Ulishawahi kukutana na nyakati hizi za kuudhi?

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
51,991
69,381
Habari wana JF,

Naamini kila mmoja wetu ameshapitia nyakati mbalimbali za kuudhi ambazo hatozisahau kwa namna moja au nyingine.

Je, umeshawahi kupitia hizi nyakati au nyinginezo?( Ongezea....)

1.Uko kwenye daladala, mara ghafla linapita gari la takataka, harufu inaingia ndani, ukifunga vioo inabaki ndani, ukifungua vioo inazidi kuingia! Mbaya zaidi mko kwenye foleni.

2.Unaangalia simu yako mara ghafla inaingia meseji ya kuchekesha, unacheka kwa sauti kubwa, unagundua kila mtu alikuwa kimya na sasa wote wanakuangalia wewe huku wanatikisa vichwa!

3.Uko hotelini au shopping, mara anatokea mtu anakuuliza bei ya vitu akidhani wewe ni muhudumu!

4.Umekutana na mtu hujaonana nae mda mrefu, unataka kumkumbatia halafu yeye anakupa mkono.

5.Unataka kumsimulia mtu habari unayohisi ni ya kuchekesha, unamaliza kusimulia alafu yeye hajacheka akidhani inaendelea!

6.Unamjibu mtu maswali yote, kumbe hakuulizi wewe anaongea na simu!

7.Unampungia mtu mkono mbele za watu, alafu yeye hajibu chochote kumbe umemfananisha.

8. Unahangaika Kusukuma mlango ili ufunguke kwa sekunde kadhaa baadae unagundua kumbe mlango umeandikwa "pull" yaani Vuta!

9.Unasimulia Kitu katikati ya watu, mara mate yanaruka na kumuangukia mtu wa jirani, na kila mtu ameona.

10. Unasikiliza muziki masikioni (earphones), unagundua watu wote wanakuangalia wewe kumbe unaimba kwa sauti ya juu mbaya zaidi unaukosea wimbo.

11. Upo benki mtu anakuja kukuuliza eti samahani hili ni tawi gani au leo ni tarehe ngapi vile?
 
Hii ya gari ya takataka hapana chedhea aisee. Ni habari nyingine kabisaaaa. Nakereka hatari.

Unaweka earphone halafu unaanza kujamba ukiamini unatoa kitu cha yusuph.sasa watu wanakuangalia halafu wanacheka kwa nguvu sana mpaka unauliza vepee,unaambiwa umelishusha mother of bomb.
 
Kwenye mkusanyiko wa Watu, Mtu anajamba ule Ushuzi wa kimyakimya ule Ushuzi ambao unanuka.

Anawaachieni Hewa chafu nyie mnabaki mnaziba Pua zenu au kukunja Nyuso ilhali mkiwa hamfahamu ni nani alieJamba
 
Uko kwenye daladala, mara ghafla linapita gari la takataka, harufu inaingia ndani, ukifunga vioo inabaki ndani, ukifungua vioo inazidi kuingia! Mbaya zaidi mko kwenye foleni.


Umenikumbusha ilitokea siku moja pale Magomeni Mikumi, tupo kwenye foleni kukaribia Traveltime hotel nyonyanyonya ikachomoka kizibo maji taka yakaanza kutiririka abiria wengine tuliamua kushuka kwenye daladala tumalizie safari kwa miguu kwa kupitia vichochoroni maana ile ilikuwa ni hatari unaweza kufa kwa kukosa hewa safi

Sijui kwanini wanayatembeza mchana hayo magari!!!

Tena naomba niulize hapahapa wataalamu, hivi harufu inapimwa kwa kipimo gani (mf, urefu ni mita, joto-baridi centigrade, uzito kg ...)
 
Back
Top Bottom