Ulishawahi kukutana na mtu mwenye ugonjwa wa Low Latent Inhibition: Fahamu ugonjwa wa Low latent inhibition

View attachment 1546592View attachment 1546113
Mates,
Wakati wengi tukiwa tunajua kwaba ubongo wa mwanadamu umegawanyika sehemu tatu ambazo ni ubongo wa mbele,katikati na nyuma tu, kuna wataalamu wa masuala ya akili (Neuorologist) na wataalamu wa masuala ya ufanyaji kazi wa akili (psychologist) wamekua wakiamini/waki-Ague kwamba ubongo wa mwanadamu umegawanika katika hemisphere (pande) ambazo ni kushoto na kulia. Hivyo basi wanaamini kwamba mtu anaweza kuwa mtumiaji wa ubongo wa kushoto (left- brain) au mtumiaji wa ubongo wa kulia (right- brain)
Waumini wa dhana hii ya left-brained na right-brained wanaamini kwamba upande mmoja wa ubongo unaweza kuwa dominant kwenye upande mwingine wa ubongo, utamgundua mtu ni right au left brained kwa kutizama Tabia,mawazo na personalitiy ya mtu husika.Lakini pia wanasema kwamba pande hizo mbili za ubongo kila moja ina kazi yake tofauti na upande mwingine.

Ubongo wa kushoto.

Wanasema kwamba ubongo wa kushoto hua unajishughulisha zaidi na maswala ya Mantiki (Logical), pia wanasema kwamba watu wanatumia ubongo wa upande wa kushoto hua vizuri zaidi katika masuala ya mchanganuo(analytical), mahesabu, wanapenda zaidi kuatumia ukweli na uhakika,wanapenda kufikiria zaidi kwa maneno.

Ubongo wa kulia.

Wanasema kwamba ubongo wa kulia hua unajishughulisha na masuala ya ubunifu zaidi (creativity), ni watu wanaofikiria kwa upana zaidi, hua ni wanaofikiria bila kufungwa sehemu moja (critical and free thinker), hua hawaishii kufikiria bali kutenda kile walichokifikiria na hupenda kusimamia kile wanachokiamini kua ni kweli (intuitive)…..Toka miaka ya 1960 wataalamu hao wamekua wakifanya tafiti kuhusu dhana hizi lakini bado haizijapokelewa officially lakini bado tafiti zinafanyika tutaona huko mbeleni labda ikawa accepted officially hasa wataalamu wakifanikisha kuunganisha (embing) ubongo wa mwanadamu na Artificial intelligence.

LOW LATENT INHIBITION (LLI)

Mates kwa jinsi ninavyoelewa mimi neno stimulus kwa mujibu wa topic ya Co-ordination tafsiri yake kwa lugha ya Kiswahili ni kichochezi (vi). Mwaka 1897 mwanasaikolojisti Ivan Pavlov kutoka urusi alichapisha tafiti yake aliyekamilisha kuifanya inayohusu Classical conditioning…. Classical Conditioning ni hali ambayo hutokea pindi Vichochezi visivyo vya hiari (conditioning stimulus-CS) vinapoungana na vichochezi vya hiari (Unnconditional Stimulus-US). Pindi vichochezi hizi vinapotenganishwa kiumbe akina kichochezi kimojawapo basi anaanza kurespond kama kaona vichochezi viwil

Mfano 1.
Tuchukulie mfuga mbwa ni kichochezi CS na chakula cha mbwa ni kichochezi US, hivyo pindi mfuga mbwa akija na chakula mbwa ataona vichochezi viwili vimeungana kisha ataanza kurespond kwa kutoa mate au kuunguruma ili kuashiria kwamba anaenda kupata chakula, hali ikiwa hivyo kwa muda mrefu kuna siku atakua akimuona mfuga mbwa tu basi anaanza kutoa mate maana anajua anenda kupata chakula. Hali hiyo ndio Classical condition

Mfano 2. Kama wanafaunzi walishazoea kengele hua inalia ikishalia wanajua ni muda wa kupata chakula, hivyo basi hali ikiwa hivyo kwa muda mrefu wanafunzi watakua wakisikia kengele wanarespond kua wanaenda kupata chakula maana vichochezi viwili ambavyo ni chakula na kengele vimeungana, hata kama siku chakula kikiwa hakuna wakisikia kengele watashindwa ku-concertrate na kengele bali chakula. Natumai tumeelewana.

Sasa basi ndani ya hii Classic conditioning kuna kitu kinaitwa Low Latent Condition, kwa mliowahi kuangalia series ya Prison Break mtakumbuka kwamba Michael Scolfied alikua anasumbuliwa na ugonjwa (?) huu wa kiakili unaoitwa Low latent Inhibition, ugonjwa huu ndio ulipelekee Michael kua Smartest and Intelligent character in series history.

LLI inafanyeje kazi?

Schizophrenia ni ugonjwa wa kiakili ambao unamfanya mtu kuelewa/kutafsiri matukio kinyume na vile yalivyo, hivyo Low latent inhibition inahusuiana na Schizophrenia. Mtu mwenye Low Latent Inhibition hua anarespond kwenye stimuli/vichochezi za zamani au anavyovifahamu kama anavyorespond kwenye Vichochezi ambavyo ni vipya. Nikimaanisha kwamba mtu mwenye LLI akiona kitu ambacho ni kigeni ataanza kujiuliza kitu hichi ni kitu gani, kinafanyeje kazi, kwanini ni kipo hapa na maswali mengine kibao. Kutokana na maswali hayo mtu anajiuliza yatapelekea akifahamu kitu hicho kwa undani zaidi. Lakini pia siku akikiona kile kitu kwa mara ya pili hua anajiuliza tena maswali yaleyale juu ya kile kile kitu anachokifahamau na atahakikisha mpaka kapata majibu. So naweza kusema kwamba wakati wewe mtu wa kawaida unaona taa liko hapo juu linawaka basi mtu wa mwenye Low Latent Inhibition atazama ndani zaidi na kutaka kujua yaliyomo ndani ya taa hadi lipo hapo linawaka.

Kwa upande wangu LLI hua naiita kama Curiousity, kuna watu wengine humu wakiona ID imeposti kitu humu wataishia kusoma na kuondoka lakini kuna wengine hawataishia hapo watataka kujua ID hiyo ni ya nani na kwanini iposti mada hii, hivyo wataanza kupekua id hiyo. Mtu mwenye LLI hua haridhiki na kile anachokiona maana akili yake haiwezi kutafsiri kawaida vichochezi vilivyoko mbele yake, kiwe ni kichochezi kipya au cha zamani ambacho mtu anakifahamu..

Mfano.
Unaweza ukawa una tisheti mbili zainazofanana kila kitu, mtu mwenye LLI na asiye na LLI wakiona tisheti ya kwanza watarespond kama new stimulus (kichochezi kipya kwao) hivyo watakagua details zote juu ya hiyo tisheti. Siku nyingine ukiwa umevaa tisheti ya pili ukakuta na watu hao Yule asiye na LLI ataichukulia kwamba hicho ni kichochezi cha zamani (shati la kwanza) hivyo hatojishughulisha kujua details za tisheti hilo. Lakini Yule mwenye LLI akiona hiyo tisheti ya pili akili yake haitachukulia kama kama kichochezi cha zamani bali ataichukulia kama kichochezi kipya (tisheti la zamani) hivyo atachunguza kila details anazotaka kujua kuhusu tisheti hilo. Mwisho anaweza kugundua detail zingine ambazo hazipo kwenye shati la kwanza ambae Yule mtu asiye na LLI hakuzigundua
Kutokana na ugonjwa huu inaswemakana ndio kulifanya tupate watu ambao wamefanya dunia yetu kupiga hatua mpaka hapa ilipo, maana kila tafiti ya kisayansi hua inaanza na neno WHY? Na swali why ndio msingi wa watu wenye ugonjwa wa LLI.

Autodidactism

Autodidact ni neno linalotumiwa kuwaelezea watu wenye uwezo wa kujifunza vitu wa pekee yao (self-taught), kuna watu wamejaliwa kipaji hichi cha kujifunza wao pekee yao. Watu hawa hua hawahitaji mwalimu awasimamie au kuwafunza vitu ili waelewe bali wanachohitaji ni kujua is where to find right material for them to read…Watu hawa ukilazimisha wafundishwe na mwalimu kamwe hawawezi kuelewa, wataishia kufeli tu.

Mara nyingi watu wenye low latent Inhibition ndio hua na hali hii pia ya Autodidactism, wanasayansi wengi hawakupita vyuoni bali walitumia LLI yao kujifunza vitu na kugundua mambo mengi mapya..!

Baadhi ya watu maarufu ambao walikua ni autodidact ni galileo, Da vinci, Euclid, Socrates, Plato, Pythogras, nk.. zaidi unaweza kutizama orodha hapa..

List of autodidacts - Wikipedia.
NB. Usichanganye LLI na Umbea

~Vinci
el maestro..
Kweli!
 
Kuna uwezekano huu ugonjwa nao ukawa na categories zake, kuna ambao unakua acute na unapona kutokana na kuongezeka kwa majukumu, wengine unakua chronic na hauponi. I used to be curious and creative back in days, siku hizi naacha maisha yasogee
 
  • Thanks
Reactions: T11
mfano wapelelezi wengi wanatakiwa kuwa hivi.
kabla hajaanza kuulizia baadhi ya detail kuhusu kitu fulani tayari ameisha chunguza ni kitu fulani kwa uchache.

WWWW.hiyo w ya kwanza inasimama na WHY.
 
mfano wapelelezi wengi wanatakiwa kuwa hivi.
kabla hajaanza kuulizia baadhi ya detail kuhusu kitu fulani tayari ameisha chunguza ni kitu fulani kwa uchache.

WWWW.hiyo w ya kwanza inasimama na WHY.
Kuna somo nilisomaga 4yrs back ilikua inadili na maswali ya WH questions jinsi ya kuyajibu na kuyauliza..Ukimasta hako kasomo unajiona ushakua detective kabisa
 
Umenikumbusha mbali Sana na ningekuwa nimepata hili desa psychology ningepata 100 kipindi hicho napiga BA yangu pale Udsm, big up I appreciate ur thread!
 
Umenikumbusha mbali Sana na ningekuwa nimepata hili desa psychology ningepata 100 kipindi hicho napiga BA yangu pale Udsm, big up I appreciate ur thread!
Lakini si ulifanikiwa kumaliza desa lako kwa Gpa za juu
 
Kuna somo nilisomaga 4yrs back ilikua inadili na maswali ya WH questions jinsi ya kuyajibu na kuyauliza..Ukimasta hako kasomo unajiona ushakua detective kabisa
Bila shaka Hilo somo ni communication in art katika University of Dar Es Salaam
 
Mara ya kwanza nilifanyia reseach hii kitu ni 2007 niliikutana na LLI kwenye PB pale Sara alipoenda kumuuliza doctor/ mwalimu wa Michael kuhusu Michael ndio akawa anamweleza kuhusu Michael na LLI...

Nondo safi kabisaa
 
69 Reactions
Reply
Back
Top Bottom