Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Taarifa za kifo chake nilizipata trh 9 kutoka kwa mtu ambae hawezi kudanganya ila nikajua uzushi tu.
Tetesi zikaendelea mitandaoni, sasa siku ya trh 17 saa 11 alfajiri nilikosa usingizi nikaingia jf nikakuta mtu kaweka uzi akisema " si watangaze tu raisi wa nchi yupo kwenye fridge wiki nzima si watangaze"

Yesuuuu, moyo ulidunda mbio nikatoka kitanda nikashika biblia sikuifungua nikapiga magoti nikasema Mungu nakuomba hiki nikachokihisi nikilinganisha na tetesi za mitandaoni mungu naomba isiwe ni kweli.
Yaani nilihisi naumivu ila nikajisemea hapana hizi hisia mbaya nikajiandaa nikaenda kazini.

Nikiwa ofisin kuna kijana mmoja kaingia akicheka kweli akasema "jiwe lazima lidondoke" nilimjibu magufuli hafi leo tukaishia hapo.

Nyumbani nilifika saa 3 nikajilaza kwenye sofa nikapitiwa usingizi, sasa nikiona simu ya mama inaita najua ni saa 4 usiku, nikampokea usingizini tukasalimiana mwisho akaniambia eti " dada nimesikia jpm kafa? Nikasema mama hao waongo.
Nilienda chumbani nikalala mida kama ya saa 6 kasoro naona shoga yangu wa moro ananipigia, bila hata salama nikasikia, " wewe unalala hovyo wakati raisi kafa? Yesuuuuuuu, usingizi ukikata nikamjibu, wewe ni uzushi uko mitandaoni, akasema washa tv samia anatangaza.

Fasta nikaingia insta nikakuta samata kapost yesuuuuu nilipiga kelele, na ninavyoishi mwenyewe, nikaanza kupigia watu nikiuliza.

Nikaona haitoshi, kuna ndugu yake jpm namjua nikampigia alivyopokea simu kwa muda ule nilijua tiyari, nilibaki tu napiga ukunga, kila ninaempigia yupo hewani watu wanalia aiseee.

Nakili magufuli nilikuwa namkubali kawaida tu ila sijui baada ya kusikia kifo chake yale maumivu yalitoka wapi yaan utadhani mimi ndugu yake. Nililia sana.

Kuna fala mmoja akanipigia najua hampendaji jpm, nikapokea nikasikia kicheko nikakata simu nikamblock. Siku mbili baadae akanitafuta kwa no nyingine nilimchamba hakuamini. Akinipigia siku hizi lazima awe na adabu sina hasara hata asipokuwa rafiki yangu.

Magufuli ulijua kuniumiza jamani.

RIP JPM.
HAdi nimepata simanzi jinsi ulivyoelezea, best president ever he was
 
Back
Top Bottom