

Ego is the Enemy

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
7,398
14,155
Habari zenu wanajamii forum!

Kama kichwa cha habari kilivyo nipo hapa kuisaidia umma Wa watanzania kuhusiana na biashara hizi ambazo zimeibuka ivi karibuni kwetu huku lakini ila huko nje ni biashara za muda mrefu sana tokea huko karne ya 18.

Sie tumezipata kutokana na ujio Wa simu janja ikiwa imeunganishwa na internet.

Watu wanajua kuwa kuna upigwaji kweli Upo kwa watu wengine kuwaambia wengine wao ni Guru wanawapiga pesa.
Kama tulivyoshuhudia huko kama miaka mitatu inapita ivi.

Ishu hii ni halali sema inatakiwa upate MTU sahihi sana akuelekeze ila siye mwenye kuweka Hela mbele.

Ukweli ni kuwa unaweza ukafanya kama kamari na unaweza ukaifanya kama biashara zingine tu.

Na uzuri Wa hii kuijua hakuna cha TRA,wateja,bosi,wala nani yaani hakuna kubembeleza mteja.

Pia kumbuka ni fani kama fani zingine zilivyo jamani mfano kuwa mfanyabiashara mkubwa ana uzoefu Wa kutosha na sio kuwa amelala na kuamka akajikuta hapo alipo.

Ni kama ilivyo sheria, engineering, Doctor of Medicine, mhasibu ama mwalimu.so hakuna ulelemama kuwa kuna pesa nyepesi kama wengi wanavyoinadi.

Binafsi nimejitoa kwa biashara hii hata kama itakuja kunilipa huko mbele kwa miaka 20 tokea sasa siogopi mana hakuna mafanikio cheap tunavyopenda binadamu.

Ila ni nzuri ukiijua unachofanya.

Biashara hii ni suala zima kuhusu psychology.

Pia haitakiwi ufanye live trades before ya demo trading na umeki faida kwa demo account kama mwaka mzima ndo uamue kuingia huko kwa live trades.

Wengi wanafundisha watu kwa kuwapotosha kuwa kuna pesa laini.

Hii fani sintoiacha mana najua hata wanangu nitawafundisha maarifa yake so yaweza kutokea kwao matunda.

Yaani unaipofanya tegemea miaka mitano ama kumi huko mbeleni kabisa usiwe na haraka na utoe mawazo ya Hela kichwani.
Usiwe kama students eti ni fani gani yenye kulipwa pesa nyingi.

Binafsi napenda niwe Nina interact na watu wenye passion nayo mana shuleni huwezi ukakaa mwenyewe. Pia unawafundisha wasio ijua kuna vitu unaimprove. Kwa wale walikuwa wanawaelekeza wenzao shuleni nadhani unajua unaletewa swali hulijui ila unashangaa unalijibu na unapata solutions fasta sana.
 
Forex ndo imekuwa maarufu sana hapa nyumbani ivyo wengi wanajua.
Hizi ni liquid market yaani ni easy kuibadilisha bidhaa kuwa Hela yaani ni haraka sana.
Mfano ni rahisi sana kuuza Hela yako iliyoko kwa Mpesa kuwa Hela halisi kuliko kuuza kiwanja chako. Ivyo kiwanja ni illiquid asset.
Hizi kama stocks ama bonds aka security assets.
 
Pia mkumbuke kuwa tuna move from analogy to digital world. Yaani kwa siku zijazo mambo mengi sana itakuwa unaingia online tu unacheki.
Hata Malaya Tanzania nimeona wameanza na wame move into Digital world. Binafsi napenda sana digital Yaani hakuna kubembelezana wala kumlamba MTU ili aje kununua dukani kwako.
Pia muda huu badala ya kutumia kwa mambo ambayo hayana faida ni bora niwe natoa hapa darasa huru kuhusu uwekezaji huu.
 
Nasikia bot ashakunya, na mavi wameyarushia forex... 😂😂
Sasa mtafanyaje baada ya shambulizi hilo..??
 
Stocks ni kama mfano kwa nje ambao haya mambo yameendelea Sana mana sie wengine kila kitu tunakopi tokea kwao.
Mfano wake ni; Apple, Amazon,alibaba,Bac,BIdu,googl ntflx ,Tesla,twtr na Microsoft.
Kwa hapa nyumbani ni kama TWIGA cement, crdb,NMG,swala,DCB, mkcb,tbl,tpcc na nyinginezo nyingi
Hii ni elimu ambayo inatakiwa umpatie mwanao akiwa mdogo sana.
Hapa ukiwa mwekezaji unanunua hisa za kampuni husika ambayo unaona kuwa kulingana na mwenendo Wa uchumi itafanya vizuri. Mfano halisi awamu hii ujenzi sana umefanyika ivyo hisa za kampuni ya TWIGA lazima zipande thamani yaani kiwanda kitapata faida. Na ivyo na ile gharama ya uwekezaji wako lazima ipande kama mfano ulinunua hisa moja sh 20k TZS utajikuta imekuwa 23k TZS ivyo utapata faida ya sh 3 kama umenunua hisa zako hata laki ama Milioni angalia utakuwa una sh ngapi.

Hii Mara nyingi inakuja kuwa unajikuta una Hela afu huwezi kuifanyia biashara. Kuna watu wanakula faida za hisa huko ulaya walizinunua mababu zao wao ni kupata gawio tu.
 
Nasikia bot ashakunya, na mavi wameyarushia forex... 😂😂
Sasa mtafanyaje baada ya shambulizi hilo..??
Acha maneno ya kusikia kaka naomba ukasome vizuri hiyo habari ndugu.

Hii ni biashara kama biashara zingine sema hapa nyumbani ni ngeni watu wengi hatuijui.
Mana mtandaoni tunashinda kuongea vumbi LA longo na kung'oa pisi Kali jamani na huko Instagram ni show off za kutosha. Na kuangalia mambo ambayo hata hayakuongezei chochote kwenye akili yako
 
Unavyonunua hisa za kampuni lazima ufanye uchunguzi ama analysis ya kampuni kuhusu balance sheet zao uone liability na assets mpaka faida na loss kwa mwaka husika ujiridhishe kwanza.
Mfano Warren Buffet aliyajua haya mambo tokea akiwa mdogo sana mana baba yake alikuwa ni stock broker Ilikuwa ni rahisi sana Ku develop talent yake.
Ni kama umezaliwa kwenu ng'ombe wapo ni rahisi sana kuijua ng'ombe ilivyo na akili yako itakaa ivyo ivyo King'ombe ng'ombe. naombeni haya masomo tuwafundishe watoto wetu wanapokuwa wadogo. Mana haya masomo hayafundishwi huko mashuleni.
Kuliko mtoto anakaa anamaliza muda wake anaangalia TV ambayo itamjaza uchafu kichwani.
 
Ukiona mwenendo Wa uchumi Wa bidhaa Fulani unawekeza huko. Mfano saivi huwezi ukanunua hisa za tbl unywaji umeshuka na mfano koka kola sijui kama PLC imeshambuliwa na kinywaji vingine mbadala akina Azam ana Mo. So lazima uuzaji uushuke.
Stocks ndo ziko kama ivyo
 
Kwa mfano saivi ukiangalia stocks za voda hapa nyumbani zimeshuka wakati ule qa IPO Ilikuwa ni sh 850 ila saivi ukizipeleka crdb wazinunue watakupa sh 770 kila moja.
Pia wapo stockbrokers ambao hawa wananunua stocks kwa ya jumla tokea kampuni hiusika mana huwa kuna kiwango cha chini kununua . so wao ni wananunua jumla wana uza rejareja kwa anayetaka idadi yoyote kulingana na Hela yake.
Yaani ni kama unampatia MTU Hela yako anafanyia kazi akipata faida anakupa gawio sio lazima wote tufanye biashara.
Mfano saivi hali mabenki sio nzuri ivyo lazima hisa zao zitakuwa chini ivyo ni muda Wa kuzinunua mana awamu inayokuja itakuwa ni ya nzuri ila na assume tu.
Ivyo benki zitafanya sana kazi zitazalisha faida na stocks zao zitapanda utajikuta umetengeneza Hela huku umekaa tu.
Ila kumbuka hali ikiendelea kuwa mbaya thamani ya hisa zinaporomoka na pesa yako inashuka thamani pia.
Jamani hakuna pesa nyepesi hata ulaya pesa ni ngumu pia.
 
Ukiona hali ya uchumi ni nzuri watu wanakunywa bia sana ni muda Wa kununua hisa za tbl . kwenye nchi zilizoendelea haya mambo ukinunua tu hisa wadau ni wengi sana.
Jamani nimeona nisaidie Tanzania kwa nililo nalo hata nikija kufa watu watakuja kuukuta huu Uzi watajifunza kitu na kunishukuru humohumo kaburini.
 
Ukiona watu wanaishambulia bidhaa Fulani sana tena sana ni muda Wa kuwaza kuwekeza na kampuni iyo pia.
Uwekezaji mwingine unatazama mbele mfano miaka 10,20,30 mpaka 100 utakuja kuwaje wekezeni hata kwa wajukuu wenu. Aliye utengenezewa njia inakuwa ni rahisi kuzidi kufika mbali sema jamii zetu nyingi sana ni masikini sana tena sana. Ila waza mbele huko kuwa benki ya NMB itakuwa je kiuchumi. Wekeza nao faida unakuja kuivuna huko mbele sana.
 
Wale wawekezaji Wa kimataifa wenye Dola bilioni ambao hapa Tanzania ni Wa Ku hesabu na sidhani kama kumi wanaweza fika kabla ya kuwekeza kwenye stocks za nchi Fulani lazima waangalie hali ya utulivu Wa kisiasa ulivyo.
Ndo mana nchi iliyotulia kisiasa ni lazima kuendelea ila kodi lazima walipe tena wako strictly sana.

Mfano kuna Mortgage hizi ni share za kampuni zinazojenga nyumba ama apartments kupangisha na kuziuza huko nje demand ni kubwa sana.
Kuna miaka Fulani ivi japan waliwekeza kwenye kampauni Kama hizi huko USA ila kuna economic crisis ilitokeaga zikashuka Sana wakapata pigo kubwa. Ilikuwa ni ile ya 2008.
Saivi nyumba zipo nyingi huko USA zinataka wapangaji ama wateja Wa kuzinunua. Huko Dubai unaweza ukamiliki chumba cha hotel mteja akiingia unalipwa Hela na Uko hapa Tanzania.
 
Hayupo hapa kutambiana ama kuonyeshana kuwa huyu anajua kuliko mwingine hapana.
Leo nadhani suala zima LA stocks kitakuwa limeeleweka.
 
Back
Top Bottom