Ulishawahi kuona mwizi aking'ang'ania polisi ampeleke kituoni!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,800
34,189
Mwizi huyo.jpg

Kama alivyokutwa huyu mwizi kariakoo huku raia wakimuomba afande awaachie mwizi huyo angalau dakika 5 wamlainishe mtuhumiwa apate kwenda vizuri

polisi,Lakini kilisikika kilio kutoka kwa mwizi huyo aliyejitambulisha kwa jina la alfani akisema” kaka mkubwa afande twende wote sentro kaka watanimaliza hawa

baba yangu afande’’na raia nao walizidi kumuomba afande yule amuachie wizi huyo,kwa bahati nzuri lilikuja gari la polisi na kuondoka nae..
 
Wezi wakikuibia ndio unaona shida yako kama hawajawahi kukuibia utawaonea huruma tu
 
Juzi nilikuwa mahali jamaa akamchoma mwenzake kisu..Jamaa aliechomwa kisu akakimbizwa hospital kufika hospital madokta wakasema ameshafariki...Umati wa watu ukarudi kumtafuta yule aliemchoma ili wamuue na Polisi nao wakawa wameshafika maeneo ya ugomvi kuangalia ni nin kilichotokea walikuwa na PT...Muuaji alivyoona polisi akjificha ndani ya hiyo nyumba lakini alivyosikia umati wa wale watu wakisema lazima tumuue aliponyoka akakimbilia kwenye PT mbele pale kwa dereva...Akamwambia derva ni mimi nimeua hawa wataniua..Dereva akatoka kwa kasi akiwa amewaacha wale askri wengine na raia wakawa wamesanuka PT ilikimbizwa na toyo kama elfu na raia waenda kwa miguu kama 1000 ilikuwa ni kazi sana kumsitiri yule bwana..Hadi mabomu yalipigwa kutawanya watu..
 
Wamuache tu maana taratibu za kisheria zinafahamika, sio kujichukulia hatua mikononi
 
engi wanajua wakifika polisi watahonga wataachiwa lakini kwenye wananchi wenye hasira hukumu ni palepale ila si vizuri kuchukua sheria mkononi maana watu wengi wasio na hatia wamepoteza maisha yao
 
Wamuache tu maana taratibu za kisheria zinafahamika, sio kujichukulia hatua mikononi
Hivi mwizi nae si anajichukulia sheria mkononi? Au huwa wanaiba kisheria ila wananchi ndo wanajichukulia sheria mkononi? Mimi naona anaeanza kujichukulia sheria mkononi ni mwizi na wananchi wanakamilisha alichoanzisha mwizi.
 
Issue ni kwamba kuna wengine huwa wanasingiziwa na kuuawa bila kuwa na makosa
 
Hivi mwizi nae si anajichukulia sheria mkononi? Au huwa wanaiba kisheria ila wananchi ndo wanajichukulia sheria mkononi? Mimi naona anaeanza kujichukulia sheria mkononi ni mwizi na wananchi wanakamilisha alichoanzisha mwizi.

Kosa moja halihalalishi jingine.
 
polisi wana roho nzuri sana. Usishangae ukiambiwa huyo mwizi ni member wa humu JF ambae mara nyingi anasema hawapendi polisi, leo kawekwa mtu kati anamuita afande kaka mara baba twende wote sentro.
 
Unafikiri ni mchezo kuchungulia Kifo? Utatumia mbinu zozote kukwepa. ....

Lakini wananchi walikuwa sawa kabisa.......waliomba wamlainishe kidogo ili aende polisi akiwa laini.......hapo kulikuwa na ubaya gani......?.....mi naona wananchi wamenyimwa haki yao ya kutumia lubricant.........
 
He he he he he. Acha utani na wananchi wenye hasira. ...Bora ukutane na mtumbua majipu. ...

Hiyo lubricant ingemlainisha mpaka kuzikwa. ...
 
Back
Top Bottom