Uliwahi kuwa mwanafunzi wa Bunge Primary School,Dar es salaam? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uliwahi kuwa mwanafunzi wa Bunge Primary School,Dar es salaam?

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mpogoro, Oct 17, 2009.

 1. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Uliwahi kuwa mwanafunzi wa Bunge Primary School,Dar es salaam?Je,unaweza ku-spare muda kujaribu kufanya kitu kwa shule yetu ambayo kwa sasa imekabiliwa na matatizo kadha wa kadha....

  Nilibahatika kutembelea shule hivi karibuni na kuongea na Mwalimu Mkuu.

  Changamoto za shule kwa sasa ni kama ifuatvyo:

  1. Uchakavu wa mfumo wa maji safi na taka:

  Kwa kweli hi ndio changamoto kubwa kwa shule kwa hivi sasa kwani
  mabomba yanavuja na hivyo kusababisha rangi kuchafuka na wakati
  mwingine maji kuingia kwenye ofisi mbalimbali…hili linathibitika hata
  kwenye ofisi ya Mwalimu Mkuu ambamo kuta zimepata “ramani” na ukungu.

  Kwa upande wa maji taka…mfumo mzima wa DAWASCO umekuwa na gharama kubwa sana ambazo shule haiwezi kuzimudu kwa sasa.Kuna wakati serikali ilikuwa inalipa bili kwa DAWASCO lakini kwa sasa imeshindwa na hivyo kwa sasa shule inadaiwa kwenye milioni mbili na kitu baada ya harambee iliyohusisha wazazi kufanikisha kulipa shilingi milioni tatu na kitu.

  Matatizo ya mifumo hii imekuwa na athari kubwa sana hasa kwenye upande
  wa vyoo.Licha ya kuwa shule imefanikiwa kuchimba kisima chake kirefu
  lakini mfumo wa maji taka umekuwa ni tatizo sana kwani kwa sasa shule
  ina harufu kali sana ya choo…yaani kwa kweli hata unapokuwa ofisini
  kwa Mwalimu Mkuu hali inakuwa si shwari…ukipata nafasi tembelea uone
  mwenyewe!

  Suluhisho: Baada ya kuongea na Mwalimu Mkuu tumeona kuwa suluhisho la
  kudumu hasa la mfumo wa maji taka ni kuchimba mashimo ya vyoo pale
  shule maana bado kuna eneo la kutosha tu na hivyo tutaondokana na
  tatizo la kutegemea mfumo wa DAWASCO ambao si tu unagharimu shule na
  wazazi kiasi kikubwa kwa kulipa bili za kila mwezi lakini pia hauko
  safi na hivyo umekuwa kero.

  Kwa sasa shule bado inategemea vyoo saba ambavyo ni matundu 2 ya shimo kwa wavulana na matundu 5 ya vyoo kwa wasichana.Idadi ya wanafunzi pia imekuwa kubwa kufukia jumla ya wanafunzi 1450 kwa sasa…..ikumbukwe hii indo shule pekee kwa kata ya Kivukoni.

  2. Umeme:
  Shule ya Bunge imekuwepo toka 1957.Mfumo mzima wa umeme yaani wiring
  imechoka kabisa.Shule imechukua jukumu la kufanya wiring ya muda
  lakini tunahitaji suluhisho la kudumu ambalo ni kufanya wiring upya.

  3. Rangi:
  Shule inaitaji kupakwa rangi…licha ya kwamba hili ni jambo la
  msingi.Upakaji rangi bila kufanya ukarabati wa mfumo wa maji safi na
  taka unaosababisha kuvuja kwa shule ni sawa na bure hivyo suala la
  marekebisho ya mifumo ya maji ni lazima yaanze na upakaji rangi
  kufuatia.

  Kwa ujumla kuna matatizo mengi hayo ndo kwa haraka haraka tuliweza
  kuyabaini kwa ushirikiano wa Mwalimu Mkuu.Nafikiri sisi kama wadau
  tunajukumu la kuhakikisha tunafanya kitu kwa ajili ya shule yetu.I
  suppose hapa kuna ma-engineers na mafundi ambao wangeweza kutusaidia
  katika assessment ya hali ya shule na hivyo kuweza pia kutusaidia
  kupata gharama halisi za kuweza kufanya ukarabati wa shule yetu.

  Siamini kama tuna nafasi ya kufanya haya yote kwa pamoja na mara moja
  ila tukijipanga tunaweza kufanya mobilization ya resources na
  ku-identify suala ambalo tunaweza kuanza nalo.Naomba tutumie ofisi
  zetu yaani makampuni ambayo tunafanya kazi nayo kuaona kama wanaweza
  ku-support initiative ya kubadili taswira ya shule.Tukijipanga
  yote yanawezekana!

  Kama huko interested,tafadhali ni PM.Napokea ushauri kila kitu...
   

  Attached Files:

 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hizi shule inabidi tuanze utaratibu wa PPP.......i.e ziwe za kulipia, hii mmabo ya kutegemea serikali ambayo haioni umuhimu wa elimu (kutokana na kupunguza bajeti ya wizara kila mwaka) si ya kuitegemea.

  Hii shule ilikuwa ni moja kati ya shule nzuri sana nyakati hizo........

  .....mnaweza kujikusanya ili kutatua matatizo yaliyopo.....tatizo bado litakuwepo.......i.e. maintenance (neno ambalo halipo kwenye dictionary zetu).......a sustainable solution is needed..........

  Pendekezo:
  Shule iendeshwe kwa mfumo wa kuchangia.......iwe chini ya baraza la wadhamini kwa kipindi likishirikiana na serikali..........i.e.....PPP
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  T.I.D,........RENATUS NJOHOLE........PIUS IRERI(jkt ruvu).......CLEOPHAS WAANE(hon)...MARIAM IDRISA RASHID.......NOELA MWAILOLO......MUSA KAJIRU......!
  JUSTto mention the few......!
  yes we can.... lets join forceeeeeeeeeees.......!
   
 4. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,042
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  hao ni makinda(bongo flava) wa bunge p/s.....wazee wa kazi (bakulutu)hujawataja hapo.
   
 5. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri ungemsaidia kuwataja hao Bakulutu/Wazee wa kazi basi
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hapo uwanjani bado panakuwa swiming pool wakati wa mvua? Tehe tehe
   
 7. MamaParoko

  MamaParoko JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 465
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du! Inasikitisha sana, picha hizo zimeleta kumbukumbu nyingi kwangu, kama mmoja wapo ya waliosoma bunge.
   
 8. GP

  GP JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  sasa si asavali yenu nyie wa bunge mna vyoo vya kuflashi, mna kaumeme kakuzugia, sie tuliosoma madongokuinamamadongokuporomaka primary school tusaidiwejee??
   
 9. a

  asger New Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Dec 17, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Man i am in pia dah yani shule yetu ndio imekuwa hivyo this was the best school man naitwa Asger nimemaliza pamoja na nyie mnanikumbuka??? nilikuwa group moja na luhinda eric sharon lupi mayowela raymond suli chillipweli zei arafa mkindi asma mwinyi 7B
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2016
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Asgeral M Raza
   
 11. s

  shaurimbaya JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2016
  Joined: Oct 3, 2013
  Messages: 1,950
  Likes Received: 1,643
  Trophy Points: 280
  bunge washkaji zetu forodhani primary....... sisi shule yetu wameichukua ma sister imependeza sana
   
Loading...