Ulipokuwa UDSM nakumbuka ulisema kuwa 'Unateua' tu 'Wasomi' hasa wenye 'Masters' na 'Doctorates' pekee katika Serikali yako, leo Kulikoni umegeuka?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,172
2,000
"UONGOZI SIO MADEGREE" MAGUFULI

"Uongozi sio Madgree, ni kipaji unachopewa na Mungu, Mbunge wenu Lusinde ni Kijana mzuri anafanya kazi nzuri, ndio maana ni Mjumbe wa NEC,niliahidi Barabara ya lami KM 16 kutoka Mlowa hadi Mvumi, RC njoo nikuagize tumalizane hapahapa,zege halilali"-JPM akiwa Mlowa, Dodoma

"Zege halilali, RC Dodoma mwagize Meneja TANROADS Mkoa wa Dodoma huu mwezi wa tisa ndani ya miezi miwili Barabara ya Mlowa kwenda Mvumi itangazwe tenda kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami ili wagonjwa wanaougua hapa wawe wanapelekwa Mvumi”-JPM

"Nileteeni Wabunge wa CCM ninao uwezo wa kuwatumbua mkiniletea mwingine sina uwezo wa kumtumbua, pesa zitaliwa na sina cha kumfanya, Mbunge wenu Lusinde ni mchapakazi, narudia Ubunge sio Madegree ni uwezo wa kujenga hoja"-JPM

“Nawapenda sana watani zangu Wagogo, naamini kabisa mtanipa kura, nimekuja kujifunza na Kigogo, tena inawezekana Lusinde akanitafutia Kasichana kazuri ka Kigogo au mnasemaje Wagogo?, si mtanipa?" - JPM

"Hata kuhamia Dodoma haikuwa rahisi tumekaa zaidi ya miaka 47 hilo halijawezekana, tunajenga uwanja wa Ndege mkubwa Msalato, Ndege zote za Kimataifa zitakuwa zinatua hapa, tumejenga Reli, Soko na Stendi ya kisasa, tunataka kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa"-JPM

ccmamaniyatanzania

Sasa GENTAMYCINE nadhani taratibu ninaanza kuyapata 'Majibu' ya kwanini 'Mjeruhiwa' anakubalika na 'Mtawala' haaminiki tena na Wapiga Kura.
 

Graph Theory

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,784
2,000
Akiwa anahutubia Samira, kajikanyaga hadi kero. Mara aseme msichague wapinzani maana hawatawaletea maendeleo, kisha tena anasema maendeleo hayana chama.

Aliyemmezesha script ya maendeleo hayana chama, inabidi afanye utaratibu wa kui-format kutoka kichwani kwake.

Kwa tuliosoma logic hiyo kauli itaishia kwenye fallacy.

Hivyo jamaa anaongea uongo mtupu.
 

Mshughulishaji

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
874
1,000
Hiyo na mimi kama nakazia juu ya kuelewa na nafikiri bado zipo sababu nyingi sana zaidi Ya hii moja ya kuruka na kuyapinga maneno na kauli zetu za awali.
 

mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
3,722
2,000
Si alimalizia sentence kuwa anatafutiwa kasichana ka kigogo?

Hivyo uongozi kwa ccm sio degree ila ni connection za kumtaftia boss Mali ya kubonyeza kama alivyokuwa anafanya DAB
 

mangikule

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
4,245
2,000
"UONGOZI SIO MADEGREE"
Tena inawezekana Lusinde akanitafutia Kasichana kazuri ka Kigogo au mnasemaje Wagogo?, si mtanipa?" - JPM....[b/]

Mwisho wa kunukuu
Kumbe huyu kibaka bado anakumbuka alivyokuwa anasumbua mabibo hostels! Ni lazima tumpeleke huyu majinuni chattle!
 

This is...

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,709
2,000
"UONGOZI SIO MADEGREE" MAGUFULI

"Uongozi sio Madgree, ni kipaji unachopewa na Mungu, Mbunge wenu Lusinde ni Kijana mzuri anafanya kazi nzuri, ndio maana ni Mjumbe wa NEC,niliahidi Barabara ya lami KM 16 kutoka Mlowa hadi Mvumi, RC njoo nikuagize tumalizane hapahapa,zege halilali"-JPM akiwa Mlowa, Dodoma...
NEC hii Ni rushwa,au hamuoni.
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
11,884
2,000
"UONGOZI SIO MADEGREE" MAGUFULI

"Uongozi sio Madgree, ni kipaji unachopewa na Mungu, Mbunge wenu Lusinde ni Kijana mzuri anafanya kazi nzuri, ndio maana ni Mjumbe wa NEC,niliahidi Barabara ya lami KM 16 kutoka Mlowa hadi Mvumi, RC njoo nikuagize tumalizane hapahapa,zege halilali"-JPM akiwa Mlowa, Dodoma...
Wewe ni rafiki/ndugu yangu bado nakuhtaji. Nasikia ukimpinga kama hivi linakupata la kukupata? Uwe makini!!
 

Koffi Yardley

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
553
500
Mkuu:
1. FINESSE- Impressive delicacy and skill - e.g " political playing of great

2: INTEGRITY - the quality of being honest and having strong moral principles.

3: PRESIDENTIAL MATERIAL - has among others, having qualities 1,2, ... ad infinitum

Pamoja na UTAMADUNI wa UTANI, yapo ya kutania KIHUNI and otherwise. MHUNI hata AKIJAMBISHWA atafanya yale yale yaendayo na hayo. Aweza KUJAMBA pia hapohapo! Shame
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
1,403
2,000
Aisee,

Yaani bado tu anahubiri tenda za barabara?

Na hizi 'dry sense of humor' za mume wa mtu kutaka kabinti kadogo hadharani kila kona anayopita ni kama kujidhalilisha sana.

Hawamuandikii tena cha kuongea?? Sielewi Kwann walijifungia Dodoma kama wamerudi worse than before.

Kauli za mkichagua upinzani sileti barabara zinanidisappoint.
Harakaharaka yawezekana ni pandikizi la upinzani, aisee :D

Everyday is Saturday.............................😎
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,535
2,000
Magufuli haishi maneno yake, ni kigeugeu.

utamsikia akisema maendeleo hayana chama...

Then mkiwachagua wapinzani siwaletei maendeleo....

Haaminiki tena.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom