britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 15,636
- 30,004
- Thread starter
- #61
TumefananaUkweli ni kwamba uchaguzi wa 2015 haukuwa na mgombea urais mzuri; si Lowassa wala Magufuli. Kama ali yosema Mzee Ruksa kwamba wagombea wote ni wa CCM bali wao (UKAWA) wana CCM B na sisi CCM tuna CCM A.
Binafsi ilinilazimu kumpigia kura Magufuli sio kwasababu nilikuwa na matumaini angekuwa rais bora, bali kutokana na kukosa mgombea sahihi kwa upande wa UKAWA. Bali nilimchagua Magufuli kutokana na hasira za maamuzi ya msaliti Mbowe ya kubadili gia angani.
Tofauti na watu wengine, mimi nilimkataa Lowassa si kwasababu ya tuhuma ya ufisadi wa Richmond juu yake. Sikumkubali Lowassa kutokana na mambo yafuatayo.
1. Aliutamani na kuupania urais kiasi cha kuogofya.
2. Lowassa aliamini urais baada ya JK ni haki yake yeye peke yake.
3. Alianza kufanya harakati za "nguvu" (safari ya matumaini) za "kuufukuzia" urais mara tu baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu kana kwamba alitaka kuutumia urais kulipiza kisasi kwa wale waliopelekea ajiuzulu.
4. Aligeuza kashfa ya Richmond kuwa mtaji wa kujipatia huruma ya wananchi katika kuendeleza harakati za Safari ya Matumaini.
5.Aliuaminisha umma kuwa kujiuzulu kwake ni matokeo ya fitna dhidi yeke kutokana na uwaziri mkuu wake na si kutokana na kuhusika kwake na upendeleo wake kwa kampuni ya kitapeli ya Richmond katika zabuni za TANESCO.
6. Alifanya "mchezo" aonekane anapendwa na wananchi kwa kuandaa makundi mbali mbali ya watu wa "kumshawishi" ajaze fomu wakati mwenyewe alishapania awe rais.
7. Alifanya hira kuwakwamisha wagombea wenzie ndani ya chama wakose wazamini kwa "kuwatekaka" viongozi wa chama wa wilaya na mikoa na "kukomba" wazimini wengi zaidi ya idadi iliyotakiwa.
8. Alizunguka nchi nzima kuandikisha na kufanya mikutano mikubwa ya hadhara kwa ajili ya kuandikisha wazamini. Badala ya wazamini 30, aliandikisha zaidi ya makumi elfu katika mkoa mmoja.
9. Ziara zake za kutafuta wazamini ilikuwa ni zaidi ya kampeni na zilitumia magari mengi ya msafara kana kwamba tayari alishakuwa rais. Alitumia rasilimali nyingi kwa ajili na kufanya mkutano mkubwa wa hadhara kwa ajili ya kutangaza nia
10. Yote tisa, kumi alitumia walinzi wa chama kumpiga na kumdhalilisha mgombea mwenzie ndani ya chama Dr. Kalokola katika mkutano wake wa kutafuta wazamini Tanga mjini.
11. Alipohamia CHADEMA ni wazi ilionekana hakuwa na mapenzi ya dhati na chama hicho na UKAWA, bali alifanya uwamuzi huo ili apate jukwaa la kupata urais alioupania.
12. Hakuwa tayari kushindanishwa na wenzie kwa utaratibu uliokuwa umepangwa wa kumpata mgombea wa kuwakilisha UKAWA, bali aliendeleza matakwa yake kuwa urais baada ya JK ni haki yake yeye tu.
Mbinu, hira na njama zilizotumiwa na Lowassa kuuendea urais zilinifanya nimchukie Lowassa. Bali zilinifanya niwe na mashaka naye nikijiuliza kwanini alipania kwa gharama yoyote awe rais.