Ulishawahi kuambiwa "wewe siyo type yangu" baada ya kueleza hisia zako?

CarloJesus

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
431
833
Ushawahi kukutana na swali hili: "Hivi unanionaje; jamani muoneni huyu!! Hivi nina mkosi gani mimi?!" Baada ya kumwambia au kumuonesha mtu unampenda? Au ushawahi kuambiwa "we siyo type yangu?"

Wakati kupenda linaaminika ni zawadi ya Mungu kwa wanadamu, kukamilisha furaha ya juu kabisa ya baraka zote ambazo Mungu kaziweka kumzunguka binadamu kama mali nk, upendo ndio utimilifu wa yote, wengine imekua ni fimbo ya kuvunja mioyo ya watu kiasi wamejiona siyo kitu tena.

Ndio, ndio maana mtu anakwambia nahangaika ili familia yangu ifanikiwe katika hili, katika hili na lile. Familia ni matokeo ya Upendo.

Dada mmoja na kaka mmoja walivutwa na upendo, kwahiyo inakuja kuleta maana kubwa sana baadaye, watoto, wajukuu nk. hadi kutengeneza amii ya kuchukuliana na kuvumiliana katika kubebeana madhaifu katika shida na raha, yaani FAMILIA.

Jambo hili jema mara nyingi mwanzo wake umekua wa vituko vingi na wakati mwingine maumivu kama siyo kabisa kumkosea alieliumba, yaani Mwenyezi Mungu.

Wako ambao leo ni mume na mke kwa sababu tu walipigana vikumbo katika daladala au walikutana masomoni, au ya uadui wao. Ni vema Basi tujifunze kuuheshimu mwanzo mzuri unaweza kuleta kitu kikibwa kizuri zaidi. Kila mtu hupenda kupendwa hata wale ambao wana kasoro kiakili; hata walio katika comma hupenda kupendwa; watoto wachanga pia, hutabasamu wakiambiwa wanapendwa.

Dada inawezekana una "mshape" wa haja, una chura, una sura nzuri kama malaika, wewe ni mzuri saana kiasi watu wanajikwaa barabarani, ukiambiwa unapendwa, bila kujali na nani au mtu gani ameonesha hisia kweli za kukupenda, hiyo ni zawadi kubwa sana amekupatia. Usimdharau, usimshushe mtu kwa maneno ya kumnyong'onesha kama wewe siyo type yangu, unanionaje nk. Hata kama hujavutika naye, ogopa dhambi ya kujiona kuwa wewe ni daraja nyingine ya binadamu na kuanza kudharau wengine.

Hiyo ni housing tu na ina undergo deterioration as well. Kumbuka hiyo shape, hilo tako, hiyo sura ni namna inayofaa tu, labda Mungu ameiweka kukukutanisha na Mr Right wako.

Nadhani unajifunza ma first lady jinsi wako wa kawaida na wanaume wao wanaonekana kutulia kabisa; labda wako wanawake kibao leo wakimuona Magufuli, Kikwete, Kenyatta n.k walifanya kosa kama hilo. Tafuta namna nzuri ya kumshukuru Mungu wako kwa zawadi ya uzuri kuung'arisha na usafi, unyenyekevu, utu wema, saburi na uvumilivu.

Kaka kweli inawezekana una umbo, sura nzuri, lakini financially uko vizuri pia na yoote yanayofanya wanawake/dada zetu wengi wakose amani kwa kuhamanika kukukosa hata kama hawajakupata kwa mvuto wako.

Ni kweli labda tayari roho ya kiburi imekuingia na una standards zako unataka mwanamume wako awe nazo lakini Mungu amekuweka katika Jamii. Hizo standards ni za nje tu, ndani ya moyo hao wanawake wanatumia sawa, wanapendana sawa. Ikitokea, ametokea mmoja akaonesha kukupenda au anakwambia anakupenda, tafadhali usimvunje moyo; ng'arisha mvuto wako na busara asiondoke ameumia hata kama umeshaamua huwezi kuwa naye.

Mwisho nisiwachoshe. Ni ngumu kukutana na mtu umevutika naye sana, naye amevutika nawe sana. Tunachofanya kufanikisha hili, ikitokea fulani ameonesha kukupenda sana usipuuze hata kama unaona haja-meet 100% ya matarajio yako, wala usimvunje moyo.

Kama hisia zako lau kwa mbali unaona unamkubali kubali, basi just huyo ni "Mr Right au Mrs Right"

We learn to love. Niliwahi kuvutika na binti siku ya kwanza nkachukuwa na no ya simu, lakini kesho nikamuona tofauti, kesho yake zaidi, kila siku nikianza kumuona mtu mwingine.

Mwisho nikajilaumu kwanini nilichukua no ya simu.

Ukipendwa pendeka, usivunje watu moyo.

78a7d74c2f87c01d4793e4ea80e3bde7.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujumbe mzuri sana.

Kimsingi kumjibu mtu kwamba sio type yako ni sawa kwa kumaanisha sio wa aina yako lakini ni mbaya sana kihisia kwa anayeambiwa, nampunguzia sana kujiamini.

Kuwa na ubinadamu na kuweka akiba ya maneno ni jambo la msingi sana katika haya maisha.
 
Ujumbe mzuri sana

Kimsingi kumjibu mtu kwamba sio type yako ni sawa kwa kumaanisha sio wa aina yako lakini ni mbaya sana kihisia kwa anayeambiwa inampunguzia sana kujiamini.

Kuwa na ubinadamu na kuweka akiba ya maneno ni jambo la msingi sana katika haya maisha
Kabisa. Na wengi hali imeharibu kabisa maisha yao japo huwa ni kazi kutrace.

Mtu akikosa kujiamini hawezi kutambua hata potentials zake. Anabaki Ni victim wa humiliation siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya nyuma nikisoama Advance pale Arusha, kuna binti mmoja kumbe tangu siku ya kwanza kuniona alinipenda sana. Mimi sikuwa na habari japo alikuwa kama anapenda kuwa karibu na mimi, nikajua labda ni kimasomo maana nilikuwa vizuri kwenye Uchumi na Pure.

Sasa siku ya mwisho tumemaliza mitihani kabla kesho yake hatujatawanyika, alinifuata akaniambia ana zawadi yangu, anaomba baada ya chakula cha jioni (saa1) tuonane darasani. Kulikuwa na Rafiki yangu mmoja wa karibu sana, nikamwambia E anasema ana zawadi yangu nikaonane naye darasani. Jamaa alinicheka sana akaniambia yule demu anakupenda sana. Sasa jamaa alinicheka sana mana kwa muonekano wangu ni kama bint haendani na mimi.

Kweli nikakutana nae jioni, kwanza alianza kuniomba samahani kwa atakayoyasema, na akasema anajua hatafanikiwa lakini hawezi kuondoka shuleni bila kuniambia linalomsukuma kwa muda mrefu, ndio akaniambia alinipenda tangu siku ya kwanza kuniona, na nilishangaa anakumbuka matukio tangu mengi sana hata nisiyo yakumbuka mwenyewe.

Alilia akaniambia muda wote nikikuona napatwa na kitu moyoni, lakini najiona sio wa level yako, mwisho akanikabidhi Diary aliyokuwa anaandika kila kitu juu yangu tangu siku aliponiona, na ameweka record vizuri na tarehe. Nilishangaa sana, mimi sikuwa na hisia naye na nilimwambia ahsante, nikamwambia ninae mchumba tiari.

Alilia kiasi akaniaga. Sikuwahi kumuona mika mingi mpaka miaka mingi baadaye naona FB anaomba urafiki, kumuangalia nakumbuka jina tu, bint amekuwa mrembo balaaa, nikamtamani sana lakini sikuweza kumwambia lolote mana nilikuta picha za sherehe ya ndoa na mtoto mdogo tiari.

Nikasema wanawake wote ni warembo wanahitaji AMANI ya moyo na matunzo. Sitakuja hata siku moja kumwambia mwanamke eti sikutaki wewe sio type yangu. Wanawake wote ni warembo. Nawapenda sana.

Safi Mkuu, hongera pia kwa hekima. Advance school wengi huwa na utoto, mwingine angeweza hata kukataa mwito kama sio kumuaibisha pia. Uli act ki-gentleman. Umenikumbusha same situation iliwahi nitokea chuo. Kuna muda niligombana na wale waliodhani kuwa nastahili kuwa nao tuu wao, lakini baadae ilinipa heshima sana.

Big up

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi situation huwa zinatukuta sana sisi wanaume.

Miaka ya 2000's nilimpenda sana dada mmoja hivi ila nilipenda kumwambia anilinijibu kwa kejeli sana tena aliniambia kuwa sio wa hadhi yake na sina uwezo wa kumlisha na kumuhudumia.

Ila life is karma the lady now ameolewa na kijana muhuni tu hana mbele wala nyuma isitoshe huyo mwanamke anauza vitumbua na sambusa. Nikiwa naenda kutembelea yale maeneo huwa ananionea aibu sana maana amekuwa mzee zaidi yangu na ana watoto watatu .

Wakati nipo O level kuna binti alinipenda ila mimi sikuwa na hizo hisia kabisa juu yake , enzi zetu kadi ndio zilikuwa kwenye chati, Hivyo binti alinunua kadi na perfume nzuri na maua akampa rafiki yake akaniletea , nilisoma ujumbe uliopo kwenye ile kadi akaniwekea dedication wimbo wa Westlife ''My Love''. Sikumvunja moyo nikamuita nikamwambia ujumbe wako nimeupata ila sasa hivi kama unavyoona tupo shule . Tuzingatie masomo tukimaliza tu mtihani wa kidato cha nne tutafungua ukurasa rasmi wa mapenzi.

Kweli msichana alinielewa tukaanza mahusiano kwa style hiyo ukizangatia kwao walikuwa njema basi nilifaidi sana zawadi zake. Kuna mwamba alikuja akaingilia kati penzi akamtwaa yule msichana nilishukuru sana kwanza sijawahi sex naye as sikuwa na hisia naye. Lakini sikuwahi kumwambia na mpaka anachukuliwa na mwana niliigiza kuumia tu ili ahisi aliuteka moyo wangu.

Haipendezi kumvunja tu moyo kwa majibu ya karaha, binaadamu tuna akili hivyo unaweza ukamwambia mtu jambo akalielewa tu bila maneno ya shombo na akafuata hamsini zake kiroho safi.
 
Hizi situation huwa zinatukuta sana sisi wanaume..

Miaka ya 2000's nilimpenda sana dada mmoja hivi ila nilipenda kumwambia anilinijibu kwa kejeli sana tena aliniambia kuwa sio wa hadhi yake na sina uwezo wa kumlisha na kumuhudumia.

Ila life is karma the lady now ameolewa na kijana muhuni tu hana mbele wala nyuma isitoshe huyo mwanamke anauza vitumbua na sambusa. Nikiwa naenda kutembelea yale maeneo huwa ananionea aibu sana maana amekuwa mzee zaidi yangu na ana watoto watatu .

Wakati nipo O level kuna binti alinipenda ila mimi sikuwa na hizo hisia kabisa juu yake , enzi zetu kadi ndio zilikuwa kwenye chati, Hivyo binti alinunua kadi na perfume nzuri na maua akampa rafiki yake akaniletea , nilisoma ujumbe uliopo kwenye ile kadi akaniwekea dedication wimbo wa westlife ''my love''. Sikumvunja moyo nikamuita nikamwambia ujumbe wako nimeupata ila sasa hivi kama unavyoona tupo shule . Tuzingatie masomo tukimaliza tu mtihani wa kidato cha nne tutafungua ukurasa rasmi wa mapenzi.

Kweli msichana alinielewa tukaanza mahusiano kwa style hiyo ukizangatia kwao walikuwa njema basi nilifaidi sana zawadi zake. Kuna mwamba alikuja akaingilia kati penzi akamtwaa yule msichana nilishukuru sana kwanza sijawahi sex naye as sikuwa na hisia naye. Lakini sikuwahi kumwambia na mpaka anachukuliwa na mwana niliigiza kuumia tu ili ahisi aliuteka moyo wangu..

Haipendezi kumvunja tu moyo kwa majibu ya karaha, binaadamu tunaakili hivyo unaweza ukamwambia mtu jambo akalielewa tu bila maneno ya shombo na akafuata hamsini zake kiroho safi.
Kabisa Mkuu, ulifanya jambo jema

Na wakati mwingine Kuna Jambo unamuomba Sana Mungu. Kumbe Mungu Anataka yule mtu awe mikono ya wewe kupata hilo jambo, sasa unakosa busara unamfukuzia mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama demu akikwambia ww sio type yake usimlaumu bali ni njia ya ww kutafuta mwingne tusilazimishage haya mavitu,hv fikiria huyo msichana anatongozwa na wanaume zaid ya 100 atawakubali wote???...tena mm mtu akiniambia hvyo huwa nashukuru coz kuna mtu anaweza akakukubalia kinafk halaf baadae,akaja kukuvunja moyo so bora ukwel mchungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Mara baada ya kutongoza nikakubaliwa niliombwa 500,000/- nikajua tu hapa sitakiwi na Mimi siyo type yake,
Mwingine nilimtongoza akaniambia eti nikatafute type yangu Mimi wala sikumjibu vibaya nilimwambia tu wanawake wako wengi sana huko peke yako.
 
Hii sijui ni mule mule!?

Kuna mdada wa chuo nampenda mno nayeye analitambua hilo, nikamtongoza akanikataa kwa ujasiri kama wa buku tano hivi mia nane hamsini mia tisa mia nne arobaini. Hiyo siku ikapita, mara nyingine nilimtongoza akanijibu You Dont Deserve Me, mara nyingine tena siku nyingine akanitamkia hilo neno nikamwambia Asante ila siku nyingine kuwa na Akiba ya maneno
 
Mpaka mfike huko basi ujue wewe uliyeambiwa hivyo una matatizo kichwani, kwani kwa kawaida demu mpaka aseme hivyo ina maana ameshakukataa lkn haukubali na unataka kumlazimisha!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom