Ulivyoagiza gari yako spare key uliikuta sehemu gani?

trplmike

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
701
775
Ulivyoagiza gari yako ufunguo wa akiba..uliukuta sehemu gani?

Njooni tupeane maujanja. Kuna gari moja niliiagiza ufunguo wa spare niliukuta ndani ya Manual book ya gari. Kwenye gari nyingine baada ya kutafuta sana.. nilikuja kuukuta kwenye hivi vidroo vidogo dogo ambavyo vipi kwenye dashboard.

Kuna gari nyingine nilikuta ile antenna imefunguliwa haipo.. nikajua wamepita nayo wahuni, siku nimekwenda kuosha gari nikaikuta chini ya siti ya dereva.

Ila kuna gari moja Suzuki Grand Vitara mpaka leo sijawahi kuona spare key.

Wewe ya kwako uliikuta sehemu gani? Au zilikuwa zote sehemu moja?
 
Wewr jamaa unanunuaga magari ya wizi. Nachojua mm unapokabidhiwa gari iwe yard au bandarini na wakala funguo zote mbili zinakuwa attached pamoja.
 
Back
Top Bottom