je wanyambo ni wakimbiz
Mkuu,ndio maana kuna kila sababu ya watu kuachana na ubaguzi wa kijinga kijinga.
Nasema hivyo kwa sababu moja: watu walio wengi wanajua ukanda huo wa wanyarwanda.Lakini hayo makabila mnayoyaongelea,ukienda Rwanda utaambiwa enzi za utawala wa kifalme maeneo hayo yalikuwa ya Rwanda,ndo maana wanafanana.Lakini swali la kujiuliza,wanyarwanda wana sura za kipekee? Ukienda Uganda,hao hao wataitwa wanyankole.Na huko utaambiwa hivo hivo. Sasa najiuliza,kwa nini badhi watambuliwe kama watanzania,wengine wafukuzwe? Na kama ungefika kambini ukaona wanavyohangaika,hawana ndugu hata mmoja,ndo ungegundua kwamba kuhukumu mtu kwa sura ni kosa kubwa.Kuna haja watu wakaweka utu mbele kwanza kuliko chuki binafsi.Mfano ukiulizwa wajaluo na wamasai kabila gani siyo watanzania utajibu lipi?
Kwa hiyo siamini kama ni wakimbizi kweli kwa sababu wamekuwepo toka enzi.Af kumbuka wanavozaliana na kuoana na wale mnaowaita watanzania halisi,kitatokea kitu gani?