Ulipaji wa kodi kwa kampuni mbalimbali hapa Tanzania.

MZAWATA

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
556
95
Kampuni mbalimbali zinazofanya biashara tofautitofaut kwel zinalipa kodi kulingana na kile wanachopata? Nahamasika kulizungumzia hili suala kwa kuwa tuna utitir wa makampun hapa Tanzania lakin nina wasiwasi na ulipaj wao wa kodi. Naomba wadau mnielimishe zaidi juu ya hili suala.
 
Sio makampuni tu hata sisi wananchi wa kawaida ni wangapi tunalipa kodi kwa vipato vyetu vyote kama sheria inavyotaka? Wengine wanalipa kodi kwenye mishahara tu lakini unakuta mtu huyo huyo ana vipato vingi tu vya ziada ambavyo halipii kodi. TRA wangekuwa makini wangeweza kuanzia kwenye mali watu wanaozimiliki kuweza kuassess possible incomes zao!
 
nafikiri kuna tatizo katika sera zetu pamoja na mitizamo ya wengi katika suala la kodi kwa maendeleo ya nchi yetu.Pia sheria za kodi hazijaweza kufikia malengo ya kodi kwa maendeleo. Bado kuna mianya mingi na pamoja mtizamo wa ulipaji kodi kwa hiyari. Mrusho nyuma wa kodi zinazolipwa pia hazitoi ushawishi watu kulipa zaidi. Tujiulize je hata wachache wanaolipa ni kwa sababu wanajua umuhimu wa kulipa ama ni kwa vile hawana njia ya kukwepa?
 
Mfano mzuri ni vodacom ambao wanajisifu wana wateja zaidi ya mil 10 lakini katika large tax payers wanapitwa na airtel, na hapo ndio inadhihirisha wazi kuwa hawalipi kodi ipasavyo
 
Makampuni makubwa mengi hayalipi kodi na kama wanalipa haizidi 20% ya kiwango wanachopasya kulipa,mfano mzuri ni makampuni ya simu,madini,na viwanda vya Mohamend ent,Zakari na wengine hawa wanashinda kwenye corridor za TRA kuomba misamaha pia na kutoa fake decrelations fake kukwepa kodi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom