Ulipaji kodi; Kwanini wafanyabishara wanawakimbia TRA?

Jul 2, 2015
18
6
Naomba kuulizwa wapendwa

Kumekuwa na tabia ya wafanya biashara wa maduka kuwakimbia maofisa wa TRA au wakisikia wapo jirani wanafunga maduka yao

Je nn kinafanya wakimbie?

Au kuna unyonyaji wowote,, na unawezaje mshauli mtu wa namna hiyo
 
Huenda kinachowafanya wakimbie ni malimbikizo ya kodi..unakuta ana madeni ya kutosha au mwenendo wa biashara yake sio mzuri kwa hiyo kulipa kodi inakuwa majanga
 
Wapo wengine wanafuata mkumbo tuu... lakin tabia hii ya kuwakimbia maogisa wa TRA ni ushamba... jambo la muhimu ni kuweka mambo yako sawasawa kulipa kodi hapo inakuwa pouwa na wala hautakimbia tena na tena....
 
Wangetuwekea sheria kwamba maofisa wa TRA wakipita na wakakuta umefunga wanakupa maelezo ya kwenda ofisini kwao kwa ajili ya maelezo kidogo na ingekuwa kila mteja wanakuwa na namba zao za simu ukifika unapiga simu kama haupo
 
Wapo wengine wanafuata mkumbo tuu... lakin tabia hii ya kuwakimbia maogisa wa TRA ni ushamba... jambo la muhimu ni kuweka mambo yako sawasawa kulipa kodi hapo inakuwa pouwa na wala hautakimbia tena na tena....

Wengi ni kweli unakuta biashara hazijachanganya lakini hata zikija changanya hayo mazoea ya kuwakimbia TRA yanakuwa yameshakuwa tabia
 
Wapo wengine wanafuata mkumbo tuu... lakin tabia hii ya kuwakimbia maogisa wa TRA ni ushamba... jambo la muhimu ni kuweka mambo yako sawasawa kulipa kodi hapo inakuwa pouwa na wala hautakimbia tena na tena....

Naungana na sechex.Nachofahamu kodi hutozwa kwenye mauzo gafi kwa wale wa mauzo kati ya 4m mpaka 20m kwa mwaka na zaidi ya 20m kwenye faida.sasa sioni sababu ya kukimbia hao TRA kama kweli kumbukumbu zako zipo vizuri.tatizo haturekodi mauzo yetu ndiyo maana, mm hata sasa hivi waje hao sijui ni TRA siogopi kwani najua nilichouza na siwezi kimbia kwani hata kodi najua ntalioaje.nashukuru niliwakuta wakati wa sabasaba mwaka jana banda la wizara ya fedha nikataka jifunza wanavyokokotoa kodi na kupata elimu hiyo.ndiyo maana natengeneza hesabu sitaki shida
 
Back
Top Bottom