Uliyeamini mkioana wote wafanyakazi mna mshahara mtatoboa kimaisha tupe mrejesho

Wee ndo kidume sasa!

Sasa kuna wanaume wengine anakuomba kabisa mwanamke hela ...hapo ndo napochokaga asee!


Kama ukidume ndo kunyonywa kipesa, wakati ww mwanamke una ajira na uwezo wa kunisaidia kwenye majukumu ya kifamilia, huo ukidume SIUTAKI witnessj
 
Hao wote wanaotetea wameoa darasa la 7 B janamke likiamka asubuhi linapiga miyayo tu......aiseee kwangu nilishaipinga vikali.

Ngoja upate ajali uoneeee kama familia haijala nyasi na mkeo atagongwa kupitilizaaaaaa
La saba E ndo hawakufika elimu ya juu. Miaka ya majuzi hadi D walichaguliwa.

Mimi niamue tu kuwa muwazi kwa mume maana naweza mkabidhi kimshahara chote cha serikali na bado vibiashara vyangu vidogo vidogo ambavyo hawezi calculate exactly napata shingapi nikampiga cha juu.

Japo mkiamua kuwekana wazi mkachangia maendeleo huja kwa kasi sana.
 
La saba E ndo hawakufika elimu ya juu. Miaka ya majuzi hadi D walichaguliwa.

Mimi niamue tu kuwa muwazi kwa mume maana naweza mkabidhi kimshahara chote cha serikali na bado vibiashara vyangu vidogo vidogo ambavyo hawezi calculate exactly napata shingapi nikampiga cha juu.

Japo mkiamua kuwekana wazi mkachangia maendeleo huja kwa kasi sana.
Asante kwa hoja safi .....
 
Aaaaah wapi bora kuoa mwanamke jobless mwenye akili ya kufanya biashara hata ya kuuza karanga mnaweza kutoboa ila sio mwajiriwa mwenye salary yake utakufa kwa stress
Kuuza karanga.........(poor plan.....think beyond)
 
Na ndipo dharau mwanamke zinapoanza sasa! Si anaona na yy anagharamika?

Ukitaka mwanamke akuheshimu mtunze na usitake hata thumuni yake! Atakuogopa balaaa, bahati mbaya wanaume hawajui hii siri!
Mwanamke akitaka nimtunze 100% akae nyumbani alee watoto. Lkn kama na yeye anaenda kazini kutafuta kama mimi, lazima ajue na awe na hakika kuwa atachangia maisha ya nyumbani and that is not a choice but a must be done thing na kuniheshimu kama mume sio hiari kama hataki mlango wa kutoka uko wazi maana mm huwa sipigi wanwake

Mimi naishi kwa principles na mke wangu anajua. Mimi ni kichwa, ninazo amri na mamlaka kama kiongozi wa familia, hii ni misimamo yangu na nilimueleza kabla sijamuoa. Mwisho wa mwezi akipata na mimi nikipata tunaweka kwenye akaunti ya familia hela inafanya mambo ya familia sio mambo binafsi.

Kwangu mm ushirikiano baina yangu na mke wangu unafanya kazi na tunapiga hatua kwa kasi na tunanufaika wote wawili na watoto wetu. Namshukuru Mwenyezi MUNGU kunipa mke asie mbinafsi maana ametanguliza familia mbele na sio kutafuta utukufu wake binafsi. Ulichoeleza Witnessj ni ubinafsi wa kiwango cha juu kabisa maana hata mababu zetu hawakuishi hivyo utakavyo. Enzi za mababu zetu Wakina mama walitafuta matunda na mbogamboga lkn wakina baba walienda porini kuwinda na kuleta nyama nyumbani, wakati wa vita wakina mama walikaa kulea watoto na kutafuta chakula wakina baba walienda kupigana. Maisha siku zote ni mgawanyo wa majukumu baina ya baba na mama tangu enzi na enzi sio majukumu yote yanabebwa na mtu mmoja, huo ni ukupe.

Familia yenye amani ni familia ambayo baba na mama ni mwili mmoja kama mjuavyo viuongo vikuu vya mwili kamwe havitegeani ktk kuutunza mwili, figo haifanyi kazi kama moyo haufanyi kazi, moyo haufanyi kazi kama ubongo haufanyi kazi n.k n.k. Mkishakuwa miili tofauti hapo kunakuwa na masononeko ya moyoni kwa mmoja wenu au nyote hususani kipindi cha dhiki.
 
Ukitegemea hela ya mwanamke hasa wa kibongo kutoboa utapata shida sana,hao chao chao,chako chao
 
Kumchunguza sana napata wakati mgumu sababu kwa sasa yuko mbali nami. Yuko Morogoro nami niko Dar hatujaonana for a while now. Jana usiku tumekwaruzana kwa sms....akaja nitumia msg za usiku mwema late nights kwenye namba zangu 2 zote na sikumjibu. Kisha asububi amekuwa wa kwanza kunijulia hali. Wonders shall never end
We ndo unachunguzwa sasa mkuu
 
Tangu nikiwa mdogo sikuamini katika kuoa mfanyakazi wala mfanyabiashara.
Labda hayo yote yatokee nikiwa nimeshamuoa.

I'm strongly enough kufa hata kupona kwa ajili ya familia yangu mwenyewe.

Wanaume tumeumbwa mateso na kuhangaika ili hawa viumbe tuloumbiwa waishi salama.
Na heshima yako ka mume utaiona
 
Back
Top Bottom