Uliyevunjika moyo pitia hapa

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,007
1,893
usihofu, Mungu anaweza yote, anaweza kukutoa katika hali hiyo uliyonayo sasa, hadi wale wote waliokudharau wakashangaa. download document hii, kakae usome kwa makini na Mungu atakusaidia.
 
Attachments

  • YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU.pdf
    127.8 KB · Views: 159
unachotakiwa ni ku download na kuondoka na hiyo document, bure umepata, wape na wengine bure.
 
Moyo tulia mjini kuna vya watu vifungu vya Bible ulivyoweka vitawafaa wagalatia me Nina free mind
 
Moyo tulia mjini kuna vya watu vifungu vya Bible ulivyoweka vitawafaa wagalatia me Nina free mind
ok, lakini cha muhimu walau umevisoma, kuna siku yatakukuta hiyo free mind yako itafika mwisho utakuwa unatafuta solution nyingine, ndipo utafungua vitakusaidia tu. kiburi cha uzima ndicho kinawafanya watu hata wakata atheists, ila ukija kubanwa na mlango ukatoa macho kama mjusi, shetani amekusambaratisha kila engle, utamtafuta tu Mungu na utamuona. fahamu na kutambua kuwa uhai wako upo mikoni mwa Mungu, na unapaswa kumwamini na kumwabudu. thanks kwa kusoma, nimenawa mikono juu yako, na Mungu akusaidie.
 
Umenikuna hapa pembeni nipo na bible mpaka tarehe 2/1/2017 kama Mungu atanifikisha salama ndiyo maana sikauki hapa JF.
amini kwamba Mungu anaweza yote hata yale ambayo wanadamu wanasema hayawezekani. cha muhimu uamini toka moyoni na umpokee tu, vingine mwachie yeye ajitwalie utukufu.
 
amini kwamba Mungu anaweza yote hata yale ambayo wanadamu wanasema hayawezekani. cha muhimu uamini toka moyoni na umpokee tu, vingine mwachie yeye ajitwalie utukufu.
Mkuu mwezi wa 12 kwangu huwa ni kipindi cha kutafakari kazi nilizofanya kwa miezi 11, nashukuru sana kwa ujumbe mzuri.
 
Mungu alinisaidia mimi na mke wanguk, tuliteseka na kutukanwa mno kwasababu hatuna watoto, mke wangu ali endure mambo mengi sana sana, mwisho wa siku, Mungu amebadilisha historia, tunazaa mapacha mapacha, na mzigo mkubwa unaotusumbua sasaivi ni NAMNA YA KUZUIA MIMBA...hahahaha, zamani tulikuwa tunatafuta mimba kw amiaka karibia 5, Mungu akabadilisha historia uzao umekuwa mwingi mno kiasi kwamba muda wote tupo makini mke wangu asi conceive tena. hebu jaribu kufikiri, mwanzoni unahangaika kutafuta mimba, Mungu anabadilisha historia unaanza kuhangaika kuzuia mimba....Mungu wetu anaweza yote, hakuna jambo hata moja asilo liweza. kama alikausha maji ya bahari ya shamu, akatoa maji kwenye mwamba watu wakanywa, akadondosha mikate/mana ya mbinguni, alifanya maajabu mbele wa Wamisri, amefanya maajabu tangu enzi hadi leo bado anafanya, Mungu huyo huyo alibadilisha historia ya maisha yangu, pale unapoona kwa akili ya kibinadamu umeshindwa ndo umefika Mwisho, Mungu ndio huwa anaanzia hapo. Utukufu na heshima ni vyake yeye milele na milele.

kama kuna mtu anahangaika kutafuta watoto, NAKUHAKIKISHIA Mungu wetu hashindwi, wala usihangaike kwenda kwa waganga watakuwekea nyoka au mzimu tu utafikiri mtoto kumbe umebeba matatizo, Mungu wetu anao uwezo wote kukupa watoto. WATOTO NI ZAWADI TOKA KWA MUNGU, na yeye ndiye anatoa watoto. kuna mengi Mungu amebadilisha historia ya maisha yangu kabisa kabisa, na maisha yangu ni ushuhuda. Mungu yupoooooooooooooooooooo. Haleluya to the Lamb of God!

was reading Isaiah 53 recently, Mungu ameahidi kuwa kwa kupigwa kwake tumepona, na kwamba "for the sake of his only begotten, he will forgive our sins, and will save us. nenda kwa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo, mkumbushe Mungu kuwa akumbuke ile Damu ya Yesu iliyomwagika, hatuendi kwa Mungu kwasababu ya matendo yetu hata yangekuwa masafi vipi, tunapokelewa kwake just for the sake of what Jesus did on the cross, and that is the only thing God can be mindful of us. mlilie Mungu, plead the bood of Jesus, utaona matokeo ya wazi na utakuwa ushuhuda. may God bless you all!
 
kibao huwa kinageuka, when i thought everything was no more, when nothing else couldn't help, he just came down and lifted me up.
 
Moyo umekuvunjika mkuu, Pole sana!!
hiyo ilikuwa zamani mkuu, nilipitia magumu, lakini Mungu saw me through, sasaivi hadi nimesahau kuwa tatizo fulani lilikuwa part of my life kwasababu Bwana amenisahaulisha kabisa. nilikuwa nakosa watoto lakini sasaivi tukiwa na mke wangu tunafanya juu chini mimba ingine isiingie. ni kama ulikuwa na njaa lakini sasaivi unasaza....nilikuwa nimetupwa sina kitu sina heshima lakin Mungu amenisahaulisha hayo yote. sifa na utukufu kwake yeye aliye juu aishiye milele Amin! yeye hachelewi wala hawahi, ahadi zake ni za milele, anao uwezo kufungua mlango na hakuna afunguaye, anao uwezo kufunga na hakuna afunguaye, anao uwezo kufanya njia pasipo na njia, hakuna aliye kama yeye, na hatakuwepo mwingine!
 
Amina,
 
Amen....
 
Mungu huyu ninayemwabudu, kama alivyonikomboa mimi na kubadilisha historia ya maisha yangu, vivyo hivyo kuna siku atakuja kuikomboa Tanzania na kubadilisha kabisa historia ya nchi, wenye kiburi watakunjwa kama karatasi, uzuri wa Mungu wetu ni kwamba ana wivu, hashei utukufu, kama kuna mtu au watu wanajiona wao ni miungu watu hapa nchini, kuna siku watakunjwa kama karatasi. ninyi wenye kiburi hapa tz, kuna siku mtashushwa hadi kuzimu, ndio maana mnategemea ushawi na uganga badala ya kumtegemea Mungu, mnaonea wanyonge, mnajiona miungu watu, Mungu anawaona na kuna siku atawahukumu mbele za hawahawa watanzania.

Zaburi 18:27, God rescues the humble and puts down those who are proud. Mungu huwaokoa watu wanaoonewa, na macho ya kiburi atayadhili.

Mithali 11:2, Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu, bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Pride can put you to shame, it is wiser to be humble.

Isaya 66:2, Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu. The people I treasure most are humble, they depend only on me and tremble when I speak.those who are humble and obey his voice/word. May God bless you. Amin.
 
Back
Top Bottom