Ulishawahi kugombana na mfanyakazi mwenzio ofisi moja ?

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,321
2,000
Haya ni mambo ya kawaida sana katika jamii yenye watun wa haiba tofauti. Kuna watu wamezaliwa na visirani na kubadilika ni ngumu, Unakuta anaamka asubuhi anaanza kukuchukia tu bila sababu kama mama mjamzito.

Dont hate back wewe msalimie tu asipokujibu atajiju. mwishowe atajionea aibu mwenyewe.
 
haszu

JF-Expert Member
Oct 10, 2017
750
1,000

mkuu kuna mmoja nawaza nimuulize kama kuna jambo lolote nimemfanyia au nikaushe tu ivi ivi, ata sielewi. Tho, naweza kua cool na mimi na mambo yakaenda
 
Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,984
2,000
Tangu siku nilipojua kimya ni jibu la mjinga niliacha kujipa stress na mambo nisioyajua vyanzo vyake hata yasio nipa faida kwa kweli nilikaa tu kimya nikimsalimia haijib salam yangu niliacha na kumsalimia na mm nikawa nafanya mambo yangu vile itakiwavyo ubaya ni tunakaa ofisi moja alikuja kunisemesha mwenyewe
 
kyaibumba

JF-Expert Member
Sep 8, 2017
646
1,000
Nshagombana sana na jamaa mhasibu wa kampuni yetu kisa ubaguzi, ananibagua kisa Mimi mweusi
 
NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,961
2,000
Unafanyake ikitokea, mfanyakazi mwenzio amebadilika juu yako, bila ww kujua kosa gani umemfanyia? Unaishi nae vipi?

Mmmh! wa hivyo ndio nawatafuta, shenzi type, yaani mie mtu akithubutu amekwisha.
Sala: Eeee Mungu ninusuru na hii tabia yangu ya ushari.
 
nipekidogo

JF-Expert Member
Apr 17, 2019
1,593
1,980
Huwa inatokea kutofautiana mitazamo, ilitokea mtu flani kazini tulitofautiana ikafikia wakati tukawa hatuzungumzi japo hatukuwahi kujibizana wala kuulizana nini tatizo, ikatokea tukapangwa team moja na tukawekwa Ofisi moja na tunashare meza moja kwa tofauti ya computer, kwasasa tumekuwa watu wa karibu sn kazini more than friends hata nje ya kazi na mpaka Leo hatujawahi kuzungumzia kilichotokea!
 
Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
824
1,000
Jifunze kusamehe na kusahau kwa kumaanisha haijalishi umeumizwa kiasi gani. Hii hali hutokea kwa njia au sababu mbalimbali inaweza kuwa wivu kimaendeleo, kimaisha, kiakili, kiuwezo ktk utendani, kukubalika ktk ofisi au kuzungumzwa vizuri zaidi au kinyume chake.
Kikubwa ni kusamehe maana kila jambo unaloliona ktk mwili chanzo chake kinaanzia rohoni.
Ukijiepusha kwa kusamehe na kusahau, wewe huyo mtu mjali kama zamani usipunguze upendo kwake ikibidi jitahidi uongeze utapata kujua baadae hasira ikiisha.
Tupendane na kuchukuliana madhaifu yetu. Leo kwake kesho kwako. Utakavyomtendea leo ndivyo utakavyotendewa kesho.
 
Sasa mkuu mfano mimi, simchukii wala sina kosa nae, ila yeye unaona hayupo vizuri na mimi bila kueleza ttzo nini. Sasa nimfanyeje ?
 
Hammaz

JF-Expert Member
May 16, 2018
3,698
2,000
Onyesha upendo tu! Wala usimkasirikie na fanya kama hakija tokea kitu. Muhimu ni kufanya naye kazi kwa uangalifu kwa sababu kwenye kazi kuna fitna nyingi.

Ikiwa ni masuala ya fitna kwenye kazi anakusababishia, mwambie tu. Kwamba anachokifanya si kizuri na hupendezwi nacho. Hii itakusaidia yeye kukufahamu ni mtu wa namna gani na itakusaidia kumjua yeye ni mtu wa namna gaini. Kwa hiyo umakini ni muhimu kufanya kazi na mtu huyo.

Ilinitokea kazini katika mazingira ya fitna na binafsi sipendi makwaruzano kwa sababu nikimbughudhi mtu moyo wangu huwa unakosa amani. Mazingira aliyonitengenezea nionekani sifanyi kazi. Nikamwambia tu mwenendo unaokwenda nao si mzuri.

Alijifanya kupaniki kuongea kwa ukali mi sikuwa hata na pressure nilikuwa naongea taratibu kama billionaire fulani hivi. Then nikapotezea nikachukulia ni sehemu ya changamoto. Kesho yake asubuhi namsalimia mwenzangu buyu! Nikimuuliza kitu anajibu kimkato! Nikaona siyo mbaya.

Daily nikifika mi nikawa namsalimia tu. Alikula buyu mpaka alichoka! Mwisho wa siku akaishia kuniita ni dhaifu. Maadamu nilishamtambua ni mtu wa namna gani, nikifanya naye kazi nafanya kiuangalifu ili chochote kikitokea nijua jinsi gani ya kujinasua. Plus mi ni mtu wa kueneza mapendo tu, mtu akinichukia ataumia mwenyewe na ndicho alichogundua kutoka kwangu.

Maisha yenyewe mafupi yanini sasa uishi kwa fitna na chuki.
 
Dharra

JF-Expert Member
Jun 23, 2017
1,667
2,000
Ofisini dawa ni kuwa kimya tu, unaongea kwa nadra sana, unawahi mapema na kuondoka kwenye mda unaotakiwa kuondoka. Hata mtu akikusemesha wewe majibu yawe mafupi tu, usishiriki kwenye vikoba na vikundi vya majungu wakati wa chai asubuhi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom