Ulishawahi kukutana na mtu aliyevaa nguo zinazofanana na zako? How did you react to it?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya Cold War, jeshi na ujasusi wa KGB. Leo ngoja tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Eti ndugu zangu Watanzania;

HUMAN BEHAVIORAL PSYCHOLOGY.
============
Ulishawahi kukutana na mtu ghafla (kwenye sherehe, daladala au njiani) aliyevaa nguo zinazofanana na za kwako? How did you react to it? mlipungia mkono, mlipeana tabasamu, mlimfuata kumsalimia au ulikwepesha macho?

images (7).jpg
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kijana wangu Infantry Soldier unaonekana bado umri wako mdogo sana kwa hapa jukwaani.

Kuna kipindi fulani nilikaa London kwa muda wa miaka mitatu ya masomo. Yaaaani If I saw the same shirt I was wearing on another person at a party, I would walk up to them and say; Great shirt! I love you taste," or something along those lines.

The last thing you want to do is stand on the opposite side of the room, glowering at that person, wishing them out of your shirt. They feel the same embarrassment you do.
 
Haijawahi nikuta. Mostly kwakua navaa nguo za mtumba ila viatu mara mbili tatu hivi. Nishakutana na mtu kavaa flight Jordan kama niliyovaa mpaka rangi, travolta mpaka rangi, New Balance na Moka.

Mara zote nilijifanya sijawaona.
 
Mimi nilikutana na mtu tunafana sura,urefu ,skin color,
Mkuu, mara zote aina hii ya mfanano huwa ni ya kuambiwa na third party kuwa mbona wewe na fulani mnafanana sana lakini sio ya wewe na huyo jamaa kugundua kuwa mnafanana.

Hii issue ya mavazi/outfits si suala la mpaka kuambiwa na third party bali ninyi wawili ndio mnajikuta mnatazamani machoni na kupeana Hi
 
sijawahi ila kukutana na mtu aliyevaa nguo ambazo hata mimi ninazo ni kawaida
 
Mimi haikuwa nguo bali magari..zote zilikuwa
Make: Toyota Cresta
Model: GX 90
Color: Silver
Registration: T800ABJ , T800ADJ
nilikuwa wa kwanza kupaki nikaingia duka la spare...akaja jamaa akapaki sawa sawa na mimi naye akaja dukani
Sikuwa makini kuhusu gari yake hivyo nilipanda yangu na kutaka kuondoka ...ghafla nikamuona jamaa keshajaa mlango wa dereva anapiga kioo..alidhani nimeiba gari yake
Nikapaki nikashuka ..kwa dakika nzima wote tulichanganyikiwa mpaka tulipokuja kuona tofauti ya number
Mpaka rims zilifanana...
Hi ilinitokea pale kituo cha garage External mwaka 2009
 
Miaka ile ya 1990s kuna wakati nilikwenda Arusha, nikiwa ndani ya "SAVCO jeans, white T-shirt & white rubber shoes". Sina hili wa lile nikapita pale hoteli ya Golden Rose, na ile nafika karibu na uwanja wa Sheikh Amri Abeid, nikakutana na kundi la vijana wa "promotion" wa BONITE BOTTLERS waume na wakike wote tumeulamba sawa sawa na mimi.

Wakiwa ndani ya gari lao la matangazo, wacha waanze kunishaishangilia. Du! Nilijihisi vibaya sana, ikanibidi mdogo mdogo nirudi zangu mdogo mdogo nilikotokea. Kusema ukweli kila mtu anataka upekee wa aina fulani, ikitoea mfanano fulani inakuwa kama date za "uniform"
 
Nilikua natoka zangu hostel naenda class nimepiga suruali nyeusi na shati fulani hivi za njano (ya duka), wakati nikiwa njian nikakutana na jamaa kavaa vile vile, nikapuuza baada ya hatua chache nikakutana na watu wengi wakiwa wamevaa vilevile dah nilistuka sana.kumbe walikua wanakwaya aisee na ilikua ni siku ya jumapili. nilikosa amani kutwa nzima. nilivyorudi kitaa(likizo) nikampa dogo na nikaapa kutokuja vaa nguo za duka tena.
 
Back
Top Bottom