Ulishawahi kuumizwa na watu uliowasadia katika maisha?

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,240
2,000
Haya maisha acha tu. Kuna wakati unaweza kukata tamaa kabisa. Ukajisema moyoni labda niache kuwa mtu mwema. Niishi maisha yangu ya ubinafsi, choyo, fitina na roho mbaya. Kisha ukajisemea tena "sitaki marafiki nataka niwe peke yangu".

Wakati huo huo sauti nyingine laini na ya chini kabisa inaanza kukunong'oneza "hapana hayo siyo maisha, huwezi kuishi peke yako, zaidi sana wewe ni mtu mwema endelea tu kutenda wema"

Ukweli ni kwamba, tumeumizwa sana na watu ambao tuliwasadia hapo awali. Walikuja kwetu wakiwa wapole na wanyenyekevu, leo wamevimba, hata salamu hawatupi tena. Wamepata walichokuwa wanakitafuta, kiburi kimemeza nafsi zao. Yote heri tumemwachia Mungu.

Je, umewahi kuumizwa na watu uliowasadia? Hauko peke yako jipe moyo, endelea kutenda wema.
 

maishapopote

JF-Expert Member
May 28, 2009
2,601
2,000
kuna jamaa nilimsaidia sana nikamtoa jela,nikamp a kazi...nikampa hela alichokuja kunifanyia ni MUNGU Anajua nimemfuta kwenye life yangu...Duniani na Mbinguni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom