Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,807
- 11,969
Leo ni Maadhimisho ya Mwaka mmoja tangu Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli atukote. Maadhimisho hayo yanafanyika mkoani Geita katika wilaya ya Chato.
Maadhimisho hayo yatahudhuriwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia suluhu, Makamu wa Rais Dkt. Isdori Mpango, Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi na viongozi mbalimbali wa serikali ya Jamuhuri.
Pia soma
1). TANZIA - Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
2). Historia ya Dkt John Pombe Magufuli
===
UPDATES;
====
“Mh.Rais nilikupigia simu lakini kwa bahati mbaya sikukupata lakini baadae ulinipigia na nikakuomba uhudhurie shughuli hii ukakubali na uliniahidi kuwa utakuja japokuwa sikuomba kwa maandishi lakini umekuja,ASANTE SANA Umeniheshimu Sana MAMA,”-Mama Janeth Magufuli
"Tunakuombea Mungu akupe nguvu ya kuendelea kuongoza Taifa vema na Mungu azidi kukulinda akupe maisha marefu,"- Mama Janeth Magufuli
“Ni imani yangu Dini zote tumefundishwa kushukuru kwa kila jambo naomba muungane nami katika kumshukuru Mungu, tunamshukuru Mungu kwa Neema zake kwani ilimpendeza kujifunza mema mengi kutoa kwa Hayati Magufuli hakika tutayaishi na kuyaenzi daima,"-Mama Janeth Magufuli
Askofu Kasala awataka Watanzania kusimamia ukweli, haki
Picha: Askofu Flavian Kasala
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Flavian Kasala amewataka Watanzania kusimamia ukweli na haki katika kumuenzi Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli.Picha: Askofu Flavian Kasala
Askofu Kasala ametoa rai hiyo leo Alhamisi Machi 17, 2022 kwenye ibada ya misa ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati John Magufuli inayofanyika katika uwanja wa Magufuli Chato.
Amesema Hayati Magufuli alisimamia ukweli na kile anachokiamini hivyo kuwataka wananchi na viongozi kushuhudia ukweli huo katika maisha yao.
“Tukisimamia ukweli na haki, marehemu wetu wanazo dhawabu walizoondoka nazo, tuko tayari kuyachukua hayo kuwa kama dira ya maisha yetu? amesema
Askofu Kasala amesema kila mmoja kwa nafasi yake awe na kiu ya haki katika maisha na kujitoa kuietea.
“Njaa ya haki ni pale katika ubinadamu wako unaposema siwezi kushuhudia kuona mtu akiwa anaonewa, ananyanyaswa na kudhulumiwa,
Maudhi kwa ajili ya haki yanakuja pale tu mmoja anaposimamia haki bila kijibakiza na kusimamia haki ni kujitoa sadaka lakini bora niudhiwe lakini haki itendeke” amesema Askofu Kasala
Amewataka wananchi kuzidi kumombea toba kwa Mungu Hayati Magufuli
"Tunapokua kwenye ibada hii tunapaswa kukumbuka huyu alikua kiongozi wetu na kuna mema mengi alitenda akiwa na sisi na kama imani ya kanisa inavyo tuambia tuendelee kumuombea toba ili Mungu ampokee mbinguni" amesema Askofu Kasala.
Ibada hiyo imehudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hasani na viongozi mbalimbali wa Serikali, taasisi, wastaafu na wananchi.
Viongozi wengine waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hassein Mwinyi na mkewe pamoja na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Philip Mpango.
Wengine ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson, Waziri wa Ardhi, Angelina Mabula, Waziri wa Tamisemi, Inocent Bashungwa, Mbunge wa Jimbo la Ismani, William Lukuvi pamoja na Balozi Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole.
Pia wapo viongozi wastaafu wakiwamo Makamu wa Rais wa awamu ya nne, Ghalib Bilali, mawaziri wakuu wastaafu Joseph Warioba na Mizengo Pinda.
Wengine ni aliyekuwa Spika wa Bunge, Anna Makinda mke wa Rais wa awamu ya tatu hayati, Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa.
Wakati wa ibada hiyo ikiendelea mvua kubwa imenyesha huku mamia ya wananchi waliopo kwenye uwanja huo wakiendelea kushiriki kwenye ibada.
Baada ya ibada Rais, viongozi pamoja na familia wataambatana kwenda kwenye kaburi la Hayati Magufuli kwa ajili ya kuweka mashada ya maua.
Rais Samia mema yote yaliyoachwa na Hayati John Magufuli yataendelezwa
Picha: Rais Samia
Picha: Rais Samia
Rais Samia Suluhu Hassan amesema mema yote yaliyoachwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli yataendelezwa.
Ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 17, 2022 alipokuwa akitoa salamu za taifa katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa kumbukizi ya kifo cha hayati Magufuli.
Rais Samia ameyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na nidhamu, uadilifu na kupiga vita ubadhilifu.
"Hivi karibuni tutafungua daraja la Tanzanite lililoko jijini Dar es salaam hii ilikua ndoto ya Magufuli na nitaiendeleza kwa kuboresha huduma za maji, umeme na miundombinu"amesema Samia
Akizungumzia miradi iliyopo Geita, Rais Samia amesema mradi wa kivuko cha Chato-Nkome kilichogharimu Sh3.1 bilioni umekamilika.
Aidha mradi wa kituo kikuu cha mabasi unaojengwa kwa Sh13.2 bilioni umekamilika kwa asilimia 92 na kuahidi kuendelea kutoa fedha ili ukamilike kwa asilimia 100
Samia amesema mambo yote hayo yatawezekana kama watanzania wataendelea kuimarisha mshikamano.
"Sisi wanadamu hatuwezi lolote bila msaada wa mwenyezi Mungu".
Awali Makamu wa Rais wa Tanzania, Philip Mpango amesema Magufuli alikua mwalimu wake aliyemfundisha kumtegemea Mungu nyakati za shida.