OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 44,908
- 88,453
Wakati fulani mwaka juzi nikawa na safari ya kikazi Musoma. Sikuwahi kufika Musoma kabla kwa hiyo sikuwa mwenyeji wa maeneo nilitegemea boda.
Nikashuka stendi nikamwambia boda nipeleke lodge nzuri nzuri. Baadaye nikaona nisichemke ngoja nimshirikishe mwenyeji wangu. Mwenyeji wangu sikuwa nafahamiana naye wala kuonana. Kwa vile alijua ile kazi ni ya kibosi sana akaamini natakiwa kulala hotel yenye hadhi. Akamwelekeza boda pa kunipeleka.
Kufika daaah, nakuta hotel kali ghorofa kadhaa. Nje napokelewa na mabendera ya nchi mbalimbali.
Nikamwambia bodaboda mmenileta cha kike. Muhudumu mrembo kabisa akaja kunipokea nikiwa mchafu vumbi na kabegi mgongoni kama nimetoka kuchimba mitaro.
Nikamwambia boda usiondoke lolote linaweza kutokea. Tayari muhudumu akawa amenihukumu kwamba sina uwezo wa kulala pale. Akaniambia lakini kaka hapa chumba ni kuanzia elfu 50!
Nikamwambia mimi sijauliza bei nimeuliza chumba. Kufika reception kila mtu anaonyesha wasiwasi huyu mteja kapotea. Basi nikamwambia nataka chumba cha juu.
Akanijibu tuangalie tu vya chini kule juu ni kuanzia elfu 70. Nikaona aaaahhhh japo nilitaka chumba cha 20 ila hapa inabidi niweke heshima tu bila kujali chochote.
Nikachukue chumba cha 70. Nikarudi mapokezi kwenye watu wengi walionitilia mashaka. Nikaanza kulipa bills kwa sauti.
Nikawaambia sikilizeni, ninakaa siku 2 nitalipa 140,000 yote, halafu dada chukua buku 10, mlipe boda buku ya nauli na buku 4 ya kunisubiri. Halafu elfu 5 baki nayo umenipokea vizuri nimepenta, lakini mwambie boda naomba namba yake.
Ndugu msomaji yote hayo niliyafanya kulinda heshima dhidi ya wajinga wachache ambao walinihukumu kwa mwonekano.
Lakini pia kujitabiria mambo makubwa mbeleni kwamba ipo siku nitakaa meza moja na wakuu, nitakula na wakuu na nitalala lodge moja na wakuu.
Je, ulishawahi kufanya jeuri ya pesa hata kama huna kingi, ili kulinda heshima yako au kujitabiria ukuu?!!