Ulinzi wa Raisi Kikwete.....!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulinzi wa Raisi Kikwete.....!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sajenti, May 26, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tangu Raisi kikwete alipokuwa katika harakati zake za kugombea uraisi kulikuwa na matukio ya hapa na pale kuhusiana na ulinzi wake kwa ujumla. Wengi tunakumbuka tukio la kikwete kuvamiwa jukwaani kule Mwanza, jaribio la msafara wake kurushiwa mawe kule mbeya, na juzi hapa Dar msafara wake kukumbwa na matukio ya gari kuharibika mara mbili kwa mtazamo wangu naona ni hatari....Najiuliza je, ni kuwa walinzi wa raisi hawajui wanachofanya? au kuna uzembe ndani ya idara ya usalama katika kumlinda raisi? Sitashangaa hali hii siku moja ikasababisha maafa kwani udhaifu tunaouona si jambo jema kabisa.....:fencing:
   
 2. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2010
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Sajenti achilia mbali gari kuzimika mara mbili; Taarifa zinasema kuwa gari hiyo ambayo rais alilazimika kushuka baadaye ilichomoka Tairi! Na kama vile kuthibitisha kukosekana umakini wa walinzi wake, ilielezwa Raisi allilazimika kulowa na mvua alipokuwa akielekea katika gari nyingine.

  Mi nadhani nchi sasa tumefikia mahali ambapo hakuna tena mambo ya muhimu...kila kitu ni cha kawaida tu
   
 3. m

  mpuguso Member

  #3
  May 26, 2010
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nchi sasa inaendeshwa kienyeji (Kitine,2009)
   
 4. hope 2

  hope 2 Senior Member

  #4
  May 26, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani ni watu wangapi wanaloa kwa mvua?

  walinzi wake wanafanya mambi kienyeji kama yeye alivyo na anavyofanya kienyeji.
  Kawaida hata watoto wanatenda kuendana na waubwa/wazazi wanavyotenda, ywyw mwenyewe kiutendaji hayupo makini hivo walio chini yake hali kadhalika
   
 5. hope 2

  hope 2 Senior Member

  #5
  May 26, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sure
   
 6. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwa hii pathetic performance ya walinzi, likitokea la kutokea conspiracy theorist watazuka bado na kusema ooh imekuwa hivi au vile. Kwa mtu kama rais makosa ya wazi kama hayo ni jambo la hatari kabisa kwani yapo mengi ambayo hayaonekani. Ukishaona makasa ya wazi yanatokea hivyo ujue seriosly kuna tatizo kwenye hizo organizations zinazohusika.

  Rais analindwa na watu tunaoamini ni makini kuliko watu wengi sana nchi hii. Eneo la ulinzi wa rais ni eneo ambalo makosa yake yanaweza kuangamiza nchi mara moja. Fikiria kuanguka kwa ndege kule Rwanda kuliko sababisha kifo cha rais wa Rwanda ilivyo trigger balaa na maangamizi!! Ulinzi wa rais si kitu cha kuchezea na inatakiwa wahusika watoe maelezo kwa wananchi. Watanzania inatakiwa tudai maelezo ya kina hasa.

  Nchi zetu hizi bado ni nchi dhaifu sana. Watu wake bado tunaakili ambazo hazijakomaa hata kidogo. Likitokea la kutokea matokeo yake hakuna anayeweza kutabiri. Lakini lililo wazi kwa Afrika ni kuwa mabadiliko ya uongozi yasiyotarajiwa au ya ghafla sana ni jambo la hatari mno. Uzoefu unaonesha hivyo.

  Watu wanapofanya uzembe kwenye suala la ulinzi wa kiongozi wa nchi kama rais, hicho ni kilele cha utovu wa nidhamu. Ni kilele cha uzembe na kutojali. Hakuna maelezo yoyote yanayoweza kutolewa ni kwa nini gari ya rais izimike ghafla barabarani. Tena ichomoke tairi!!!!!

  Mabalaa huikumba jamii yoyote pale watu wake wanapoamua kuangalia maovu yakitokea na kukaa kimya. Hili la kuzembea ulinzi wa rais ni kubwa kuliko ufisadi wowote uliokwisha ikumba nchi hii. Lazima tutake maelezo toka kwa wahusika!!
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mkuu Hope na wengine nimefurahi angalau nanyi imeonyesha kuguswa na hili tatizo la ulinzi dhaifu wa kiongozi mkuu wa nchi. Hivi ni naini hasa anapaswa kuwawajibisha hawa watu wanaofanya uzembe wa wazi katika ulinzi wa kiongozi wa nchi?? Sidhani Raisi kama yeye anatakiwa kufanya hilo lakini bado naye pia anaweza mahali fulani akachukua hatua kama vile kumuwajibisha mkuu wa idara ya usalama wa Taifa. Nina imani mambo haya yanayotokea hapa kwetu ni wazi yangetokea katika nchi za wenzetu walioendelea vichwa vingi vingewajibika..Sijui Tanzania ni kuchukulia mambo kwa mazoea au kuna ajenda ya siri???
   
 8. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nadhani wakati mwingine matatizo anayoyapata RAIS anajitakia mwenyewe kwa kuteua watu wasiofaa kumsaidia kazi. Nanukuu kauli ya ajabu ya Salva Rweyemamu alioona kwamba hakuna ajabu kwa mkuu wa nchi kupata matatizo yakizembe aliyoyapata"Ndugu yangu yaani ninyi mnaona taarifa za matatizo ya kawaida ya magari aliyoyapata Rais ni muhimu kuliko adha za maji ambazo alikuwa akikagua katika jiji la Dar Es salaam?" Mwisho wa kunukuu. Mimi naamini ili Rais amalize kero za maji anatakiwa awe katika usalama wa hali ya juu anapofanya kazi zake.
   
Loading...