Ulinzi wa Rais: Nini athari ya picha zinazopigwa na wananchi?

ngokuro

Senior Member
Mar 15, 2017
118
98
Kwa baadhi ya ziara za Mhe. Raisi wa JMT nilizoshuhudia hususan nilizokuwepo eneo la tukio, nimeona wanausalama katika misafara hiyo wakikataza Raia kuchukua picha mnato au mjongeo.

Aidha endapo afisa usalama atakuona ukiwa umeshapiga picha atakushurutisha ufute pocha hiyo ktk simu yako au kamera.

Kuna athari gani kwa muhusika au msafara endapo raia wataachwa wakachukua picha?.
 
Kwa baadhi ya ziara za mh.Raisi wa JMT nilizoshuhudia hususan nilizokuwepo eneo la tukio, nimeona wanausalama ktk misafara hiyo wakikataza raia kuchukua picha mnato au mjongeo.

Aidha endapo afisa usalama atakuona ukiwa umeshapiga picha atakushurutisha ufute pocha hiyo ktk simu yako au kamera.

Kuna athari gani kwa muhusika au msafara endapo raia wataachwa wakachukua picha?.
Ujinga mtupu, Kama wanaogopa kupigwa picha, Basi hawajabobea ktk usalama,
Ofisi za CIA, FBI, NSA, Scotland yard, mi6, uko Ulaya na Marekani, zinajulikana zilipo na wakuu wa hivi vyombo wanajulikana, huku kwetu Bado ushamba mwingi,

Unakatazwa usipige picha kambi ya jeshi,wakati kwenye google map unaipata vzr tu
 
Huo ni uoga tu wa wana usalama. Na mtu mwenye nia madhubuti ya kumdhuru wala hatohangaika kutumia simu kupiga picha. Spy cameras zipo za kutosha.

Hata hivyo ni kweli kuwa picha zina nafasi kubwa katika kuonyesha udhaifu na uimara katika kikosi cha ulinzi na namna kilivyojipanga.
Una mawazo ya kizamani sana sana. Picha zionyeshe udhaifu au uimara wa kikosi cha ulinzi cha rais? Hivi anayepiga picha na aliyepo kwenye tukio akiangalia kwa macho yake, hatua na nyendo zote ni nani anaona mambo kwa kina? Unafikiri mtu mwenye nia mbaya atakwenda kushika simu na kupiga picha?
 
Naomba nikiri kabisa kuwa ninacho kijibu hapa najaribu tu kubuni na kutoa mawazo yangu mwenyewe, nikwamba,
Picha au video zina athari kubwa sana kiusalama kama mtu akiamua kufanya mbaya, watu wabaya wanauwezo wa kutumia picha kuset mipango yao mfano Kama rais ana takiwa adunguliwe wakora watakuwa walisha soma ulinzi mzima hukaaje kila siku au kila wiki, pia ikitokea usalama umeharibika ghafla mfano Rais kafa mkutanoni anaepaswa kutoa taarifa kwa wananchi atawahiwa na waliorekodi video au kupiga picha wakati siyo sahihi kwa raia kutoa hizo taarifa kabla ya mamlaka, mamlaka huwa Wana wajibu wa kuzipika taarifa kwanza ndiyo wazitoe hadharani kwahiyo watashindwa kuzipika taarifa kwasababu wewe uliyechukua video au picha utakuwa umerusha kwa raia hivo utaleta mkanganyiko kwa Jamii na serikali, kwa hisia tu hili suala la kuzuia picha na video nahisi lilianzia kipindi John F Kenedy alipopigwa risasi na Bwana Osward Lee, mtu pekee aliyekuwa anachukua video Kwenye msafara alikuwa mmoja tu Bwana Zapruder naye alikuwa anachukua video kwa mapenzi yake tu hakutumwa na mtu, jamaa alikamatwa na camera yake kwaajili ya kuisaidia polisi na video yake ipo hadi Leo Ila ilimpa shida Sana hadi walimuua kwa sumu iliyosababisha cancer ya tumbo Kama sikosei, kwahiyo kutokana na video ya Zapruder iliwawia vigumu serikali kupika taarifa.

Sababu nyingine ni kwaajili ya kukulinda wewe mpigaji ikitokea rapsha kiongozi akafa mkutanoni na wewe una video au picha utajumuishwa Kwenye wahusika wa mauaji kuisaidia polisi kumbe hata hukuwa na nia mbaya kwahiyo serikali inakukataza kwakukulinda na majanga, pia kumbuka si kila mwandishi wa habari pia anaruhusiwa kupiga picha au kuchukua video nao mpaka wawe wameruhusiwa na kuna mpiga picha wa serikali pia ndo anatakiwa afanye hiyo kazi ndiyo maana unaweza kuona taarifa ya habari kituo flani kinaonesha tukio la rais mwanzo mpaka mwisho ukitizama tena kituo x utaona mfanano 100%. Kwahiyo tuwe wapole tu jamani.

Nimawazo tu wajuaji watatujuza zaidi
 
Una mawazo ya kizamani sana sana. Picha zionyeshe udhaifu au uimara wa kikosi cha ulinzi cha rais? Hivi anayepiga picha na aliyepo kwenye tukio akiangalia kwa macho yake, hatua na nyendo zote ni nani anaona mambo kwa kina? Unafikiri mtu mwenye nia mbaya atakwenda kushika simu na kupiga picha?
Sikujua mkuu kama nina mawazo ya kizamani. Nashukuru umenijuza.

Lakini kwanza elewa mtoa mada hakutanabaisha kama ni picha mnato au picha za mwendo (video). Lakini vyote kwa pamoja zina nafasi kubwa katika kueleza ni kwa naoa gani kikosi kimejipanga. Na loopholes ambazo adui anaweza kuzitumia kudhuru. Wewe unaona picha, mwenzako anaona upenyo wa kutimiza lake.
 
'Nimetanabaisha' chief rudia kusoma pharagraph ya kwanza!

Kusema mawazo ya kizamani ninamaanisha kuwa siku hizi dunia imeendelea na polisi kukataza watu kupiga picha kwa mtu anayeonekana kwa macho na kwa kila mtu ni ujuha tu. Wewe umeonyesha kama kuwaunga mkono kwa namna moja.
 
Una mawazo ya kizamani sana sana. Picha zionyeshe udhaifu au uimara wa kikosi cha ulinzi cha rais? Hivi anayepiga picha na aliyepo kwenye tukio akiangalia kwa macho yake, hatua na nyendo zote ni nani anaona mambo kwa kina? Unafikiri mtu mwenye nia mbaya atakwenda kushika simu na kupiga picha?
Upi ni mtazamo wako chief?

Kwann 'raia' hukatazwa kuchukua picha maeneo aliyopo no 1?
 
Ujinga mtupu, Kama wanaogopa kupigwa picha, Basi hawajabobea ktk usalama,
Ofisi za CIA, FBI, NSA, Scotland yard, mi6, uko Ulaya na Marekani, zinajulikana zilipo na wakuu wa hivi vyombo wanajulikana, huku kwetu Bado ushamba mwingi,

Unakatazwa usipige picha kambi ya jeshi,wakati kwenye google map unaipata vzr tu
mambo hayaendi hivyo aisee, hata huko unakotaja hukujui vyema.

si kila wakati utaruhusiwa kupiga picha unachotaka, mfano hiyo google unazungumzia kwa kukudokezea, ukijaribu kufanya shambulizi sehemu nyeti kwa kutumia picha za google nchi yoyote tu, unakosa target, zimefanyiwa maneuver makusudi kiusalama ili kutoingilia uhuru wa nchi husika. nenda hapo US kaombe pcha za area5 kama utapewa,au nenda makao makuu ya MI5 kisha anaza kupiga picha tu uone nini kitatokea.

picha si kwa ajiri ya ku expose tu muonekano wa mtu au vitu, ila zinatumika kuchora ramani.
 
Mbona mmarekani anakataza kupiga picha ubalozi wake hapa bongo?
 
Unazungumzia sehemu nyeti na eneo hilo halihami,

Rais anafanya mkutano kwa muda kisha anaondoka eneo hilo ila anapokuwa eneo hilo huruhusiwi kuchukua picha

Kuna athari gani?!
mambo hayaendi hivyo aisee, hata huko unakotaja hukujui vyema.

si kila wakati utaruhusiwa kupiga picha unachotaka, mfano hiyo google unazungumzia kwa kukudokezea, ukijaribu kufanya shambulizi sehemu nyeti kwa kutumia picha za google nchi yoyote tu, unakosa target, zimefanyiwa maneuver makusudi kiusalama ili kutoingilia uhuru wa nchi husika. nenda hapo US kaombe pcha za area5 kama utapewa,au nenda makao makuu ya MI5 kisha anaza kupiga picha tu uone nini kitatokea.

picha si kwa ajiri ya ku expose tu muonekano wa mtu au vitu, ila zinatumika kuchora ramani.
 
Kwa baadhi ya ziara za Mhe. Raisi wa JMT nilizoshuhudia hususan nilizokuwepo eneo la tukio, nimeona wanausalama katika misafara hiyo wakikataza Raia kuchukua picha mnato au mjongeo.

Aidha endapo afisa usalama atakuona ukiwa umeshapiga picha atakushurutisha ufute pocha hiyo ktk simu yako au kamera.

Kuna athari gani kwa muhusika au msafara endapo raia wataachwa wakachukua picha?.

Actually nikiangalia video namna wanavolinda kiongozi flani na kulingana na movie nilizoangalia naona hakuna wa kunizuia
 
Back
Top Bottom