Ulishawahi kukutana na mwanamke/mwanaume mtandaoni akaku-prove wrong kinyume na matarajio kabla ya kuonana live?

Baada ya kujikita kusoma sana nyuzi za watu na mimi leo naandika uzi wangu.

Miaka mitano huko nyuma nilikuwa na tabia ya kutumia ukurasa wangu wa facebook kushare mambo yanayohusiana na utaalamu wa fani yangu, na watu wengi wakawa wanachangia maoni

Siku moja nikapokea text messenger kutoka kwa mtoto wa kike akinisalimia na kuhitaji msaada wa kimasomo, alikuwa anasoma telecom pale udsm.Tukaelekezana, tukaachana kwa hiyo siku. Mimi kama mimi sikuwa na interest nae kabisa na kadri siku zilivyokuwa zinaenda ndivyo nikawa napokea text za kunisalimu messenger zingine nikawa sizijibu hata zaidi ya mwezi.

Ukapita mwaka, ukaenda wa pili akawa anajiandaa kumaliza chuo na mimi nikawa siandiki tena kwenye wall yangu ya fb kama mwanzo kulingana na kutingwa na mambo yangu binafsi lakini bado akawa ananitext messenger, sasa kuna siku usiku nikiwa nimepumzika najiandaa kulala nakutana na mlolongo na message fb kutoka kwake mojawapo akiwa analamika kwamba simjibu message zake na kuna somo limemkamata anahitaji nimsaidie. siku hii ndio niliyojikuta napitia kwenye ukurasa wake kuangalia picha zake, nikakuta mara ya mwisho kuweka picha zake ni kama miaka 4 iliyopita halafu hata zilizopo ni za kawaida sana.

Kumbuka kipindi chote hiki sikuwahi hata kumfikiria, nilijua tu ni wale wanawake wagumu wa fani zetu za kiinjinia..Ule usiku tukaongea nae sana messanger pamoja na mambo mengine tukabadilishana mawasiliano rasmi, Baada ya mda akafanya UE akawa mtaani rasmi. Kipindi chote hiki hatukuwahi hata kuombana picha japo tulikuwa tunachart what'sapp, profile yake na yangu hakukuwa na picha zetu, tulikuwa tunawasiliana tu kawaida.

Alipomaliza akataka tuonane, Yeye ndiye aliyeomba hii appointment na mara kadhaa nikawa navunja ahadi ya kuonana. Sasa kuna siku ambayo tulipanga tuonane, Kesho yake ilipofika mimi sikuona umuhimu kwanza ndio alikuwa anamaliza shule na pili picha zake kule fb nilimuona ni mtu wa kawaida hata kimapenzi hakunivutia, sikuona cha muhimu kutoka kwake, na wala sikumpigia simu ili kumuelekeza sehemu ya kuonana badala yake nikawa niko kwangu na washkaji zangu tunapanga mikakati yetu.

Mida ya saa nne akanipigia simu anajiandaa kuja, Pale kwangu kuna rafiki yangu nilikuwa nae kiwembe sana nikampanga na kumuelezea kila kitu na jinsi tulivyokutana na huyo mdada nikamueleza kwamba nitamtambulisha kwake kama akivutiwa aweke mitego yake na akija kufanikiwa sio mbaya akawa koloni lake mimi siko tayari, saa sita napokea simu yake akiniambia tayari ashafika yale maeneo. Mimi na rafiki yangu tukatoka kwenda kumpokea, kufika pale hatuoni mtu ikabidi tumpigie simu, akatuelekeza mahala alipo.

Alisindikizwa na dada yake, alimpa lift ili amuache pale yeye aendelee na safari zake, kufika kwenye gari alilotuelekeza, walipaki sehemu ya kituo cha mafuta na yeye akawa tayari ameshaniona maana nilikuwa naongea nae kwa simu, Nikashangaa kuona mlango wa gari unafunguliwa Aisee alitoka mle mtoto mkali sikutaka kuamini macho yangu kama ndio yeye, tukasalimiana na dada mtu naye ni kisu hatari baadae dada mtu akatuacha akaendelea na safari zake.

Huyu mdada ni mzuri sana, mpole, mcheshi, anaongea taratibu. Na ahadi niliyompa rafiki yangu nikaivunja rasmi.
Sasa tukawa karibu zaidi tofauti na mwanzo, Niliridhika nae na nilipojaribu kumlinganisha na wale niliokuwa nao kwenye mahusiano sikuona kama wanamfikia iwe kwa tabia, uzuri, utafutaji hata uthubutu na hana ulimbukeni wa pesa, kwao amezaliwa amezikuta zipo nyingi tu.

Nikawa natumia pesa kwake kwenye kumnunulia zawadi na kumtoa out za gharama na wala sihisi kama nimepoteza.

Ikawa ni kazi nyepesi tu kuweka maombi yangu kwake, kama kawaida ya wasichana chenga za hapa na pale hatimae akaingia kingi mpaka leo ndio mke wangu.

Amenizalia watoto mapacha warembo kama yeye na familia yangu ina furaha sana. Familia yao ina watoto sita, wawili wa kiume na wanne wa kike na wote ni visu balaa, mungu anajua kuumba aiseee
Wapi kisa anahela tuu basi umeona gari ukaona mmh huyu wangu je angekuja na boda ungemwachia mshkaji.
 
Back
Top Bottom