Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Faragha: Usimpige Picha wala kumchukua Video karani wa Sensa bila ridhaa yake

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Wakati zoezi la Sensa ya Watu na Makazi likiendelea, ni vema kukumbushana kuwa Faragha ya Mtanzania yeyote, akiwemo Karani wa Sensa, ni kitu muhimu sana katika nyakati hizi

Picha na Video za Makarani zimekuwa zikisambazwa mitandaoni hivyo, tungependa kuukumbusha umma kuwa suala la faragha na ulinzi wa taarifa zao na zetu ni jukumu letu sote

Tunaendelea kusisitiza umuhimu wa Tanzania kuweka Sera na Mifumo imara ya ulinzi wa taarifa binafsi na faragha za Wananchi wake

Je, Katiba ya Tanzania inasemaje kuhusu Ulinzi Wa Taarifa?

Ibara ya 16 (1) inaeleza: Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi, maisha binafsi na familia na unyumba wake, heshima na hifadhi ya maskani na mawasiliano yake

Ibara ya 16, (2): Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa Sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho Haki ya mtu ya faragha, usalama wa nafsi yake, mali na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri Ibara hii
 
Unadhani hapa hawa makarani walipiga kwa ridhaa?
20220823_162752.jpg
20220823_162659.jpg
20220823_162632.jpg
 
Back
Top Bottom