Ulitumia njia gani kurudi mwili wako wa kawaida baada ya kujifungua?

Pisi kali

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,215
2,418
Nina miezi kadhaa baada ya kujifungua ni mtoto wangu wa kwanza, (RIP MY ANGEL) sasa tangu nijifungue nazidi kunenepa tu sipungui

Sijanywa masupu wala mitori lakini unene umegoma kuniacha nimefanya mazoezi naona nachoka tu bure nimegoogle aina ya milo kwaajili ya kupungua ila bado

Huu unene naona kama mume wangu hapendi japo ananiambia pungua kidogo tu.

Nina 98kgs nataka atleast 70 or 66kgs sio mbaya.

Kuna kampuni inaitwa TANZANITE kama sijakosea nasikia wanadawa and some treatments za kupunguza mwili, tumbo, stretch marks, kuna aliyewahi kupata matibabu hapo labda? Maana naogopa nisije nikakonda zaidi ama kunenepa zaidi
 
Badili mfumo wa chakula , achana au punguza mavyakula ya wanga na sukari.

Kula mboga za majani na wanga kidogo ili upate nguvu za kufanya kazi. Ila usiku acha kabisa kula wali , machapati na ugali. Acha kabisa. Usiku Bora ule hata yai na mboga za majani.

Hakuna shortcut ya kupungua utatapeliwa Hadi ukome.

ACHANA NA MAVYAKULA YA WANGA utakuja kunishukuru.

Kumbuka zoezi la kupungua halijawahi kuwa rahisi hata kidogo. Ni zoezi gumu mno tena Sana. Jiwekee Target ya kuona matokeo hata baada yaiezi 6 Hadi 12. Sio unataka matokeo ya kupungua uzito ndani ya wiki. Badili life style yako ya ulaji.
 
Ukitaka kupungua haraka na bila athari yoyote ya kiafya,tumia kanuni ifuatayo.

14 days fanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni(mazoezi mazuri zaidi ni kutembea umbali flani),kisha 14 days funga(jizuie na kula na kunywa chochote) kwa at least 12 hours per day,kuanzia alfajiri hadi jioni ndio unakula.

Hakikisha unapokula usishibe sana,

It works.
 
Badili mfumo wa chakula , achana au punguza mavyakula ya wanga na sukari...

Asante
Ila Kwenye sukari hapo mimi ni mpenzi sana wa soda tena pepsi kila siku lazima ninywe moja (hapo ndio nimepunguza)

Kwenye kula mimi sio mpenzi sana wa kula kula nina vitu flani flani hupendelea haswa

Nitajitahidi nifate ushauri wako
 
Ukitaka kupungua haraka na bila athari yoyote ya kiafya,tumia kanuni ifuatayo.

14 days fanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni(mazoezi mazuri zaidi ni kutembea umbali flani),kisha 14 days funga(jizuie na kula na kunywa chochote) kwa at least 12 hours per day,kuanzia alfajiri hadi jioni ndio unakula.

Hakikisha unapokula usishibe sana,

It works.

Kufunga naweza ila kutembea mmh nitajidanganya

Kula inaweza ipite siku nzima sijala ila nakunywa soda tu

Tatizo la mazoezi ukitoka hapo unasikia njaa balaa lakini nitaanza december
 
Pole sana kwa kupoteza mtoto.

-Dawa ya kupungua ni mazoezi tu.....Na pia flow ya mshiko ikikata moja haikai wala mbili ,silencer gari inakata moto lazima utakaa kama namba moja.
 
Asante
Ila Kwenye sukari hapo mimi ni mpenzi sana wa soda tena pepsi kila siku lazima ninywe moja (hapo ndio nimepunguza)

Kwenye kula mimi sio mpenzi sana wa kula kula nina vitu flani flani hupendelea haswa

Nitajitahidi nifate ushauri wako
Achana na soda kabisa zinanenepesha haraka Sana hzo, hafu Anza mazoezi ya kutembea na kukimbia
 
Dawa ya kupungua Ni chakula...Angalia chakula chako...utafanya mazoezi hata siku nzima..ila ukibugia min
wali na michapati na masoda KWA wingi..hutapungua hata kilo.

DIET 80% MAZOEZI 20%
 
Achana na hayo masukari ya soda... Pepsi ina vijiko 8 vya sukari ... Unapokunywa chupa moja ya Pepsi unakuwa umemeza vijiko 8 vya sukari ... End product ya sukari ni kuzalisha mafuta matokeo Yake ni ubonge... Sasa jiulize unakunywa vijiko vingapi kwa wiki na mwezi.
 
Achana na soda kabisa zinanenepesha haraka Sana hzo, hafu Anza mazoezi ya kutembea na kukimbia

Sijui ni mazoea napenda sana pepsi tena iwe ya baridiiii nimejitahidi ndio sikuhizi nakunywa moja per day
 
Dawa ya kupungua Ni chakula...Angalia chakula chako...utafanya mazoezi hata siku nzima..ila ukibugia min
wali na michapati na masoda KWA wingi..hutapungua hata kilo.

DIET 80% MAZOEZI 20%

Chakula sili sana kwa kweli naweza nikala asubuhi tu au mara mbili kwa siku tatizo lipo kwenye soda

Mazoezi mimi ni mvivu kusema laukweli
 
Back
Top Bottom