Ulipokuwa chuo au kazini uliwahi kupitia haya na ukaamini hakuna Mungu kabisa?

Dadavua ni siri gani ulikuja kugundua na ulifanya vipi hadi mambo yakakaa safi.....
 
Yaani kama wewe ni msomi na unaamini huo upuuzi wa "kuchezewa"basi wewe ni hasara kwa Taifa.yaani akili uwe nazo wewe!harafu kwenye kujibu mtiani mtu mwingine afaidike na akili zako wewe!!yaani kama moja jumlisha moja ni mbili ,wewe kwenye mtiani wako huwndike tatu,harafu,jibu sahihi litokee kwenye mtiani wa mtu mwingine!!we jamaa ni kichwa maji kabisa.
Jina uchawi umelijulia hapa Nini, mnajifanya mnaelimu kwenye maudhi ya watu kumbe Ni wauni flani tu.
 
Wakati nikiwa chuoni pale Mlimani, nilipitia kitu cha ajabu sana. Nilikuwa nasoma SANA, kwa maarifa na juhudi, ila matokeo yakija najikuta nina nne kati ya kumi, assignments kupata 2/5 ilikuwa ni kawaida mno kwangu. Kuna wale ambao walikuwa wanakesha club unakuta wanapata marks za juu, wasichana ambao walikuwa wanakesha kwa madanga weekends, wanapata higher marks than I got! Nilikuwa naumia sana.

Ni miaka mitano baadaye ndio nikaigundua SIRI, kwa nini hii nilikuwa naipata mimi tu? Mbona nilikuwa nina juhudi? Mbona nilikuwa nasali sana? Ilifika wakati mpaka nilitaka kwenda kwa manabii kuwekewa mikono na kuombewa ila nilikuwa ninaghairi tu nikiona ni kawaida, wakati huo nikizidi kudidimia katika giza nene.

Nilianza mpaka kuhisi nina MAPEPO, why me? Nilijiuliza sana swali hili. Kwa nini mimi? Kumbe nilikuwa nachezewa, na ukizingatia sikuwa naamini haya mambo, kumbe watu walinichukulia point hapo, nikawa nachezewa ila niliona ni hali tu ya kawaida, hakuna uchawi, japo nafsi ilinishuhudia sipo salama.

Mpaka hapo nilipochukua hatua, niliona mabadiliko makubwa, fikiria ningemaliza chuo na 1.7GPA? HII NILIIGUNDUA MWISHONI MWAKA WA PILI. JAMANI KUCHEZEWA KUPO, KUNA VIMICHEZO VYA KIJINGA SANA VYUONI, JAPO VIJANA HATUAMINIGI HIVI VITU.

Yaani jitu limekaa huko halisomi halafu linatumia kichwa changu kufaulu, haya mambo yapo aisee, sijui wanatumia mechanism gani mpaka MTU anafaulu kwa akili yako.
Nimejifunza somo kubwa mno nikiwa chuo. Namshukuru Mungu. Siku nikiamka vizuri nitaleta kisa kizito cha yote yaliyonipata wakati huo.

Uliwahi kupitia hali hii ukiwa chuo au kazini? Tupe uzoefu wako watu wapone, hali inatisha.
Mimi na baadhi ya wanafamilia tumepitia majaribu mengi sana , uchawi upo narudia tena, uchawi upo.
 
Yaani ulichezewa na wanachuo wenzio? Mmh ebu malizia story tujue ilikuaje maana hata sijaelewa na siamini hivo vitu
 
Mika 2012 huko kuna kisa kimoja humu kilipata kuandikwa, mtu anafanya mtihani majibu yanaenda kwa mwingine.
 
Brother, ulikua na uwezo mdogo. Hivyo vingine ni visingizio tu. Kama umesema ulikua unasali sana, iliwezekanaje ukachezewa?

Hata hao unaosema watu wa bata na wadangaji, wapo vilaza na vipanga pia. Nimesoma chuo na mdada anakigawa kinoma, masela karibia wote walipita nae. Ila class alikua anaperfom safi tu. Na kuna mdada alikua mtu wa dini kinoma, hana mambo mengi tofauti na kanisa na shule. Yeye aliweka rekodi ya kupiga SUP tano ( alizichomoa zote).

Kwahiyo haukuchezewa kaka, ni uwezo wako uliishia hapo!
Huu uzi ungefungwia hapa, ufafanuzi umijtosheleza kabisa na hahitaji nyongeza.
 
Brother, ulikua na uwezo mdogo. Hivyo vingine ni visingizio tu. Kama umesema ulikua unasali sana, iliwezekanaje ukachezewa?

Hata hao unaosema watu wa bata na wadangaji, wapo vilaza na vipanga pia. Nimesoma chuo na mdada anakigawa kinoma, masela karibia wote walipita nae. Ila class alikua anaperfom safi tu. Na kuna mdada alikua mtu wa dini kinoma, hana mambo mengi tofauti na kanisa na shule. Yeye aliweka rekodi ya kupiga SUP tano ( alizichomoa zote).

Kwahiyo haukuchezewa kaka, ni uwezo wako uliishia hapo!
Hujui unalosema. Kuna scenario zingine ni uwezo mdogo, ila pia kuna zingine si uwezo mdogo. Hii dunia, ina pande mbili.
 
Back
Top Bottom