Wakati wa mfumo wa chama kimoja CCM ilikuwa ikimiliki mali karibia kila kona ya nchi hii, mpaka leo hii binafsi sijui vyanzo vya mapato ya upatikanaji wa mali hizo. Huwa najiuliza tu km vyanzo ilikuwa ni kodi kutoka kwa wananchi (enzi zile) basi kwa nini mali hizo zisirudi serikalini baada ya mfumo wa vyama vingi. Waswahi wanasema mwenye pesa si mwenzako, hii kauli inathibitishwa na yanaayoendelea hivi sasa. Akili za kuambiwa changanya na zako. Naomba mwenye kujuwa vyanzo vya mapato vilivyosababisha upatikanaji wa mali hizo atupe ufafanuzi. Hapo chini ni moja kati ya kitega uchumi cha chama hicho ambapo pia kuna ofisi kuu ya chama hicho Shinyanga.