Uliza jambo lolote kuhusu Bahari na safari na vimbwanga vya Baharini

Mkuu, ulishawahi kukutana na majini ukiwa safarini, yaani kupakia abiria kumbe ni jini kufika katikati ya bahari anazama baharini.
Nishawapakia sana tena mmoja alinipa elimu ya utambuzi mambo siwezi kuyasema sana nachokumbuka kuna siku ilikuwa nimebeba sukari na mafuta ya kupikia mzigo unafikia milioni nne natoka zenji naitafuta mafia boti ya mali asili ikawa inatufkuza jini ndo alonipa elimu ya kuchuka kindu saba na kutupa baharini siwezi sema sana naweza nkawaharibia wenzangu jini ni kiumbe kama wengine tu naweza kusema hapa kwakuwa ni mambo ya kuamini wadau hapa wengine watanipopoa
 
Kila nikikumbuka hiki kisa naumia sana. Hao mmoja ni ndugu yangu. Mliwezaje kujua kama ni nusu saa ilikuwa imepita mlipo ikuta boti?
Mlipofika pwani na kutoa taarifa ilikuwa ni wastani wa muda gani toka muione boti yao baharini?
Kwa taarifa nilizopata hao watu walikodi Fiber Boat toka Nyamisati iwapeleke Mafia, so kuna baadhi ya Abiria waliiona ile boat ikiwa Nyamisati, so hata tulivyoikuta ile boat juu chini kwanza hatukujua kama Ndo ile Ilikua na Mzungu na baadhi ya Waswahili, baada ya kufika Mafia Nahodha ndo anatoa taarifa kuhusu kuiona ile Fiber Boat, Ndo anapewa habari kuwa kuna Boat imepinduka......

Baada ya siku 4 narudi Nyamisati Naambiwa Nahodha aliyekuwa anaendesha ile Boat ilopinduka alirudi akiwa anaogelea mpaka Maeneo ya Nyamisati, akiwa kavaa Life Jacket......

Toka Nyamisati mpaka Mafia ni Masaa 4 kwa mwendo wa Boat zetu za Kiswahili.
 
hapa jibu ninalotoa ni yale ninayo yaelewa mimi nayokutana nayo mfano huwezi kuniuliza kitaalamu kwann vibwengo huwapoteza watu usiku baharini sasa unataka nijibu vp kitaalam mimi najibu uhalisia ule nnaokutana nao uliza je ushawah pakia magendo ndo ntakujibu kitaalam .silali na deni mpuuzi mwenyewe
Hahahahahah Brother wazoee na kuwapuuza ndo wanadam hao,
Mkuu tupe kisaa walao kimoja cha vibwengo, na je wakojeee??
 
Nishawapakia sana tena mmoja alinipa elimu ya utambuzi mambo siwezi kuyasema sana nachokumbuka kuna siku ilikuwa nimebeba sukari na mafuta ya kupikia mzigo unafikia milioni nne natoka zenji naitafuta mafia boti ya mali asili ikawa inatufkuza jini ndo alonipa elimu ya kuchuka kindu saba na kutupa baharini siwezi sema sana naweza nkawaharibia wenzangu jini ni kiumbe kama wengine tu naweza kusema hapa kwakuwa ni mambo ya kuamini wadau hapa wengine watanipopoa

Hahaha, hizi ndo story tulizotegemea kuzipata. Ila sasa nazo zina vikwazo·
 
Mkuu kuna bahari mbili zimeungana moja ina maji chumvi na nyingine ina maji ya kawaida pale unaizungumziaje
Naomba nikujibu Kama hutojali,

Maji ya BAHARI Yana sifa ya kuwa na CHUMVI, hivyo pale BAHARI zinapokutana MAJI yote huwa na CHUMVI sema kwa KIWANGO tofauti.
 
Back
Top Bottom