Ulivyokuwa mdogo ulikuwa unataka kuwa nani?

Ladder 49

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
7,416
18,856
Wakuu habari zetu?

Najua kila mtu humu alikuwa ana ndoto zake alipo kuwa mtoto ,anataka kuwa mtu fulani kulingana kwamba alivyomwona au alisimuliwa story akapenda.

Mimi nilivyokuwa mdogo nilikuwa nataka sana kuwa pilot au mfanyakazi wa bank nilkuwa nawaona jamaa wako smart sana leo nimeishia nilipokuwapo sio pilot wala accountant.maisha hayana fomula

Japo hatufahamiana kwa majina yetu halisi humu jf lakini sio mbaya tukajua Ulivyokuwa mdogo ulikuwa unataka kuwa nani?

Nawasilisha.
 
Nilikuwa natamani kuwa rais, lkn baada ya kusikia urais una frustration zake, nipo nauza unga wa mhogo tu kwa sasa.
e9523386ace009e8c4e6cc02e52d6609.jpg
 
Nakumbuka nilisoma shule ya kata na by then nilichotaman sana ni kuwa injinia, hili wazo nililipata baada ya kuwa naenda shule nawakuta watu wanajenga bara bara yan nilikua nawaangalia tu na nilikua nataman kweli!!!

Basi harakati zikaendelea,form one, two, three kwa mbinde,form 4 ikafika huku tukiwa hatuna walimu wa maths na physics maana walienda masomoni tokea tukiwa form2!!

Daah kwenye ile shule tuli PASS tulikua watatu tu wengine waliangukia 4 na zero....

Kutokana na ufaulu wangu nikaenda private hgl (nliiomba hii kombi ili nichagulie maana kwa sayansi wasingekubali) ...nilitaman sana kuwa injinia na huwezi kuwa injinia wa kusoma arts.

Baada ya kuanza form5 nikawa siingii arts muda wote niko zangu sayansi nakomaa na pure... Watu walikua wananishangaa... Wengine wakasema nimechanganyikiwa... Maana waljua niko arts!!

Kiukweli sikupenda arts na nilijaribu mara nyingi kuomba nibadilishiwe master alikataa, siku moja kama zali mwalim wa academics akanikubalia infact hakuamin kama unaweza ama arts kwenda sayansi... Walizoea watu kutoka sayans kwenda arts...

Basi mimi huyoo nikaanza rasmi safari ya sayansi...nilifurah baada kuona ndoto yangu itatimia. Kwa kifupi nilikua nachezea tano bora na mpaka naingia form6 nilishika namba moja, maticha hawakuamin....

Long story short, nilimaliza na div one na kupangiwa chuo na sasa mimi ni injinia...

Ushauri: kufanya kitu upendacho ni hatua ya kwanza ya mafanikio...
 
Back
Top Bottom