Ulishawahi kusingiziwa jambo la uongo katika maisha yako?

mhuri25

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
1,876
2,000
Kusingiziwa kusikie tu japo wakati mwingine unadharirika sana!!Ipo hivi Iumaa ya wiki iliyopita Demu wangu ambae ni mfanyakazi mwenzangu pia aliniomba sana nikalale kwake maana Rafiki ake ambae wamesoma wote chuo kimoja na kwasasa tupo nae kituo kimoja ameondoka kaenda kwa jamaa ake wilaya moja inayounda jina la mkoa mpya Huko Kanda ya ziwa!!

Basi bwana kweli nikaenda maana kusema kweli kimepita kipindi sijala mzigo kutokana kuishi na huyo Rafiki ake( huyu manzi hapendi kabisa nimle getto kwangu au Guest/lodge yeye anataka ukamale kwake tu!!


Basi muda usiku kucha nimelala nae ile asubuhi yeye alikuwa anaenda kazini mie nilikuwa OFF, akaniacha nimelala mida ya saa1 hv mkojo ukawa umenibana sana na kwa bahati mbaya uwanj Kuna mafundi walikuwa wanarekebisha nikatoka nje nikamkuta dogo mmoja nae wamepanga alipopanga demu wangu, nikimuuliza dogo uwanj wapi nataka nikakojoe dogo akaniambia zunguka upande wapili Kuna choo Cha jirani huwa tunatumia pia kweli nikazama si nikakuta Kuna mzigo hv umeshushwa Kama muda kidogo Mimi na jinsi nilivyobana nikakojolea kwa juu juu nahakukuwa hata na Maji nikasepa zangu!!


Daah nimerudi tu getto nak kulala hata dakika 3 hazijapita akaja maza akaanza kugonga ile nafungua tu nasikia baba baba Heshima ni kitu Cha bure nausijitetee kabisa chukua maji ukamwagie tabia gani hii, mama anaongea kwa nguvu haswa Hadi akatoka mama mmoja mpangaji mwenzie akaanza kumueleza kwa kilugha asee nilifadhaika Sana Sana tu kinyonge nikaenda kumwagia!!

Ila kusema ukweli yule Mama nimemkariri vizuri najua atakuja tu kazini kwangu na sitalaza damu nimepanga nitamwambia Mama si ulinidharirisha kiasi kile siku ile asubuhi Sasa leo utajua haujui huwa Sina roho yakisasi kabisa ila kwa hili utanisamehe kabisa wewe Mama!!!
 

Tempus Fugit

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
574
1,000
Kuna mambo kwenye maisha haya ukisingiziwa kamwe hauwezi kujitetea ukaeleweka. Maana unakuta aliyekusingizia ameshasambaza maneno na yameaminiwa kuliko unavyoweza kujitetea.

Niliwahi kukutana na hii moment...inaleta uchungu na huzuni..maana unajitahidi kuelezea ukweli watu wanakuchukulia kama vile unatafuta namna ya kuuficha ukweli.

Kubwa ni kumuachia Mungu tu...usilipe kisasi.
 

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
2,473
2,000
Old skool Kuna Wana Kama 5 Hivi walisingiziwa hua wanakojoa kwenye jengo la jipya la maabara linalojengwa,wakapokea kichapo Ili wataje na wahusika wengine si wakaanza kuropoka tu na kutaja mtu yeyote mwisowe tukajikuta wadau wote wahuni wa class Kama 100 Hivi tupo Kwa Warumi weusi tunakula kichapo heavy na kusulubishwa, push up za kufa mtu
Tukapewa adhabu ya kulima ekari 2 za shamba la shule,kiupande wangu niliumia Sana ila Wana tuliwasamehe tu sababu walikua hawana namna maana wasingetutaja kichapo kingeendelea Kwa masaa kadhaa!

Cha kusikitisha zaidi wakati tunapelekwa kwenye jengo lile tukaona Ile staili ya ukojoaji ni ya kike kabisa yaani wote najua mnajua mwanamke akikojoa kwenye mchanga Kuna tujishimo hua tunachijichimba na alama za miguu,japo tulikula kichapo tukaishia kucheka na kuanza jokes kwamba utakuta demu wa selemani na abdala ndio wamefanya vile sisi na kina abdala ndio tunabeba adhabu zao!
😁😁😁😁😁
 

Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,956
2,000
Walinisingizia nimeiba hela yao. Jioni wakakumbuka walipoiweka baada ya kulewa na wakaikuta yote salama. Wakaona aibu tu Nikahama na Mazoea sikutaka nao tena.

Leo wananihitaji (msaada wangu) nawasaidia remotely. Wananiuliza mbona hauji nyumbani, Nawajibu nishakuwa mtu mzima sana, sasa hivi kusingiziwa wizi hainidhalilishi mimi pekee bali na familia yangu.
 

Amehlo

JF-Expert Member
May 8, 2019
2,887
2,000
Walinisingizia nimeiba hela yao. Jioni wakakumbuka walipoiweka baada ya kulewa na wakaikuta yote salama. Wakaona aibu tu Nikahama na Mazoea sikutaka nao tena.

Leo wananihitaji (msaada wangu) nawasaidia remotely. Wananiuliza mbona hauji nyumbani, Nawajibu nishakuwa mtu mzima sana, sasa hivi kusingiziwa wizi hainidhalilishi mimi pekee bali na familia yangu.

Itakua inawaumiza sana hiyo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom