Ulinzi waimarishwa taasisi ya moyo alikolazwa Manji

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,388
24,947
Hali ya ulinzi imeimarishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikolazwa mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya kuugua ghafla akiwa polisi alikokuwa akihojiwa.

Manji aliyekuwa akihojiwa katikaKituo Kikuu cha Polisi jijini hapaalipelekwa hospitalini hapo juzi jioni akiwa ndani ya gari la wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser lenye nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)huku gari lake aina ya Range Rover likifuata kwa nyuma.

Mwandishi wa Mwananchi aliyeweka kambi katika taasisi hiyo aliwashuhudia askari wenye sare na wengine wakiwa na mavazi ya kiraia nje ya wodi aliyolazwa mwenyekiti huyo wa klabu maarufu nchini ya Yanga.Ilipofika saa 4:13 asubuhi mfanyabiashara huyo alitoka kwenye chumba hicho na kuongozwa kuelekea upande mwingine wa jengo hilo.

Akiwa amevalia nguo za wagonjwa zenye rangi ya kijani, Manji alitembea taratibu kuelekea upande aliokuwa akielekezwa.

Alipoulizwa kuhusu uwapo wa Manji hospitalini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema hawezi kuzungumzia taarifa za mgonjwa.

Februari 8, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa orodha ya watu 65, akiwamo Manji ambao aliwataka wafike Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu masuala ya dawa za kulevya.

Chanzo: Mwananchi Online
 
Chanzo : Mwananchi Online
Mmm yetu macho sishangai kusikia hatunae!!maana hii dunia..... ngoja nikae kimya!!
 
Lakini hawa akina Manji si ndio wanaowapa ccm pesa za rushwa wakati wa kampeni kwanini wanamtesa hivi au Magufuli ana amino atatumia jeshi na polisi kushinda uchaguzi ? Make ccm ikifika nyakati za chaguzi wanakusanywa akina mama 200,wanapewa milioni mbili,wanaita vicobaccm
 
2020 wahindi wa tz watabadili gia angali, wametumikishwa sana kwa miaka mingi wakilazimishwa hata kutoa hela za kampeni bila wao kupenda, lakini nahisi uchaguzi ujao watafanya maamuzi sahihi kwasababu bila hivyo, wachache sana watabakizwa.
 
Lakini hawa akina Manji si ndio wanaowapa ccm pesa za rushwa wakati wa kampeni kwanini wanamtesa hivi au Magufuli ana amino atatumia jeshi na polisi kushinda uchaguzi ? Make ccm ikifika nyakati za chaguzi wanakusanywa akina mama 200,wanapewa milioni mbili,wanaita vicobaccm
"Hata akiwa mke wangu mkamateni." Statement hii inaonyesha how serious the President is about the war on drugs.
 
Back
Top Bottom