Ulinzi wa Rais ni kitu cha kwanza katika Taifa lolote lile

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,173
27,223
Katika kipindi fulani hivi kuliibuka watu ambao wanaotumiwa vibaya na wanaotumiwa na maadui wa Taifa hili wakawa wana-question sana ulinzi wa Rais, mara ooh mbona analindwa sana mara oooh mbona anatembea na gari la machuma chuma.

Anatembea na Askari wana mi-bunduki, mara analindwa kuliko kim jong un, hizi zote ni siasa za kutaka kutoa sytem nje ya reli.

Rais hata awe mzuri kiasi gani ni lazima atakuwa na maadui ambao 24/7 wanawaza kumdhuru, na sio Rais tu hata viongozi wengi huwa wana maadui hata ufanyaje.

Mama Samia ni sahihi kutumia kila aina ya ulinzi anaoona unafaa kama ilivyo kwa mtangulizi wake. Maana vijana wa ufipa walianza ooh ngoja tuone kama lile gari la machumachuma juu litakuwepo, mara ooh ngoja tuone kama wale wanajeshi wanaovaa bunduki watakuwepo.

Walipoanza kuona ulinzi upo vilevile wakanuna wakaja na maneno mengi ya kuonyesha eti CCM ni ile ile. Rais hajipangii ulinzi Bali anapangiwa, na hata Rais atayekuja bado atatumia hilo gari na hao Askari

Screenshot_20210707-155555_1.jpg
Screenshot_20210501-120153_1.jpg
 
Likitokea la kutokea, hao hao watakuja kuwapopoa mawe wanaohusika na ulinzi wa Rais........yaani hadi povu la njano litoke mdomoni.
 
Dikteta alikuwa na kila aina ya ulinzi lakini now anaoza peke yake kawaacha walinzi wake, ulinzi wa kweli watoka kwa MUNGU wa mbinguni, tenda mema na MUNGU atakulinda. Lissu risasi 38 lakini bado yupo hai aliyeagiza apigwe hizo risasi kafa kifo kibaya.
Wewe ukipewa kazi hiyo ni ulinzi wa namna gani utakaoweka, tuanzie hapo kwanza.....hivi unaweza kuaminisha watu ikitokea shida kwamba ulikuwa umemwekea rais ulinzi wa Mungu? hahaha...wewe jamaa bhana.
 
😂😂😂😂😂😂 JPM mlimsema sana kuwa analindwa mpk na wanyarwanda haya tuambieni hawa ni Wapemba au Waunguja?

Ulinzi wa nchi na uimara wa nchi unaanzia kwa Ulinzi wa Rais , Ulinzi wa Kiongozi wenu ndo unamake statment ya Ulinzi na utayari wa nchi ,hata maadui zenu inawapa taarifa jinsi gani mko tayari na umakini mlionao

Ndo maana mataifa makubwa kama China,USA ,Russia wanawalinda viongozi wao kwa mbwembwe hii imekaa kisaikologia zaidi
 
Wewe ukipewa kazi hiyo ni ulinzi wa namna gani utakaoweka, tuanzie hapo kwanza.....hivi unaweza kuaminisha watu ikitokea shida kwamba ulikuwa umemwekea rais ulinzi wa Mungu? hahaha...wewe jamaa bhana.
Hawa watu hawaishi vizuri na jamii, watu wanalindwa na mitambo ya kisasa, umemuona Uhuru Kenyatta analindwa kiboya hivi? wajitahidi kutenda haki wasiwe na maadui wengi na jamii itawalinda, tenda haki sawa kwa wote uone jamii kama haitakulinda yenyewe, hata na sungusungu wanaweza kukulinda na maisha yakaenda vizuri.
 
😂😂😂😂😂😂 JPM mlimsema sana kuwa analindwa mpk na wanyarwanda haya tuambieni hawa ni Wapemba au Waunguja?

Ulinzi wa nchi na uimara wa nchi unaanzia kwa Rais kwanza Ulinzi wa Rais unamake statment hata kwa maadui zenu jinsi gani mko tayari na umakini mlionao
Mbona Uhuru anaenda kanisani na gari lake mwenyewe na anaendesha tena kuna hatari ya Alshababu? huyu mama utachukua nini kwake cha maana hata ukimuua?
 
Hawa watu hawaishi vizuri na jamii, watu wanalindwa na mitambo ya kisasa, umemuona Uhuru Kenyatta analindwa kiboya hivi? wajitahidi kutenda haki wasiwe na maadui wengi na jamii itawalinda, tenda haki sawa kwa wote uone jamii kama haitakulinda yenyewe, hata na sungusungu wanaweza kukulinda na maisha yakaenda vizuri.
Unaweza kukuta hizo ni protocol za kiulinzi tu, na yeye anamtegemea mungu wake........Nyerere aliwahi kusema atakaye muua yeye ni kichaa tu.....
 
Rais wenu muoga, anaogopa kunyolewa na Mdude? Maana sio kwa ulinzi huo, hapo hata Covid-19 haipenyi.
 
Mbona Uhuru anaenda kanisani na gari lake mwenyewe na anaendesha tena kuna hatari ya Alshababu? huyu mama utachukua nini kwake cha maana hata ukimuua?
Security detail yake ulifanikiwa kuijua mkuu? maana wewe ulichoshuhudia ni kwamba aliendesha gari kuelekea kanisani baasi, huna uelewa kuhusu ulinzi wake ulivyokuwa katika mazingira hayo. Kila nchi ina taratibu zake kwenye maswala ya ulinzi na usalama wa rais....
 
Mbona Uhuru anaenda kanisani na gari lake mwenyewe na anaendesha tena kuna hatari ya Alshababu? huyu mama utachukua nini kwake cha maana hata ukimuua?
"huyu mama utachukua nini kwake cha maana hata ukimuua"
Halafu wewe ni miongoni mwa watu wanaopiga kelele za katiba mpya. hata kama asingekuwa rais hii statement haiwezi kutolewa na mtu ambaye hana matatizo ya kisaikolojia.
 
Mbona Uhuru anaenda kanisani na gari lake mwenyewe na anaendesha tena kuna hatari ya Alshababu? huyu mama utachukua nini kwake cha maana hata ukimuua?
Ficha ujinga wako wewe kilaza unapomuona rais yoyote peke yaje jua nyuma yake kuna ulinzi wakutosha sio kila ulinzi uone watu wamevaa makoti na mawani meusi.
 
Back
Top Bottom