Uliza chochote kuhusu unenepeshaji mbuzi, kilimo na biashara ujibiwe

Kigoma, Pwani na Dar es salaam.
Ndugu upo Dar sehemu gani? ufugaji wako unaufanyia kigoma au Dar. Kama hauto jali ningeomba tutembelane kwenye mashamba yetu ya ufugaji mimi nipo Dar kibamba ninaufugaji wa Mbuzi na nahitaji baadhi ya mbegu kutoka Kigoma kunawale wa mgongo mpana wazaao mapacha nawahitaji 4.
 
Mbuzi kuzaa mapacha au 3 inategemeana na ukoo aliotokea, mara nyingi huwa watu wanataka Mbuzi wanao zaa mapacha lakini kuna baadhi ya wafugaji wasio waaminifu huwapatia wenzao Mbuzi asie zaa mapacha mwisho huyo anaetaka kuanza ufugaji hapati matokeo yanayo stahili.
Nakushauri ukihitaji mbuzi wa mapacha fanya utafiti wa kizazi na kuwaangalia kwa umakini maana kuna baadhi ya vitu vya ambavyo vitakusaidia kumtambua Mbuzi azaae mapacha.
Shukrani kwa maelezo mazuri,ningelipenda kujua ni vitu gani ambavyo vinaweza kusaidia kutambua kuwa huyu ni wa ukoo wa mapacha,mfano kwa jike ambaye hana watoto wakati wa kumununua,asante
 
Mkuu kuna mdogo angu anataka kuanza kufuga kapata aina ya zile mbuzi zinazo zaa mapacha ajawai ata kufuga kaanza na watano ni vitu gani vya kuzingatia mkuu ushauri tafadhari na madawa yapi ya kutumia
Sawa napenda kujua anafuga tu kizamani au anafuga kisasa(kunenepeshwa)...?
 
Mkuu naomba kujua kuhusiana na suala la mbuzi kuzaa mapacha na wengine wanafikia hata kuzaa wanne kwa wakati mmoja,je hii ni ukoo wa mbuzi au kuna jinsi unaweza ukawafanya wakazaa hivyo?
Hii hasa huwa ni Ukoo wa mbuzi na Aina ya mbegu wa mbuzi husika
 
Mkuu naomba kujua kuhusiana na mbuzi kuzaa mapacha na wengine wanafikia hata kuzaa wanne kwa wakati mmoja,je hii hutegemea ukoo wa mbuzi au kuna jinsi unaweza ukawafanya wakazaa hivyo?
Hiyo nikutokana na Ukoo pamoja na aina ya mbegu wa mbuzi husika.
 
Mbuzi kuzaa mapacha au 3 inategemeana na ukoo aliotokea, mara nyingi huwa watu wanataka Mbuzi wanao zaa mapacha lakini kuna baadhi ya wafugaji wasio waaminifu huwapatia wenzao Mbuzi asie zaa mapacha mwisho huyo anaetaka kuanza ufugaji hapati matokeo yanayo stahili.
Nakushauri ukihitaji mbuzi wa mapacha fanya utafiti wa kizazi na kuwaangalia kwa umakini maana kuna baadhi ya vitu vya ambavyo vitakusaidia kumtambua Mbuzi azaae mapacha.
Asante sana naona umemaliza kila kitu.
 
Mkuu eneo la mbeya au dodoma wapi panafaa kufuga mbuzi kitokana na hali ya hewa
Kwa Mbuzi wa maziwa Mby,Iringa,Moro, Moshi kunafaa sana maana hawapatani sana na joto na wana penda sana kufugwa kwa mtindo wa zero grazing. kwa mbuzi wa nyama Dodoma kuna faa, ila cha msingi kwanza ujuwe unataka kufuga mbuzi wa aina gani na ufanye utafiti wa mbegu zilizo bora kwa mahitaji na eneo husika, Mimi nimejaribu wamaziwa kwa Dar kidogo ni changamito hasa wakati wa jua kali.
 
Mfano nikawa na mbuzi 50 niahitaji kua na shamba la ukubwa gan?
Kwanza kabisa unataka kufuga kwa njia ipi, free zone au Zero grazing? Na ujuwe unataka kufuga Mbuzi gani wa Maziwa au Wanyama? ukisha jua aina na mfumo wa ufugaji unaoutaka ndipo utafiti kiwango cha eneo linalo kutosha kufugia, Mf Mimi nafuga kwa free zone kuwachunga wamaziwa wameshindwa kuendana na mfumo huo wa kuwachunga kwa hiyo nimebakia na hawa wa nyama peke yake na sasa nataka kuweka mbegu ya Isiolo kwaajili ya nyama na nitawa cross na hawa wakienyeji.
 
Kwa Mbuzi wa maziwa Mby,Iringa,Moro, Moshi kunafaa sana maana hawapatani sana na joto na wana penda sana kufugwa kwa mtindo wa zero grazing. kwa mbuzi wa nyama Dodoma kuna faa, ila cha msingi kwanza ujuwe unataka kufuga mbuzi wa aina gani na ufanye utafiti wa mbegu zilizo bora kwa mahitaji na eneo husika, Mimi nimejaribu wamaziwa kwa Dar kidogo ni changamito hasa wakati wa jua kali.
Shukrani boss
 
Kwanza kabisa unataka kufuga kwa njia ipi, free zone au Zero grazing? Na ujuwe unataka kufuga Mbuzi gani wa Maziwa au Wanyama? ukisha jua aina na mfumo wa ufugaji unaoutaka ndipo utafiti kiwango cha eneo linalo kutosha kufugia, Mf Mimi nafuga kwa free zone kuwachunga wamaziwa wameshindwa kuendana na mfumo huo wa kuwachunga kwa hiyo nimebakia na hawa wa nyama peke yake na sasa nataka kuweka mbegu ya Isiolo kwaajili ya nyama na nitawa cross na hawa wakienyeji.
Mkuu mbegu ya Isiolo inapatikana wapi
 
Arusha ndugu tena hapa nafanya juhudi mwisho wa mwezi wa mwezi nikabebe mbegu.
Naomba unipe address wanapatikana wapi Arusha niwafuate. Maana Nina mpango kwenda kuchukua wale kondoo wenye mikia mikubwa Lake Natron ambao wanatoka Narok Kenya. Kama unahofu ya ku share address ,nitumie inbox plz. Na wanauzwaje.
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
Shukrani sana kwa darsa.
Naomba kuuliza.
Nimeona mabanda mengi ya Mbuzi yanajengwa kwa Mabanzi.
Mpk sakafu ni Mabanzi. Je? Sakafu ya Mabanzi haiwezi kuoza kutokana na Mikojo na kinyesi cha Mbuzi?
 
✓Yeah kwa hapa Tanzania minada mikubwa ipo Dar es salaam hasa pugu pamoja na vingunguti, lakini pia kwa dodoma kidogo hasa mbande-kongwa.

✓Changamoto zipo lakini inatokana na uhitaji wako Kama ni wakufuga tu au kunenepesha, maana Kuna sifa zinazohitajika kujua Kama mbuzi huyu ni wakunenepesha au laaah, na hapo ndo watu wengi wanakosa elimu ya kujua ni Aina gani wa mbuzi anahitajika kunenepeshwa.

✓Changamoto ya usafirishaji ni hasa kupata magari kwa wakati na umbali pia ni changamoto sana hasa kwa mbuzi wa kunenepeshwa maana uchangia wawe stressed na kupoteza uzito unaotakiwa ili waweze kunenepeshwa.

~kigoma.
Naomba kujua ratio ya idadi ya Mbuzi per square meter. Mf nikiwa na BANDA la 100 sqm ..... kwa Mbuzi wa kienyeji naweza fuga wangapi?
 
Naomba unipe address wanapatikana wapi Arusha niwafuate. Maana Nina mpango kwenda kuchukua wale kondoo wenye mikia mikubwa Lake Natron ambao wanatoka Narok Kenya. Kama unahofu ya ku share address ,nitumie inbox plz. Na wanauzwaje.
Kule Arusha tunakwenda kwa wafugaji wa Masai ndugu basi ndipo unaweza pata mbuzi wa kweli ukipita kwa
 
Back
Top Bottom