Uliwezaje kudumu kwenye mahusiano na mpenzi asietaka romance, kiss wala sex?

snayper

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
302
217
Habari za asubuh wakuu,

Mimi nina mpenzi ambae tupo kwenye mahusiano kama miezi mitano sasa, wakati tunaanza mahusiano, mapenzi yalikuwa moto sana kiasi kwamba nikaona ni serious relationship, tulikuwa tunakutana mara moja moja weekend usiku tunalala pamoja japo hatukuwahi fanya sex coz alikataa kufanya sex kwa kipindi hiki, pia alisema yeye hajawahi fanya sex ni bikira, na ilikuwa nikimshawishi kufanya sex lazima tugombane, nilimuelewa sikutaka kumbaka lakini mambo mengine kama romance na kiss tulikuwa tunafanya.

Tatizo limekuja hivi karibuni, anasema kufanya romance, kissing ameona anamkosea Mungu yaani ni dhambi, hivyo hataki tena tukiss, romanse, wala sex mpaka tutakapooana, yaani tuwe kama kaka na dada.

Hili jambo limekuwa mitihani kweli ukizingatia nampenda na sipendi nimsaliti. Kwa waliowahi kudate au kukutana na changamoto kama hii mliwezaje kudumu katika mahusiano haya? Mlifanyaje kutatua changamoto hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom