Uliza chochote kuhusu unenepeshaji mbuzi, kilimo na biashara ujibiwe

Minada ya mbuzi inapatikana wapi na vipi changamoto za usafirishaji na unenepeshaji kwa ajili ya biashara.
 
Asante , Mkuu last time nimeandaa kitalu cha miche ya Nyanya chungu wengine waita "Ngongwe" miche ilitoka vizuri ila baada ya muda ikaanza kunyauka yenyewe na maji nlikua namwagilia vizuri tu !! Nikaandaa tena ila matokeo yakawa yaleyale.

Baadhi ya watu wakasema kwamba huenda maji ya chumvi yana impact mbaya !! Je ni kweli kuna baadhi ya mazao hayaendani na maji ya chumvi au ? Baadhi ya mazao yanaenda vizuri tu ! Bamia , Hoho, Bilinganya , na Nyanya !!
 
Minada ya mbuzi inapatikana wapi na vipi changamoto za usafirishaji na unenepeshaji kwa ajili ya biashara.
✓Yeah kwa hapa Tanzania minada mikubwa ipo Dar es salaam hasa pugu pamoja na vingunguti, lakini pia kwa dodoma kidogo hasa mbande-kongwa.

✓Changamoto zipo lakini inatokana na uhitaji wako Kama ni wakufuga tu au kunenepesha, maana Kuna sifa zinazohitajika kujua Kama mbuzi huyu ni wakunenepesha au laaah, na hapo ndo watu wengi wanakosa elimu ya kujua ni Aina gani wa mbuzi anahitajika kunenepeshwa.

✓Changamoto ya usafirishaji ni hasa kupata magari kwa wakati na umbali pia ni changamoto sana hasa kwa mbuzi wa kunenepeshwa maana uchangia wawe stressed na kupoteza uzito unaotakiwa ili waweze kunenepeshwa.

~kigoma.
 
Asante , Mkuu last time nimeandaa kitalu cha miche ya Nyanya chungu wengine waita "Ngongwe" miche ilitoka vizuri ila baada ya muda ikaanza kunyauka yenyewe na maji nlikua namwagilia vizuri tu !! Nikaandaa tena ila matokeo yakawa yaleyale. Baadhi ya watu wakasema kwamba huenda maji ya chumvi yana impact mbaya !! Je ni kweli kuna baadhi ya mazao hayaendani na maji ya chumvi au ? Baadhi ya mazao yanaenda vizuri tu ! Bamia , Hoho, Bilinganya , na Nyanya !!
✓Yeah ninkweli kabisa baadhi ya mazao hayaendani na maji ya chumvi hasa nyanya, na nzuri zaidi Kama unafuatiliaga wanaofanya kilimo Cha horticulture wengi wana fanyiaga kwenye mabonde na hayo huwaga wanaotumia maji ambayo so ya chumvi na mazao huwa mazuri sana.

✓Pia,sio tu maji yanaweza yakawa Yana changia lakini inawezekana Kuna sababu kem kem Kama ardhi yenyewe, wadudu na pia mbolea unayotumia.

✓Nakushauri sana uanze kutumia Drip irrigation maana huwaga nzuri sana kumlinganisha na irrigation za kawaida.

~kigoma.
 
✓Yeah kwa hapa Tanzania minada mikubwa ipo Dar es salaam hasa pugu pamoja na vingunguti, lakini pia kwa dodoma kidogo hasa mbande-kongwa.

✓Changamoto zipo lakini inatokana na uhitaji wako Kama ni wakufuga tu au kunenepesha, maana Kuna sifa zinazohitajika kujua Kama mbuzi huyu ni wakunenepesha au laaah, na hapo ndo watu wengi wanakosa elimu ya kujua ni Aina gani wa mbuzi anahitajika kunenepeshwa.

✓Changamoto ya usafirishaji ni hasa kupata magari kwa wakati na umbali pia ni changamoto sana hasa kwa mbuzi wa kunenepeshwa maana uchangia wawe stressed na kupoteza uzito unaotakiwa ili waweze kunenepeshwa.

~kigoma.
Hujatoa juu ya njia sahihi ya kunenepesha Mbuzi, aina ya vyakula na uwalishaje na nikwamuda gani, ili wafikie kilo ngapi kwa Mbuzi jike ua Dume
 
Habari kiongozi, aomba kujua idadi ya mbuzi wanaoweza kuingia kwenye eneo la heka tatu(mbuzi wa kunenepesha)
Inategemeana na Aina ya Banda na eneo la malisho, maana Kama utatumia zero grazing(kuwalishia ndani) mbuzi watapungua na kama utakuwa una waswaga mbuzi(kuwalishia nje) wataongezeka, kwa hiyo sema unafugia kwa njia gani ili uweze kuwanenepesha, ndo tupate jibu lako.

~kigoma.
 
Hujatoa juu ya njia sahihi ya kunenepesha Mbuzi, aina ya vyakula na uwalishaje na nikwamuda gani, ili wafikie kilo ngapi kwa Mbuzi jike ua Dume
✓Njia sahihi ya kunenepesha mbuzi.

Kwanza,kabisa njia sahihi ya kunenepesha mbuzi ni kwakutumia mfumo wa zero grazing(yaani kuwalishia kwa ndani) au kwakutumia hay(malisho ya majani ya kukauka) ambayo utunzwa kwa mda katika mifuko midogomidogo mithili ya mikate.

pili,ni kwakuwapatia chanjo ya CCCP walau Mara 1 Kika mwezi kwa miezi miitatu kwa mbuzi mtoto na Mara Mara moja kwa miezi mitatu baada ya kuachishwa kunyonya.

Kutokupigwa ili kumuepusha na stress maana upelekea kutokula vizuri na kupungua uzito.

Kutengenezewa mabanda yasiyona uwezo wakupitisha mvua/miale ya jua.

Banda kuwa mbali na vyanzo vya maji hasa yaliyo tuama.

Banda kuwa na sehemu ya kutokea taka na maji pindi litakapo hitajika kusafishwa.

✓Aina ya vyakula kwa sababu ya kunenepesha.

Kwanza,mbuzi wanahitajika kula walau 50% hadi 55% ya majani kuliko Aina yeyote ile.

Pili,20% ya protein

Tatu,20%concetrates

Nne, 5% Vitamin

Tano,5% madini

✓Namna ya kuwalishia mbuzi wa kunenepesha.

Hapa watakishwa kwa njia ya kawaida maana wanakuwa wamefungiwa katika zizi,lakini ukumbuke pia wanaweza kutolewa kwenda kulishwa.

Kama watalishwa wakiwa zizini,maana yake itahitajika mchanganyo maalumu wakulishwa kwa kila mbuzi.

Kitaalamu inashauliwa kila mbuzi alishwe 1/3 ya uzito wake(kwa mfano Kama mbuzi Ana 40kg inatakiwa alishwe 4kg*1/3 ya uzito wake.

✓Mda mahususi wa kulishwa mbuzi wa kunenepeshwa.

Kitaalamu inashauliwa mbuzi wakunenepeshwa alishwe kwa mda wa mwaka 1 hadi 1.5 ili aweze kukupatia faida,maana akizidisha hapo ataanza kupungua na Mwisho wa siku ukimuuza utamuiza kwa hasara maana ataanza kupoteza uzito.

N.B: lengo la kunenepesha mbuzi ni kwa ajili ya biashara ili aweze kutupatia faida na sivinginevyo.

~kigoma.
 
✓Yeah kwa hapa Tanzania minada mikubwa ipo Dar es salaam hasa pugu pamoja na vingunguti, lakini pia kwa dodoma kidogo hasa mbande-kongwa.

✓Changamoto zipo lakini inatokana na uhitaji wako Kama ni wakufuga tu au kunenepesha, maana Kuna sifa zinazohitajika kujua Kama mbuzi huyu ni wakunenepesha au laaah, na hapo ndo watu wengi wanakosa elimu ya kujua ni Aina gani wa mbuzi anahitajika kunenepeshwa.

✓Changamoto ya usafirishaji ni hasa kupata magari kwa wakati na umbali pia ni changamoto sana hasa kwa mbuzi wa kunenepeshwa maana uchangia wawe stressed na kupoteza uzito unaotakiwa ili waweze kunenepeshwa.

~kigoma.
Mkuu tueleze hizo sifa zinazopaswa kujua kama mbuzi anafaa kunenepeshw
 
Kitaalamu inashauliwa kila mbuzi alishwe 1/3 ya uzito wake(kwa mfano Kama mbuzi Ana 40kg inatakiwa alishwe 4kg*1/3 ya uzito wake.
Boss hapa kwa hesabu yako mbuzi anakula kilo 12
 
Back
Top Bottom