Uliza jambo lolote kuhusu Bahari na safari na vimbwanga vya Baharini

chongoe

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,128
2,717
Habari zenu waungwana,

Leo nipo hapa kwa ajili ya maswali ambayo yanahusu mambo ya bahari tu. Mimi ni nahodha wa majahazi ya mizigo Mafia, Kisiju, Kilwa, Nyamisati na Koma.

Uliza swali linalohusu maeneo hayo pia kuhusu safari na vimbwanga vya baharini.

Karibuni.
 
Bamvua ni nini?
Bamvua ni maji ambayo mengi hasa yale ambayo huanza kujaa wakati mwezi huchomoza usiku mfano mwezi kumi na tano au kumi na nane maana maji yake ya usiku huwa ni mengi sana hata mchana pia huwa tofauti na siku ingine maana halisi ya bamvua ni maji kuwa mengi kwakuwa kuna kipindi maji huwa machache mfano maji mafu
 
Ukishawahi kufika kwenye kile kisiwa karibu na Nyamisati ilipozama meli kubwa ya kivita ya wajerumani?

Jr
Kisiwa cha Salale nishafika pale najua mwanzo mwisho baada ya vita kuisha baadhi ya wazungu ambao walijificha maeneo yale sasa wakati wanataka kuondoka warudi kwao kuna mzee mmoja ndio aliwasaidia pale kisiwani muda ulipokaribia wakuondoka wakamuuliza yule mzee sisi tunaondoka unataka nini tukufanyie yule mzee akawaambia nataka redio na kweli akapewa redio
 
Bila shaka wewe ni mtu wa Pwani. Kumekua namatatzo sana kuhusu huduma za usafiri hasa wamizigo kwa visiwa vya Unguja na Pemba, Mafia mpaka Comoro, shida hasa inakua ni nini mpaka kuwa ni tatizo kiasi hichi?

Niliwahi sikia kua upande huo kunakuaga na upepo mkali na vimbunga mara kwa mara?
 
Back
Top Bottom